Kard.Zuppi mjini Moscow azungumza na Antonij kuhusu mzozo wa Ukraine
Vatican News
Matatizo ya kibinadamu yanayohusiana na mgogoro wa Ukraine yalikuwa katikati ya mazungumzo tarehe 15 Oktoba 2024, kati ya Kardinali Matteo Maria Zuppi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia na mjumbe maalum wa Papa nchini Urusi na Antony Volokolamsk, rais wa Idara ya Mahusiano ya Kikanisa ya Nje ya Upatriaki wa Moscow. Kwa njia hiyo katika siku ya pili ya utume wake ikiwa ni kwa mara ya pili nchini Urusi, ambapo alifika tareheOktoba 15 ili kuhamaisha muungano wa familia ya watoto wa Kiukraine na kubadilishana wafungwa, kwa nia ya kufikia amani inayotarajiwa, asubuhi Kardinali alikutana na Maria Llova-Belova, kamishna wa urais wa Urusi wa haki za watoto (walikuwa tayari wameonana katika utume wa Juni 2023) na kisha Antonij na wajumbe husika.
Mkutano kati ya Zuppi na Antonij
Mkutano wa Kardinali Zuppi pia ulijumuisha Balozi wa Vatican wa Shirikisho la Urusi, Askofu Mkuu Giovanni D'Aniello. Hii iliripotiwa na tovuti rasmi ya Upatriaki wa Moscow(Mospat.ru,) ambayo pia ilichapisha baadhi ya picha za mkutano ambao Kardinali Zuppi na Antonij waliweza kuonekana wamekaa nyuma kwenye meza kubwa. Kando ya mji mkuu, “Waziri wa Mambo ya Nje wa Upatriaki wa Moscow - ambaye alikuja Roma mara nne na alikutana na Papa Francisko kwa mkutano faragha - kulikuwa na makamu wa rais wa DECR, Archimandrite Filaret (Bulekov) na Askofu Mkuu Igor Yakimchuk.
Salamu kutoka kwa Patriaki Kirill
Antonij wa Volokolamsk alisalimiana na wageni kwa niaba ya Patriaki Kirill wa Moscow na Urusi Yote, kama tunasoma kutoka taarifa ya Upatriaki, ambayo inaripoti kwamba “Wakati wa mazungumzo pande hizo zilijadili matatizo ya kibinadamu kuhusiana na mzozo wa Ukraine, pamoja na masuala mengine yenye maslahi kwa pande zote.” Kardinali Zuppi na Antonij walikuwa tayari wameonana tarehe 29 Juni 2023, kama sehemu ya utume wa kwanza wa Kardinali huko Moscow (kituo cha pili kwenye ziara ambayo pia ilimwona huko Kyiv, Washington na Beijing). Mwenyeji wake alikuwa mjumbe wa wajumbe waliofuatana na Kirill katika mkutano na mjumbe wa Kardinali wa Papa kwamba “Tunashukuru kwamba Baba Mtakatifu alimtuma mjumbe wake huko Moscow,” Alikuwa amesema.
Mazungumzo na Kamishna Lvova-Belova
Na siku zote katika utume wake wa kwanza katika ardhi ya Urusi, Kardinali Zuppi, kati ya uteuzi wa kitaasisi, alikuwa amemwona Maria Llova-Belova, kamishna wa Rais wa Urusi Putin wa haki za watoto. Hata leo hii 15 Oktoba mkutano kati ya hao wawili ulirudiwa na yalikuwa mazungumzoya kujenga, kamishna mwenyewe aliripoti kupitia taarifa iliyowekwa kwenye chaneli yake ya Telegraph, akisisitiza kwamba ushirikiano na mjumbe wa Papa na Balozi wa Vatican katika Shirikisho la Urusi imekuwa. kuendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja.” Lengo la mazungumzo kati ya Kardinali Zuppi na Llova-Belova ni kuwarejesha nyumbani watoto wa Kiukreni walipelekwa kwa lazima nchini Urusi. Zaidi ya watoto 19,000, kulingana na serikali ya Kyiv. Kikundi kidogo tayari kimeunganishwa na familia zao, shukrani pia kwa njia ya upatanishi iliyofunguliwa na Vatican. Kazi inaendelea: “Tulijadili matokeo na mwingiliano zaidi kwa maslahi ya familia na watoto, ikiwa ni pamoja na kuunganishwa kwa familia kutoka rus ina Ukraine,” alituma kamishna akiripoti maelezo ya mkutano na kardinali. “Tunafanya hivyo kwa ushiriki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi. Tuliamua kuendelea kufanya kazi pamoja.”
Mkutano na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Bwana Lavrov
Kardinali Matteo Zuppi mara alipowasili Moscow, alikuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Bwana Sergey Lavrov, juu ya “ushirikiano katika nyanja ya kibinadamu katika muktadha wa mzozo wa Ukraine na masuala mengine kwenye nyanja ya kimataifa. Ujumbe kutoka kwa Wizara uliotolewa siku hiyo ulisisitiza juu ya “maendeleo yenye kujenga ya mazungumzo ya Russia na Vatican.”