Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 9:kusikiliza,kimya na sala kwa kumbukumbu ya kuanza kwa Mtaguso
Na Roberto Paglialong,Edoardo Giribaldi na Angella Rwezaula-Vatican.
Tarehe 11Oktoba ni tarehe ya ukumbusho wa kufunguliwa kwa Mtaguso Mkuu wa II wa Vatican, uliofanyika mnamo mwaka 1962. Ili kujua mtindo huo wa pamoja wa kumbukumbu ya maisha na wakati ujao ndicho kilitokea Ijumaa tarehe 11 Oktoba Asubuhi, kama ilivyosimuliwa na Dk. Paolo Ruffini Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi na Bi Sheila Peres, Katibu wa Tume hiyo ambao walitoa mhutasari wa Sionodi inayoendelea mjini Vatican mbele ya Waandishi katika Chumba cha Waandishi wa Habari mjini Vatican. Pamoja nao walikuwapo Kardinali Joseph William Tobin, Askofu Mkuu wa Newark, nchini Marekani, Askofu Shane Anthony Mackinlay, askofu wa Sandhurst, Australia, na Profesa Giuseppina De Simone, profesa wa Falsafa ya Dini na mratibu wa taaluma ya Taalimungu Msingi katika Kitivo cha Kitaalimungu cha Kipapa cha Kusini mwa Italia.
Kutunza mahusiano
Akiripoti Bi Pires, alisema "Tangu alasiri, tarehe 10 Oktoba 2024, tumekuwa tukifanyia kazi sehemu ya tatu ambayo, kama zile zilizopita, ilianzishwa na Mjumbe Mkuu wa Kardinali Jean-Claude Hollerich. Walikuwepo washiriki 346 katika Ukumbi wa Paulo VI. Mada kuu ya sehemu hiyo ilikuwa ni utunzaji wa uhusiano, hasa, kwamba "mahusiano katika Kanisa lazima yawe na msingi wa uaminifu, uwazi na mshikamano. Tunahitaji mafunzo muhimu ili kuandaa mashuhuda wa utume wa kikanisa, kama Kardinali Hollerich alivyosisitiza, akikumbuka, hata hivyo, kwamba utambuzi wa kikanisa ni tofauti na mbinu za usimamizi." Kwa ufupi, kulikuwa na mwaliko kuendeleza michakato shirikishi na ya uwazi ya kufanya maamuzi ndani ya Kanisa, kwa kuzingatia kwamba tathmini ya mara kwa mara ya matendo ya wale walio na majukumu ni ya msingi.”
Mkutano kati ya Yesu na mwanamke Mkanaani
Ripoti ya Kardinali Hollerich tarehe 10 mchana ilitanguliwa na tafakari ya Kardinali mteule, Padre Timothy Radcliffe, Padre Mdominikani, ilichunguza michakato ya mabadiliko ya Kanisa kupitia ukurasa wa kiinjili wa Yesu kukutana na mwanamke Mkanaani. Ukimya wa Yesu unaonekana kama wakati wa kusikiliza kwa kina. Na kwa hakika"ukimya huu unawakilisha fursa kwa Kanisa kukabiliana na maswali magumu na kukaribisha vilio vya wale wanaotafuta msaada," aliripoti Bi Pires.
"Na iwe kama unavyotakavyo"
Zaidi ya hayo, "Padre Radcliffe alitualika kutafakari juu ya masuala ya kimsingi, kama vile uhusiano kati ya usawa na tofauti na jukumu la Kanisa kama jumuiya ya waliobatizwa na madaraja, miito na majukumu tofauti. Masuala haya yanahitaji kuishi kwa uangalifu na maombi endelevu, badala ya majibu rahisi na ya haraka. Na kwa hivyo "jibu la Yesu: "Na lifanyike kwako kama unavyotaka," kwamba ni ishara ya uwazi na ushirikishwaji, na linaonesha ubunifu wa kimungu katika kushinda vikwazo na kukaribisha utambulisho, na kwa mtazamo wa wale walio tofauti," ndiyo yalikuwa ni maneno ya mhubiri huyo," Katibu wa Tume ya Habari alidokeza.
Mkesha wa kiekumene
Dk, Ruffini aidha alisema “Ijuma tarehe 11 Oktoba 2024, baada ya sala mjadala katika meza za miduara uliendelea na kumalizika, ukiwa tayari umeanza tangu tarehe 10 Oktoba baada ya ripoti ya utangulizi ya Msemaji mkuu wa Sinodo Kardinali Koch. Kulikuwa na washiriki 341 katika Chumba hicho alasiri Oktoba 11 na ripoti za vikundi kwa kuzingatia lugha zitawasilishwa. Baada ya kupiga kura kwenye Ajenda ya majadiliano, hotuba za bure zilifuata. Hata hivyo tarehe 11 Oktoba jioni saa 7.00, washiriki wa Sinodi walishiriki mkesha wa kiekumene uliofanyika mjini Vatican - "mbele ya Baba Mtakatifu"katika uwanja wa Mashahidi wa Roma. Wajumbe ndugu waliohudhuria katika Sinodi na pia wawakilishi wa Makanisambalimbali wanaoishi mjini Roma walishiriki mkesha huo, mahali ambapo umoja wa Kikristo tayari unashuhudiwa. Zaidi ya hayo kwa kushirikiana na sherehe mjini Vatican sala kutoka mahalia zilipangwa katika maeneo 80 tofauti katika mabara yote," Alisisitiza Dk Ruffini.
Usikilizaji wa kina
Kusikiliza, kimya, maombi. Hivi ni vigezo vitatu vilivyo dhahiri zaidi vya mbinu ambavyo kazi ya Sinodi imeegemezwa. Kardinali Tobin alieleza hayo. "Wakati huu, ikilinganishwa na siku za nyuma - aliendelea kardinali, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la kawaida na Tume ya Habari - usikilizaji ulifanyika kwa njia ya kina sio tu ndani na kwa mashirika ya Kanisa, lakini ni kweli wa kujitahidi kufikia kila mtu.” Hii pia ilipendelea "ushiriki mpana zaidi, na hii ilitoa fursa ya kufuatilia maendeleo ya kazi na uchambuzi wa kina wa mada kwa njia tofauti".
Taalimungu ililetwa katika ukweli
Profesa De Simone kisha alisema: "Kwa maoni yangu, njia ambayo ni sifa ya vikao hivi viwili ni ya kimapinduzi kweli, na yenyewe ni ishara ya matumaini. Ni njia ambayo ina mengi ya kusema kwa ulimwengu." Profesa pia alikumbuka kipengele cha kusikiliza "ambacho tafakari nzito, kali hutokea, na ya ukimya: "Hii yenyewe ni uwezo wa kukaa katika swali. Hatutafuti jibu la uhakika mara moja, lakini tunasalia ndani ya swali linalojitokeza kutokana na majeraha ambayo ubinadamu huwasilisha na kutupatia." Zaidi ya hayo, De Simone alisema, inashangaza pia kwamba "watu wote wa Mungu wamekusanyika kwenye meza za kufanya kazi, shukrani ambayo tunaishi hisia ya kuwa pamoja." Kwa njia hiyo, taalimungu pia "inachukua uwepo na uzito mkubwa, kwa sababu inaangukia moja kwa moja katika ukweli, katika kitambaa hai cha mahusiano".
Njia mpya ya kufanya mambo
Askofu Mackinlay alizungumza kuhusu uzoefu wa sinodi waliyoishi katika jimbo lake na katika bara lake analotoka. "Baraza la Maaskofu Australia lilianza safari miaka michache kabla ya Sinodi ya sasa, likileta pamoja watu wapatao 250, wakiwemo maaskofu, watawa kike na kiume na waamini walei. Na hata katika hafla hiyo tulipata masuala mengi ya kushughulikia, yakigusa maswala ya watu moja kwa moja. Ilikuwa ni jambo la msingi, basi, katika kazi yetu kuingilia utamaduni wa Kanisa kwa njia ya kushughulikia masuala; na hivi ndivyo pia tunajaribu kufanya hapa kwenye Sinodi: ili kujaribu kubadilisha jumuiya ya kikanisa kuelekea njia mpya ya kufanya mambo. Ni njia ya kujitolea kwa uwajibikaji pamoja na utambuzi ambao unatuongoza kufikia pamoja katika maamuzi ambayo yanafaa iwezekanavyo," alielezea Mackinlay, na ambaye pia mjumbe aliyechaguliwa wa Kamati kwa ajili ya kuandaa hati ya mwisho.
Mkutano na Papa Francisko
Kama kawaida, kulikuwa na nafasi ya maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwapo kwenye Chumba cha Wanahabari. Kardinali Tobin aliripoti mkutano ambao ulifanyika siku ya Alhamisi 10 Oktoba 2024 asubuhi na Papa Francisko pamoja na makardinali wengine wawili wa Kiamerika. “Tulitakiwa kukutana saa 1.30 na hatukuwa hata watu wa kwanza kumuona. Nadhani aliamka saa 10 alfajiri", alibainisha Kardinali huyo huku akiripoti kwamba alikuwa ameomba kuwa na mahojiano kwa sababu "Kanisa daima linatafuta njia za kufanya vizuri zaidi kile tunachoitwa kufanya. Kama vile unavyokuwa na wenzako ambao uko karibu nao," Kardinali Tobin alisema, akimaanisha moja kwa moja kwa waandishi wa habari, "vivyo hivyo na sisi pia tunaulizwa juu ya mada ya unyanyasaji." Akikumbuka, baadhi ya vipindi vilivyotokea katika jimbo lake ndivyo vilivyosababisha kutokuwepo kwake katika Sinodi ya 2018 iliyoandaliwa kwa ajili ya vijana. "Nadhani Papa anataka kufanya jambo bora zaidi kwa Kanisa na kwa watu ambao wameathiriwa. Suluhisho zinazopendekezwa ni kwa manufaa ya wote”, alisema, akirejea pia matukio yanayohusiana na jumuiya ya maisha ya kitume ya Peru Sodalitium Christianae Vitae, ambayo alikabidhiwa mwaka 2016.
Sinodi ndogo ambayo siyo ya kiulaya
Kisha maswali yaligusia mada zinazohusiana na Sinodi inayoendelea. Askofu Mackinlay, ambaye atawakilisha Oceania katika Kamati iliyotajwa hapo juu ya kuandaa hati ya mwisho, alibainisha maono ya chini ya kiulaya na ushirikiano wa "vipimo vya kiutamaduni, hasa Amerika ya Kusini na Afrika", ndani ya mazungumzo katika Baraza la Maaskofu. "Tunasikia kwamba kuna uwajibikaji wa pamoja katika maisha na maamuzi ya jamii," aliongeza. Askofu wa Australia alikumbuka mkutadha wake maalumu kwamba: matayarisho ya mikutano yenye uwezo wa kuhusisha pia watu wa kiasili, kupitia michakato mirefu "hata miaka miwili au mitatu" ambayo, hata hivyo, "inaturuhusu kuendelea katika haki na upatanisho" kati ya jamii tofauti.
Kukumbatia hisia tofauti
Swali lilihusu mtazamo wa Sinodi kwa masuala ya LGBTQIA+, Kardinali Tobin alibainisha jinsi ambavyo masuala hayo yanavyoshughulikiwa, ingawa sio dhahiri kama wengine wangependa kusikia, japokuwa akikumbuka kifungu cha tafakari iliyoandikwa na Padre Timothy Radcliffe, na ambaye kwake alisema ikiwa mtu hajaridhika na jibu analopokea lazima asiondoke kwenye meza kabla ya kupata jibu. Kuna uwezekano wa mazungumzo kwa kila wakati. Profesa De Simone alisisitiza kanuni ya msingi ambayo kulingana nayo "suluhisho kubwa, juu ya funzo haziwezi kutarajiwa, akitumaini kujua jinsi ya kukaribisha hisia tofauti za kiutamaduni."
Kwa wanawake, mambo yanabadilika
Dhana iliyoidhinishwa na Askofu Mackinlay, ambaye aliakisi jinsi gani mada haianzii tena kutoka mwanzo, kutokana na mijadala iliyopita, na jinsi masuala mengine nyeti pia yanashughulikiwa wakati wa Mkutano wa Maaskofu. Askofu wa Australia alijibu "Sikufikiri - kwamba mitala ingepata nafasi kubwa sana". Akiwa na uhakika wa ufanisi wa sinodi kama chombo cha kushughulikia mazingira ya sasa, Kardinali Tobin alibainisha mambo mawili ya msingi ili kufanya kazi kwa ajili ya amani:"Kuwafanya watu wote kuketi mezani na kujumuisha wanawake". Profesa De Simone alipanua zaidi lengo: "Pamoja na wanawake majadiliano yanabadilika. Ningesema kwamba kunapokuwa na mwelekeo wa kimahusiano moja kwa moja, mijadala hubadilika. Unapotazamana na mtu machoni na maneno hata kama ya kufikirika, unasema historia ya maisha. Kisha ni historia tofauti kabisa."