Tafuta

Muhtasari wa Sinodi-Siku ya 12:Umuhimu wa kutambua makubaliano!

Katika mkutano na waandishi wa habari wa Sinodi tarehe 16 Oktoba 2024,mratibu wa wataalam wa Taalimungu,Padre Dario Vitali,alisisitiza kazi ya vikundi,kazi vya wataalimungu na waamini watakatifu kuwa siku zote ni kumsikiliza Roho,wakati kusanyiko lilishughulikia mada kama vile umoja wa Kanisa na uwezo wa Mabaraza ya Maaskofu.

Alessandro Di Bussolo,Roberto Paglialonga na Angella Rwezala – Vatican.

Umoja wa Kanisa na uwezo wa Mabaraza ya Maaskofu, kwa mtindo unaozidi kuongezeka wa Sinodi, ni miongoni mwa mada zilizohutubiwa tarehe 15 na 16 Oktoba 2024, wakati wa mikutano katika Ukumbi wa Paul VI katika kikao cha pili cha Sinodi ya Kiinodi. Wazungumzaji wanne kwenye mkutano huo katika Ofisi ya Waandishi wa Habari wa Vatican, siku ya Jumatano 16 Oktoba waliakisi wajibu wa wataalamu wa taalimungu na waamini watawa katika kipindi hiki cha pili, pamoja na umuhimu wa kutambua maafikiano yanayosogeza Kanisa mbele wakati wa kumsikiliza Roho.

Mapendekezo ya awali kutoka katika ripoti za mizunguko ya lugha

Mkuu wa Baraza la Mawasiliano na Rais wa Tume ya Habari Dk. Paolo Ruffini pamoja na Katibu wa Tume hiyo Dk. Sheila Pires walitoa taarifa za mkutano huo. Kwa siku mbili zilizopita, "tumekuwa tukijadili sehemu ya mwisho ya Instrumentum laboris," alisema Dk. Ruffini, "na vikundi vidogo vimekuwa vikifanya kazi kuwasilisha, pamoja na wazungumzaji kutoka kwenye mizunguko ya lugha, pendekezo la awali la masuala mahalia.”

Ulimwengu wa kidijitali na parokia

Katika Ukumbi wa Paulo VI, Msimamizi alisisitiza, "Kanisa daima limerejea jiji, mahali lilipoishi, likiongozwa na askofu katika uhusiano wa karibu na eneo hilo." Pia alisema, “Lazima Kanisa liishi katika ulimwengu wa kidijitali,” likizingatia “hatari zilizopo.” Kutoka katika vikundi, "tahadhari kwa parokia kama maeneo ya mikutano yalijitokeza," Dk. Ruffini aliendelea, "Lakini pia kuna haja ya kuwa wabunifu na kufikiria, kupanua maeneo ya Kanisa letu katika nyanja zingine," hasa ile ya kidijitali. Zaidi ya hayo, washiriki wa Sinodi walikuwa wameakisi “haja ya kutambua na kuimarisha miundo ya sinodi iliyopo, katika kubadilishana zawadi kati ya Makanisa  mahalia na ya bara.” Kuhusu Mabaraza ya Maaskofu, Dk. Ruffini alibainisha, kwamba wajumbe walisema “yanakuza ushirika, lakini bado ni muhimu kufafanua hali yao vizuri zaidi.”

Jukumu la sinodi ya Mabaraza ya Maaskofu

Dk.Ruffini pia aliripoti kwamba “suala la kukabidhi uwezo wa kimafundisho kwenye Mabaraza ya Maaskofu lilishughulikiwa, pamoja na umuhimu wa kugundua uzuri wa tamaduni mbalimbali, ambazo, hata hivyo, hazitoshi zenyewe.” Aliongeza kuwa "Mabaraza ya Maaskofu wa bara yalionekana kuwa mahali pazuri pa kusuka sinodi katika ngazi ya bara" na "jinsi ya kuboresha Mabaraza ya Maaskofu kama viwango vya ushirikiano wa kati." Mkuu wa Baraza la Mawasiliano aidha alibainisha kwamba wale waliozungumza walikubaliana kwa pamoja katika kutambua “umuhimu wa kuhifadhi umoja wa Kanisa.”

Huduma ya Mtume Petro katika huduma ya umoja

“Huduma ya Papa katika wakati wa utandawazi ilizungumziwa,” Dk. Ruffini aliendelea, “na utumishi wake kwa umoja si wa Kanisa Katoliki pekee, bali pia kuhusu Wakristo wengine, kuwa mamlaka kuu zaidi ya kiadili na kiroho.” Katika kutambua mada za majadiliano na vipaumbele vyake, vikundi vilianza kwa kuangalia “Mabaraza ya Maaskofu katika sinodi na ufunguo wa kimisionari: asili ya kitaalimungu, uwezo, na mamlaka katika maeneo ya mafundisho, kiliturujia, kichungaji, kinidhamu na kiutawala.” Kimsingi, swali ni "jinsi gani  ya kupanga upya ushiriki katika ufunguo wa kimisionari katika muktadha wa mabadiliko yakipindi, kwa kuzingatia matukio ya uhamaji wa binadamu, utamaduni, na mazingira ya kidijitali." Zaidi ya hayo, “jinsi ya kuweka umoja, muungano na ukuu; nafasi ya Curia Romana katika nuru ya katiba ya kitume Praedicate Evangelium; sinodi ya ulimwengu mzima, Mikutano ya  kanisa la bara, sinodi, na mabaraza mahalia.” Mada zitakazofuata zitajumuisha: “vigezo vya kufafanua ufafanuzi wenye afya, Kanisa la Makanisa, ubadilishanaji wa zawadi, matamshi ya mahali pamoja na watu wote, tanzu, na Makanisa juu sheria (sui iuris.)”

Uinjilishaji wa ulimwengu wa kitamaduni

Katika maelezo yake, Dk. Pires aliakisi umakini wa uinjilishaji wa utamaduni, akikiri kwamba kila mtu ni sehemu ya ardhi ya wamisionari na kubainisha nafasi ya jumuiya ndogo ndogo ambazo zinaweza kufanya parokia kuwa hai zaidi. Dk. Pires alisema, “Sinodi imeakisi hitaji la kuzoea mabadiliko ya kiutamaduni na kidijitali, kukuza Kanisa la Sinodi na kimisionari zaidi: mjadala ulisisitiza umoja wa imani na uwezo wa Kanisa kujibu changamoto za kisasa.”

Wazungumzaji wanne wakiwa kwenye mkutano huo

Jopo hilo lilijumuisha Padre na mtaalimungu wa Italia, Padre Dario Vitali, mratibu wa wataalimungu waliobobea wa Sinodi na profesa wa kikanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian; Padre wa Kihispania, Padre José San José Prisco, profesa wa Sheria za Kanisa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salamanca, mjumbe wa Umoja wa  Wafanyakazi wa Kipadre wa Jimbo, mtaalamu wa malezi na wito; Klára Antonia Csiszàr, Mromania kwa kuzaliwa na Mkuu wa Kitivo cha Taalimungu na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Linz nchini Austria; na kuhani wa Australia, Padre Ormond Rush, mshauri wa kitaalimungu wa Sekretarieti ya Sinodi na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Australia huko Brisbane.

Padre Vitali:Kazi ya pamoja ya vikundi vinne vya wataalimungu

Katika maelezo yake, Padre Vitali alisisitiza kwamba kazi ya vikundi vinne vya lugha za wataalimungu anazoratibu (Kiingereza, Kifaransa, Kihispania-Kireno, Kiitaliano) ni "kusoma tena mapendekezo ya Mkutano huo kwa kubainisha vipengele vinavyojitokeza vya makubaliano," na kuunda ripoti za pamoja ambazo zinaonesha "kwa wale ambao lazima waandae maandishi ya mwisho mambo ya muunganisho na yale ambayo ni ya shida." Kilicho muhimu katika safari ya Kanisa, katika kumsikiliza Roho, ni maafikiano. Sio lazima kutafuta na kuonesha vipengele visivyoendana. Ni jukumu la wataalimungu, Padre Vitali alifafanua, “Kutambua aina ya maafikiano yanayokomaa katika kusanyiko, ili andiko lilingane na yale ambayo yameshirikishwa kati ya washiriki na yale ambayo Roho anaonesha kwa Kanisa.” Kazi ya vikundi vya lugha nne ni mfano wa mtindo wa sinodi, alibainisha, matokeo ya kazi ya ushirikiano kati ya wataalimumgu iliyoanza mwaka wa 2021, pamoja na safari ya sinodi. Katika sinodi zilizopita, wataalimungu walitangamana tofauti na Sekretarieti ya Sinodi.

Padre  Prisco:Wanasheria na mapendekezo ya Sinodi

Kama mjumbe wa tume ya kisheria ya Sinodi, Padre Prisco alisisitiza kwamba kazi ya wataalam wa kanuni katika mkutano huu ni juhudi shirikishi na wataalimungu, "ilhali hapo zamani, taalimungu na sheria za kanuni mara nyingi zilitembea katika mistari sambamba inayofanana." Badala yake, kukamilishana na ushirikiano ni muhimu. Kazi ya Sinodi, Padre  Prisco aliendelea, anahofia “hasa kitabu cha pili cha Kanuni za Sheria ya Kanisa, kilichowekwa wakfu kwa Watu wa Mungu.” Tume ya waamini, iliundwa kutokana na hitaji lililooneshwa na washiriki: kikundi cha wataalam wa sheria za kanuni kuandamana na kutathmini mapendekezo ya Sinodi, "kutambua uwezekano wa marekebisho au kanuni mpya ambazo zinaweza kuboresha sheria ya kanuni, zote mbili. Kilatini na Mashariki."

Csiszàr:Katika majukwaa,"wimbo wa sinodi"

Mtaalimgu wa kichungaji Klára Antonia Csiszàr alisisitiza umuhimu wa mchango wa kitaaòimungu wa Mabaraza, ambayo "pia inahusisha kujua mengine na kuruhusu kurekebisha utamaduni wa sinodi katika Kanisa." Mwaka jana(2023) kwenye kuhitimisha kazi ya sinodi, mshiriki mmoja alisema kwamba “taalimungu haikuzingatiwa sana.” Hata hivyo, katika Jukwaa la kitaalimungu-kichungaji, Bi. Csiszàr alibainisha, “Ni dhahiri leo kwamba taalimungu inajifunza jukumu lake katika Kanisa la sinodi na kuchangia mtindo wa sinodi.” Mikutano hii “husaidia kudhibiti wimbo wa msingi wa sinodi, taalimungu ya Watu wa Mungu.” Kwa sababu jumuiya ya wasomi wa taalimungu, inataka kuunga mkono kuzaliwa kwa Kanisa la sinodi,”alihitimisha

Padre Rush:Majibu ya kutangaza Injili katika mazingira mapya

Mtaalimungu wa Australia Padre  Ormond Rush alichota kwenye dhana ya tamaduni hai. Alisema, "ufunuo ulio hai sio tu ukweli tulivu, bali mazungumzo endelevu kati ya Mungu na wanadamu." Katika hotuba yake, alieleza kwamba katika kipindi hiki cha pili, wanaingia katika “mchakato wa mapokeo hai ya Kanisa, ili kutimiza ujumbe wa Injili.” Alisisitiza kuwa taalimungu ina kazi ya kusaidia Kanisa kufikisha ujumbe wa Mungu kwa kila mtu, huku pia ikisikiliza Sensus fidei (maana ya Imani ya kila mtu. Kwa upande wa Padre  Rushy, Kanisa leo lazima litafsiri "ishara, mifano, na jinsi Yesu anavyoungana na karne ya 21" kwa msaada wa taalimungu, "pia shukrani kwa Mtaguso wa Vatican II, ambayo inabaki kuwa nuru kwetu." Kuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati, “ni jambo la msingi kwa ufahamu mpya wa maono ya Mungu kuhusu maisha ya mwanadamu leo. Majibu mapya yanahitajika ili kuruhusu Kanisa kutangaza Injili kwa kusadikisha katika mazingira mapya linamoishi,” alimalizia.

Uwezo wa mafundisho wa maaskofu na mabaraza

Waandishi wa habari katika mkutano huo mfupi walilenga maswali yao katika mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa ufafanuzi wa uwezo wa kimafundisho kwenye Mabaraza ya Maaskofu, utafiti na uidhinishaji wa marekebisho katika sheria za kanuni, na jukumu la wataalimungu. Padre Vitali alikumbuka kwamba "hata hati hiyo ilizingatiwa kuwa kizuizi zaidi kuhusu uwezekano wa uhamishaji wa kazi za mafundisho" kutoka katikati hadi pembezoni, "yaani motu proprio Apostolos suos ya Papa Yohane Paulo II kutoka 1998, kwa hakika inasema katika kifungu cha  21 kwamba 'maaskofu ni waalimu wa kweli na madaktari wa imani kwa ajili ya waamini waliokabidhiwa uangalizi wao,' na inabainisha uwezo mahususi kwao, kama vile kusimamia uchapishaji wa katekisimu kwa ajili ya maeneo yao, hakika baada ya 'kuidhinishwa na Baraza la Kipapa.’ Zaidi ya hayo, kuna uandalizi muhimu pia katika Praedicate Evangelium ya Papa Francisko kuhusu jambo hili.” Padre Vitali alibainisha kwamba "ijapokuwa hawawezi kuunda mafundisho ya kidini, maaskofu wanaweza kushughulikia yote yanayohusu mafundisho, daima kuhakikisha wanatenda kwa ushirika na Papa."

Kusasisha kanuni za kisheria

Padre San José Prisco alikazia kwamba, kwa mtazamo wa kisheria, “huenda kukawa na upya.” Mambo kadhaa—kama vile mabaraza ya kichungaji au yale ya masuala ya kiuchumi, au mashirika ambayo yanatabiri ushirikiano kati ya wachungaji,watawa na walei— "ambapo Sinodi imepata makubaliano, yatawasilishwa kwa Papa katika hati ya mwisho, na inaweza kuona sasisho labda ifikapo msimu ujao wa joto." Hata hivyo, kwa habari nyinginezo, “tahadhari zaidi itatumiwa, kwa kuwa zitahitaji mashauriano zaidi.”

Hakuna maelewano katika baadhi ya masuala; mjadala haujafungwa

Kuna maswali, hasa kutoka katika mtazamo wa kitaalimungu ambayo huenda yasiwe na majibu ya uhakika mwishoni mwa Sinodi hii, kama vile masuala yanayohusiana na jinsia au huduma za wanawake. "Lakini kile ambacho lazima tuangalie kila wakati," Padre  Rush alieleza, “ni uwezo wa kupata mwafaka. Pale ambapo hakuna juu ya mambo fulani, ina maana kwamba mjadala lazima uendelee, si lazima ufungwe milele.” Padre Vitali aliunga mkono maoni haya, akisisitiza "mkutano wa sinodi hutoa dalili za upeo wa mtazamo  ambazo zinaoneshwa kwa makubaliano," na kwamba "mamlaka na uaminifu wa Sinodi lazima utofautishwe na jukumu la uhuru wa kufanya utafiti kwa wataalimungu, ambayo inaweza kuleta maelewano katika siku zijazo.”

Hati ya mwisho inayoeleweka kwa wote

“Kinachoeleweka waziwazi na kinachopatikana miongoni mwa akina baba na akina mama wa sinodi,” Dk. Ruffini alisema, “ni umakini wa lugha: sote tunafahamu kwamba tumeitwa kuandaa hati ya mwisho ambayo si lazim ipelekwe kwa Papa tu,  bali pia lazima ieleweke kwa Watu wote wa Mungu.” Akizungumza kutokana na uzoefu wake, Csiszàr alieleza umuhimu wa taalimungu katika Sinodi na katika “mabadilishano ya karama” kati ya tamaduni na mang’amuzi ya Ulaya Magharibi na Mashariki. "Sikuzote ni jambo la msingi kukumbuka mawazo," tukitafuta "kugeuza mafundisho kuwa vitendo na kuthamini jukumu la usindikizaji na utetezi wa utu wa binadamu ambao Kanisa linaweza kuwa nalo kwa Watu wa Mungu." Juu ya hili, Padre  Rush—akinukuu kifungu cha Mtaguso wa II wa Vatican—alisisitiza tena “ufunuo ni mazungumzo yenye kuendelea kati ya Mungu na wanadamu” na wataalimungu “wanaweza kulisaidia Kanisa kuendeleza mapokeo yake hai.”

17 October 2024, 09:07