Tafuta

Mhutasari wa Sinodi-Siku ya 8:Kutembea njia ya Umoja wa Kikristo

Mkutano wa Sinodi Alhamisi Oktoba 10 uliakisi Umoja wa Wakristo.Kardinali Koch,Wamer,Askofu wa Kianglikani na Graber,Mchungaji wa Mennonite walikuwa ni wageni katika mkutano wa kila siku wa waandishi wa habari.Kardinali Koch:“Harakati ya kiekumene inatambulika kwa kutembea,kusali na kushirikiana pamoja."

Na Roberto Paglialonga, Lorena Leonardi na Angella Rwezaula – Vatican.

Kufuatia maelekezo kutoka Sekretarieti Kuu ya Sinodi, mwandishi maalum Padre Giacomo Costa aliwahimiza washiriki wa Sinodi kuwa wabunifu, wasiogope na “desborde”neno la Kihispania la "kufurika", alisema Cristiane Murray katika Muhtasari wa Sinodi kwa Wanahabari Alhamisi tarehe 10 Oktoba 2024. Katibu Msemaji mkuu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican alisimamia mkutano huo mfupi uliowasilishwa na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari ya Sinodi, na Sheila Peres, Katibu wa Tume hiyo.

Ripoti za kuhitimisha kutoka katika Miduara

Kazi ya Sinodi ya asubuhi tarehe 10 Oktoba 2024, iliyohudhuriwa na washiriki 342, ilifanyika ndani ya Miduara midogo pekee, bila uingiliaji wa wazi, na ripoti za kuhitimisha juu ya sehemu ya pili ya kazi ziliwasilishwa. Zaidi ya hayo, Dk Ruffini alisema, baadhi ya miongozo ya kimbinu ilitolewa, kutia moyo kwa ubunifu na ‘kufurika.’” Neno hilo, ambalo Dk Ruffini alikumbuka, linatumiwa katika lugha ya  Kihispania kama “desborde,” neno ambalo pia lilitumiwa na Papa katika  Waraka wa Kutume wa Querida Amazonia na wakati wa Sinodi ya Amazonia 2019.  Kwa mujibu wa maelezo ya Dk. Ruffini aliongezea, tumaini ni kwamba kutakuwa na kuongezeka kwa 'kufurika,' kwa msingi wa kutokuwa na utulivu na hamu ya kusonga mbele. Alasiri tarehe 10 Oktoba 2024  kazi ya kushirikisha na utambuzi kwenye sehemu ya tatu ya Instrumentum Laboris, sehemu yenye kichwa "Njia, Bi  Peres alielezea katika hotuba yake. Hayo yalitatanguliwa na kipindi cha sala na tafakari kilichoongozwa na Padre Mdominikani na Kardinali mteule Timothy Radcliffe na utangulizi wa sehemu hizo na Kardinali Jean-Claude Hollerich, Msemaji Mkuu wa Sinodi ya maaskofu.

Kubadilishana kwa zawadi

Sauti ilitolewa kwa wageni katika mkutano huo, ambao walizingatia uekumene, ambayo huunda muungano ambao siyo wa kutenganisha na sinodi. Kardinali Kurt Koch, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, alitoa muhtasari wa dhana hiyo kwa maneno haya: “Safari ya sinodi ni ya kiekumene. Na safari ya kiekumene haiwezi kuwa chochote ila sinodi.” Akifafanua mwelekeo wa kiekumene kama “mojawapo ya vipengele muhimu zaidi vya Sinodi hii,” Kardinali alisisitiza jinsi ”uekumene na sinodi ni msingi wa “ubadilishanaji wa karama, ambamo tunajifunza kutoka kwa wenzetu, tukiwa na imani kwamba hakuna Kanisa lililo tajiri kiasi kwamba, halihitaji mchango wa Makanisa mengine, na kwamba hakuna Kanisa lililo maskini kiasi kwamba halina cha kutoa. Utakatifu ndio njia ya uhakika ya umoja. Kardinali alichukua fursa hiyo kuakisi jinsi uwepo wa wajumbe ndugu ulivyo muhimu zaidi katika kikao hicho kuliko kile cha awali, na aliwahakikishia ushiriki wao katika mkesha wa kiekumene ulioandaliwa tarehe 11  Oktoba 2024 kwa ushirikiano na Jumuiya ya Kiekumene ya Taizé. Maombi ya kuhamasisha mkutano huo, huo  yalitolewa kutoka katika  maandishi mawili yanayolingana: katiba ya kidogma Lumen gentium na Dikrii juu ya Ecumenism Unitatis redintegratio. Mahali palipochaguliwa kwa ajili ya tukio hilo, kufanyika katika Uwanja wa Mashahidi wa Roma mahali ambapo maokeo yabainisha kuwa aliuawa Mtakatifu Petro Mtume. Hii inatukumbusha,kwamba utakatifu ndiyo njia ya hakika ya kuelekea kwenye umoja,” alihitimisha Kardinali Koch

Mazungumzo hujenga misingi, sio maelewano

Askofu Ayubu, Mkuu wa Kanisa la Pisidia na rais mwenza wa Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Majadiliano ya Kitaalimungu kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox, alikuwa wa kwanza kati ya wajumbe watatu wa kidugu kuzungumza. Yeye alisema kwamba kuhusu masuala kama vile ukuu, sinodi, huduma, na maridhiano, mazungumzo kati ya Waorthodox na Wakatoliki “yamekuwa yakiendelea kwa miaka 20 na maendeleo, si tu kutuleta karibu na kutupatanisha bali pia kuzaa matunda katika maisha ya ndani ya kila Kanisa.” Mkuu huyo wa jiji pia alitaja waraka wa hivi karibuni wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo wa Askofu wa Roma, akibainisha kwamba kilichomvutia katika uchapishaji huo ni “kukutana kwa mazungumzo haya yote. Inaonesha kwamba si tu kutafuta ‘mapatano’ fulani kati ya Makanisa bali kuhusu kuweka misingi ya maisha ya umoja wa Kikristo.”

Nafasi salama ya kufungua mioyo kwa kila mmoja

Askofu wa Kianglikani Martin Warner wa Chichester, rais mwenza wa “Kamati ya Kianglikani ya Kiingereza - Welsh,” alizingatia thamani ya uzoefu wa uhusiano, ambao unatofautisha Sinodi hii na yale ya Kanisa la Kianglikani. Tangu wakati huo aliyekuwa Mkuu wa Kianglikani, Michael Ramsey kupokea pete ya uaskofu kutoka kwa Paulo VI, Warner alisisitiza, kuwa “Tunaweza kutazamana, kutambua tofauti zetu lakini pia umuhimu wa kubadilishana zawadi ili kukua katika uzoefu wetu husika.” Tofauti na vikao vya sinodi za Kianglikani, vile vya Kikatoliki vina sifa ya sala na ukimya na, muhimu sana, “si vya kutunga sheria,” alieleza, na hili, askofu Warner aliongeza, linahakikisha “nafasi iliyolindwa ambamo mioyo inaweza kufunguliwa kwa mtu na mwenzake; katika mazungumzo na Roho, kuangalia kwa ubunifu na kwa ujasiri changamoto za karne hii.”

Kila sauti ni muhimu

Hatimaye, Mchungaji Anne-Cathy Graber, mchungaji kutoka Umoja wa Ulimwengu wa Kanisa la Mennonite na katibu wa mahusiano ya kiekumene, ambaye anashiriki katika Sinodi kwa mara ya kwanza, alisema “alishangazwa na mwaliko huo,”kwa vile yeye ni mfuasi wa “Kanisa lisilojulikana sana” ambalo liliibuka kutoka katika (mabadiliko ) ya Kanisa katika karne ya 16 na lina sifa ya ubatizo wa waamini na kutotenda jeuri. Akitafakari kuhusu kuwapo kwake, alisema: “Kanisa Katoliki halihitaji sauti yetu, ambayo ni ndogo sana, lakini hilo lenyewe linasema mengi kuhusu sinodi, linaonesha kwamba kila sauti ni muhimu.” Kwa Mchungaji Graber, “Umoja wa Kikristo sio tu ahadi ya kesho, iko hapa na sasa, na tunaweza kuiona tayari. Hatuko karibu tu bali ni wa mwili uleule wa Kristo, sisi ni viungo vya kila mmoja, kama vile Mtakatifu Paulo alivyosema.” Ingawa hatuna haki ya kupiga kura kama wajumbe ndugu, "sauti yetu na uwepo wetu ulikaribishwa kama kila mtu mwingine. Hadhi sawa ya ubatizo inaonekana. Hakuna Kanisa lenye nguvu linalotawala kutoka juu. Sisi sote ni watu wanaotembea pamoja na kutafuta,” aliendelea.

Uekumene hauko katika mgogoro

Kipindi cha Maswali na Majibu kiligusa hasa mada za mahusiano ndani ya mazungumzo ya kiekumene na kati ya ukuu wa Askofu wa Roma na sinodi. Kardinali Koch alieleza kwamba “tunachofanya kinaonesha kwamba uekumene hauko katika mgogoro, bali unakabiliwa na changamoto mbalimbali.” Alikubali, akijibu maswali ya waandishi wa habari, kwamba "hali ya kusikitisha ipo, iliyosababishwa kwa sehemu na maneno ya Patriaki Kirill wa Moscow, Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la Urusi, ambalo lilisababisha mpasuko kati ya Constantinople, lakini ni lazima tutofautishe misimamo hii na safari inayoendelea.” Kwa hakika, alikazia, “Kuna tume iliyochanganyika inayohusisha Makanisa 15 ya Kiorthodox ambayo inaendelea kufanya kazi, kumaanisha kwamba mazungumzo yanaendelea kwa matumaini ya kuunda wakati ujao ulio bora zaidi, kutia ndani tumaini la kuandaa mkutano mkuu pamoja.”

Umuhimu wa ishara ndogo

Uhakikisho huu pia ulisisitizwa na Mkuu wa Kanisa la Pisidia kwamba: "Kanisa la Kristo linabaki hai, licha ya misimamo ya kisiasa iliyotolewa na Kirill, kwa sababu mazungumzo ya kitaalimungu yanaendelea kuweka misingi thabiti," alisema. “Hii ni harakati; hakuna kupumzika katika safari yetu,”Kardinali Koch aliongeza. “Harakati ya kiekumene inatambulika kwa kutembea pamoja, kusali pamoja, kushirikiana pamoja. Yesu Mwenyewe hakuamrisha umoja wa Kikristo bali anauombea: ni jambo gani bora zaidi tunaweza kufanya kuliko kusali ili upatikane kama zawadi ya Roho Mtakatifu?” Labda "kinachotarajiwa," Mchungaji Graber aliingilia kati, ni "ishara ndogo za ishara za upatanisho ambazo bado hazipo." Kuhusu uhusiano kati ya ukuu wa Petro na sinodi, Kadinali Koch alifafanua kwamba “tunaweza kuthibitisha kwamba sinodi na ukuu hazipingani. Kinyume chake: moja haipo bila nyingine na kinyume chake aliongeza kuwa "ukuu sio upinzani, lakini fursa ya kujadili na kupata msingi wa pamoja."

Swali la ukarimu wa sakramenti

Akizungumzia suala la ukarimu wa sakramenti, ilikumbukwa kwamba Papa ameanzisha kikundi cha kazi kinacho jitolea na kwamba "bado hakuna maono ya kawaida ya Kanisa na sakramenti katika mazungumzo kati ya Makanisa ya Magharibi." Job alionesha matumaini kwamba “tunaweza kukubaliana siku moja juu ya tarehe moja ya Pasaka kati ya Wakristo na Waorthodox lakini kwa sasa, hilo linasalia kuwa matashi tu.” Akijibu maswali juu ya zile zinazoitwa huduma za wanawake, Msimamizi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo alisisitiza: "unyeti wa mada hiyo, ambayo Papa ameanzisha vikundi 10 vya kazi." Alisema kwamba “pia Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa imekuwa ikifanya kazi juu yake kwa muda fulani kwamba "tume mbili za uchunguzi hazijafikia uamuzi mmoja, kuonesha kwamba uchunguzi zaidi unahitajika. Kwa hivyo ni muhimu kuchanganya shauku ya masuala haya na uvumilivu wa mafunzo,” Kardinali alihitimisha.

12 October 2024, 09:46