2024.10.03 XV1 Sinodi inaendelea mjini Vatican. 2024.10.03 XV1 Sinodi inaendelea mjini Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kazi imeanza ya Sinodi.Oktoba 7,kufunga na kusali kwa ajili ya amani!

Wito wa kusitisha vurugu ulifungua kikao cha II cha Sinodi ya Maaskofu kama ilivyoelezwa tarehe 3 Oktoba 2024 katika mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi ya Vyombo vya Habari,Vatican.Miongoni mwa mada ni umuhimu wa Vikundi vya Mafunzo na nafasi ya wanawake katika Kanisa.Ushemasi nyakati hazijaiva.Kardinali Grech alithibitisha,kuwa washiriki wote watashiriki mipango ya amani ya Papa:Rozari na Siku ya Sala na Kufunga.

Na Isabella Piro na Angella Rwezaula – Vatican.

Amani, msamaha, jukumu la wanawake na mbinu ya vikundi vya kazi: hizi ndizo mada kuu zilizojitokeza Alhamisi, tarehe 3  Oktoba  2024 kutoka kwa mkutano wa waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa kazi ya kikao cha Pili cha Mkutano Mkuu wa XVI Sinodi ya Maaskofu  unaoendelea hadi tarehe 27 Oktoba 2024. Mkutano huoulifanyika katika Chumba cha Waandishi wa Habari cha Vatican mbele ya makatibu maalum wa mkutano: Padre Giacomo Costa,(JS) naMonsinyo Riccardo Battocchio; marais wajumbe wa Sinodi, Sr. Maria de los Dolores Palencia Gómez, wa Shirika la Mtakatifu Yosefu, Askofu Daniel Ernest Flores, wa Jimbo la Brownsville, Texas; Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Ruffini: kiroho na sala

Kwa njia hiyo akianza kueleza kuhusu tukio hilo, Dk Paolo Fuffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Msemaji kwa waandishi wa habari kuhusu Sinodi, alisema "Asubuhi tarehe 3 Oktoba 2024 ilitangazwa, kuwa watu 356 kati ya 365 walikuwepo katika Ukumbi wa Paulo VI, na wasemaji wa kila Kundi walichaguliwa. Kwanza ni vingele  vitano vya kazi pia vilianza, vilivyowekwa katika sura ya kwanza ya Instrumentum laboris (IL), moja kwenye “Misingi,” alieleza Dk. Ruffini. Na akiwakilisha aidha alikumbusha jinsi hali ya kiroho na sala zinavyochukua nafasi muhimu sana katika ukumbi na jinsi hali ya ulimwengu ilivyo vizuri katika akili na mioyo ya washiriki wote wa Sinodi, hasa kwa kuwa kati yao kuna wale wanaotoka katika nchi zilizo kwenye vita au katika hali ya mateso.” Kwa njia hiyo Dk. Ruffini alisema: “katika ufunguzi wa mkutano huo asubuhi, tuliomba kwa ajili ya amani, tukirudia maneno ya Papa aliyosema wakati wa sala ya  Malaika wa Bwana Dominika iliyopita kwamba: “Kila kitu lazima kifanyike kukomesha vurugu na kufungua njia za amani.”  Kwa upade wake Dk Ruffini, basi, alitoa msisitizo juu ya vikundi kumi vya kazi vilivyoanzishwa na Papa kwamba: “vinavyoratibiwa na Sekretarieti Kuu ya Sinodi, vinafanya kazi ndani ya mchakato wa sinodi na kazi yao sio nje ya njia ya sinodi

Papa Francisko na Dk Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano
Papa Francisko na Dk Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano

Padre Costa:vikundi vya kazi, maabara ya maisha ya sinodi

Padre Costa, kwa upande wake, alirejea kile ambacho Papa amekuwa akisema mara kadhaa, kwamba “Sinodi si mkutano wa Bunge, bali ni mahali pa kusikiliza na kuungana”. Aliongeza, sio “dalili ya kejeli, lakini ni uzoefu ulio hai. Sio bahati mbaya kwamba hali ya awali ambayo inaweza kuhisiwa darasani ni ya furaha sana, kuna furaha ya kukutana tena, na uwezo mkubwa wa kuzama kwa undani katika mjadala.” Padre Costa, kisha akikazia vikundi kazi,  na kusihi tuviangalie kama “maabara ya maisha ya sinodi" ambayo lazima yaungwe mkono na waamini wote, kupitia michango inayoweza kuwafikia hadi Juni 2025.” Kwa hivyo “sio tume zilizofungwa lakini ni vikundi vilivyo wazi, hafla ambazo tunajifunza kufanya kazi pamoja kama Kanisa shirikishi, wasindikizaji katika safari wasafiri wa kweli wa Sinodi, na jukumu la kufanya kazi ya mchakato wa sinodi ndogo  kuhusu baadhi ya mada zilizounganishwa lakini haziwiani na Instrumentum Labori.”

Tofauti za mbinu kati ya 2023 na 2024

Alipoulizwa na waandishi wa habari, Mjesuit  huyo alieleza tofauti ya mbinu kati ya kikao cha kwanza na cha pili cha Sinodi kwamba: “mnamo 2023, lengo lilikuwa kusikiliza mitazamo katika utofauti wao, historia za Kanisa"ambazo zilipaswa kuibuka. Na mnamo mwaka 2024, Mkutano huu una kazi nyingine: kumpatia Baba Mtakatifu, kama Kanisa zima, miongozo kama matunda ya njia iliyochukuliwa wakati huo huo, ili kuunda maelewano, na sio kuhofia.  Kwa kuongezea Padre Costa alisema “badala ya kufungua maswali, husaidia kutambua baadhi ya mambo ya kuchambua kulingana na mazungumzo ya kina ya kiroho na daima kuacha nafasi wazi, ili kuepuka kuishia yamefungwa.”

Monsinyo Battocchio: umuhimu wa wataalimungu

Kwa upande wa Monsinyo Battocchio alizingatia umuhimu wa msamaha, ambao ulijitokeza zaidi ya yote wakati wa mkesha wa toba ulioongozwa na Papa Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,  jioni ya siku ya Jumanne tarehe 1 Oktoba 2024: “maadhimisho  hayo, yalionesha mtindo, ufahamu wa maana ya kuwa Kanisa, kwa sababu ndugu mwenye dhambi si mgeni, bali ni mtu ambaye ni lazima kubeba mzigo wake ili kutekeleza njia ya uongofu ambayo wanahusika kila mtu. Sisi ni Kanisa kwa kadiri tunavyofikiwa na huruma ya Mungu” alisema Katibu maalum ambaye baadaye alichunguza jukumu la wataalimungu ndani ya mkutano. Akitoa shukrani kwa mchango wao wa thamani, Monsinyo  Battocchio aliakisi kazi yao ya kusikiliza kwa makini, kwa akili ya kitaalimungu kwa kile kitakachojitokeza kwenye mjadala ukumbini. Umuhimu wao pia unaoneshwa na ukweli kwamba meza zao za kazi, mwaka huu, zimewekwa katikati zaidi katika chumba hicho ikilinganishwa na 2023.

Sr. Palencia Gómez: hatua mbele kwa wanawake

Sr Palencia Gómez alizungumza juu ya uhuru mkubwa na shauku kubwa, akielezea jinsi ambavyo Mkutano huo “unaruhusu washiriki wake kutembea pamoja kwa kuzingatia uhalisi wa ulimwengu huu, ambao umekithiri, lakini ambao unapaswa kuzingatiwa kwa mtazamo wa  Mungu, Baba Yetu.” Ni kwa njia hiyo tu, “kiukweli, itawezekana kukua katika uzoefu halisi wa sinodi na utume.” Kisha akaulizwa na waandishi wa habari kuhusu nafasi ya wanawake katika Kanisa, mtawa huyo aliakisi matunda ambayo tayari yapo katika eneo hili katika mazingira na mabara tofauti. Kutokana na uzoefu wake katika Amerika ya Kusini, hasa, aliweza kubainisha jinsi maendeleo yamepatikana, kiasi kwamba “wajibu wa wanawake, karama zao, michango yao inazidi kutambulika katika Kanisa la Kisinodi.” Sr. Dolores pia alisisitiza uwezekano wa kujifungua kwa uzoefu mpya, kwa mapendekezo mapya ya kugundua na kutafakari hata zaidi katika jukumu la mwanamke.”

Juu ya Ushemasi wa kike

Mtawa huyo alisisitiza kuwa: “Tunaendelea hatua kwa hatua, lakini ni safari ambayo inaendelea, kwa wanawake wa kawaida na kwa wanawake waliowekwa wakfu. Pia ni juu yetu kujikomboa kutoka kwa mtindo wa kujisikia kikuhani kikuhani. Maswali kutoka kwa wanahabari pia yalihusu shemasi wa kike: kuhusiana na hili, wazungumzaji wa mkutano huo walikumbuka yale yaliyosemwa siku moja kabla  ukumbini na Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Kwa upande wake alieleza kuwa: “Wakati bado haujaiva, imesemwa, na ni vizuri mada hiyo ikachunguzwa kwa kina, katika safari ya kikanisa yenye uzoefu pamoja.”

Kisha neno jingine lilitolewana Askofu Flores, ambaye alieleza jinsi, ambavyo tangu kikao cha kwanza cha sinodi ya 2023, mambo mengi yamepevuka, kwa sababu “maisha ya Kanisa yamesonga mbele, kwa hiyo hatuko katika hatua sawa na mwaka jana. Kama miti, tunakua usiku, ikimaanisha ukuaji huonekana tu baadaye. Katika hotuba yake, pia alizingatia umuhimu wa ukimya, mada, hii, iliyochambuliwa katika tafakari iliyofanyika tarehe 1 Oktoba na Sr Maria Ignazia Angelini, kwamba ukimya siyo si kitu kitupu, lakini ni kama kitu kilichojaa ambako Neno linatoka. Ni sehemu ya msingi ya mtindo wa sinodi, kwa sababu inaturuhusu ufahamu wa kiroho wa ulimwengu unaojidhihirisha kwetu” alielezea Askofu Flores.

Mitazamo ya ndani huturuhusu kuona uso wa Kristo ulimwenguni

Jambo kuu pia katika tafakari yake ni uelewa wa mitazamo ya mahali, ambayo, alisema, si maadui wa ukweli, lakini huruhusu Kanisa kuwa na nidhamu na usikivu wa subira ambao huturuhusu kuwa na picha pana ya uso wa Kristo katika ulimwengu tunamoishi. Kazi ya Sinodi, ni kujaribu kutafuta sauti thabiti ambayo ni kielelezo cha sauti ya Kanisa, ya maisha yake leo, ya mang’amuzi yake. Kuna sisi ambayo ni ya msingi katika kazi ya sinodi na kwamba ni ya thamani zaidi kuliko umimi. Sinodi inatafuta kuwa 'sisi' ambayo ni watu wote kuwa' mali yake,'” Alihitimisha.

Mipango ya amani ya tarehe 6 na 7 Oktoba 2024

Hatimaye, kwa kutazama mipango miwili ya amani iliyotangazwa na Papa ya tarehe 6 na 7 Oktoba – sala ya   Rozari Takatifu huko Mtakatifu Maria Mkuu na Siku ya Kufunga na Kusali. Wasemaji katika mkutano wa waandishi wa habari walikumbuka kwamba washiriki wote katika Sinodi walialikwa kwenye tukio la Dominika  na kwamba siku ya Jumatatu mwendelezo wa kawaida wa kazi utashughulikiwa katika muktadha wa sala na kufunga.

Mhutasari wa Sinodi tarehe 3 Oktoba 2024
03 October 2024, 17:23