Tafuta

SPECIALE/Papa Francesco, i momenti salienti di 10 anni di pontificato Tahariri

Miaka 11 iliyopita ya mkasa wa Lampedusa

Tarehe 3 Oktoba 2013,wahamiaji 368 walikufa mbele ya kisiwa cha Sicilia karibu na Afrika kuliko Italia.Leo hii,kama ilivyokuwa wakati huo,Papa Francisko anatoa wito kwa ulimwengu kuwa na ukarimu zaidi,msaada na udugu.

Massimiliano Menichetti

Ulaya, dunia nzima iliyokumbwa na vita, umaskini na vurugu, inaendelea kukabiliana na kugawanyika kuhusu mada ya uhamiaji, karibu kusahau kwamba neno hilo halitoi mawazo, lakini linazungumzia nyuso, historia, watu, mara nyingi za maumivu na majanga. Mipaka iliyowekwa na kuta mara nyingi ni mipaka isiyopitika kwa wale wanaokimbia hofu ya migogoro au kutafuta maisha bora. Wanaume, wanawake na watoto waliokufa katika jangwa wakijaribu kuvuka, mateka katika vituo vya kizuizini, kumezwa na mawimbi ya bahari, kama miaka kumi na moja iliyopita.

Mnamo tarehe 3 Oktoba 2013, tumaini la roho za watu 543 likawa la kutisha. Boti ya wavuvi waliyokuwa wakisafiria ilipinduka na kuzama takriban nusu maili kutoka kisiwa cha Lampedusa cha Italia. Waethiopia na Waeritrea walikuwa wameondoka siku mbili kabla kutoka Misurata nchini Libya, wakipanda mtumbwi huo takriban mita ishirini. Ilikuwa ni moja ya majanga makubwa zaidi ya baharini kutokea tangu mwanzo wa karne ya 21 katika Bahari ya Mediterania: ni vifo 368 vilivyothibitishwa na walionusurika 155, wakati  huo watu 20 waliodhaniwa kuwa hawajulikani walipo.

Huku Lampedusa, msalaba mdogo wa mti uliotengenezwa kutoka kwenye mitumbwi ya wahamiaji
Huku Lampedusa, msalaba mdogo wa mti uliotengenezwa kutoka kwenye mitumbwi ya wahamiaji

Papa Francisko, mwezi Julai mwaka huo huo, akifanya ziara yake ya kwanza ya upapa mjini Lampedusa, alilia kwa uchungu wake kwa janga lingine la bahari lililotokea katika pwani hizo kipindi  kifupi kilichokuwa kimepita. Alizungumza juu ya “utandawazi wa kutojali” ambao unatufanya sote “kuwajibika.” Alithibitisha kuwa “hatupo tena makini na ulimwengu tunamoishi, hatujali, hatulindi kile ambacho Mungu aliumba kwa kila mtu na hatuna uwezo tena wa kulindana sisi kwa sisi.” Nyaraka tatu, mamia ya miito, ziara na safari ambazo Papa Fransisko katika miaka ya hivi karibuni ameshughulikia moyo wa mwanadamu ili kuamsha dhamiri, ili kuangusha ubinafsi, kutojali, unyonyaji na kujenga ulimwengu wa amani, wenye ukarimu, udugu, na msaada. Bahari ya Mediterania na kitovu cha ustaarabu, badala ya kuungana, imezidi kuwa mbali na kaburi la kimya. Katika bahari hali sio tofauti. Katika jamii ya mitandao ya kijamii, ambayo akili mnemba huahidi janga na ajabu wakati huo huo, inaonekana kuwa ni rahisi kuangalia kwa njia nyingine, kupuuza, na kuondoa.

Hatuwezi kusahau, kwa mfano, taswira iliyosonga na kuwashtua mamilioni ya watu mnamo 2015 ambayo: ni ile ya Aylan, mkimbizi mdogo wa Siria asiye na uhai, aliyekuwa amelala kifudifudi, uso wake mchangani, ukiwa umebanwa na maji, kwenye ufukwe wa Bodrum, nchini Uturuki. Papa Fransisko anaendelea kuhimiza juhudi za kisiasa na kidiplomasia zinazolenga kuponya kile alichokiita “jeraha la wazi la ubinadamu wetu” kwani haachi kuunga mkono dhamira ya wale wote wanaowasaidia, kuwakaribisha na kuwasaidia wahamiaji. “Suluhisho si kukataa - alisema huko Marsiglia mnamo mwaka 2023 katika kikao cha mwisho cha “Rencontres méditerranéennes”- lakini kuhakikisha, kulingana na uwezekano wa kila mtu, idadi kubwa ya maingizo ya kisheria na ya kawaida.” Kwa upande wa Papa, jambo kuu ni kukutana, kuchukua hatari, kupenda, kutembea na kutafuta suluhisho pamoja. Haya yote yanahitaji kila mmoja wetu kubadili mtazamo wake, kuhama kutoka ile tabia ya umimi kwenda ile ya sisi, kurejesha kumbukumbu zetu na kutazama ili kuweza kutambua uso wa huruma wa Yesu kwa wengine.

MENICHETTI KUMBUKIZI LAMPEDUSA
03 October 2024, 14:32