Tafuta

Muhtasari wa Sinodi-Siku ya 14:Kuelekea Kanisa lililotengwa zaidi

Katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 18 Oktoba 2024,majadiliano yaliripotiwa juu ya uhusiano kati ya ndani na ulimwengu wote.Na Makardinali Aveline,Rueda Aparicio na Mulla walizungumza kuhusu umuhimu wa kazi ya Sinodi katika muktadha wa ulimwengu uliojaa mateso kwa waandishi wa habari mjini Vatican.

Na Edoardo Giribaldi, Roberto Paglialonga na Angella Rwezaula – Vatican.

Ugatuaji wa madaraka ni afya unapoongozwa na kanuni thabiti, ndiyo wazo lililokuwa kitovu cha muhtasari wa  kazi ya Sinodi  iliyoshughulikia mijadala ya tarehe 17 Oktoba  mchana na asubuhi ya tarehe 18 Oktoba 2024, ambapo Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari ya Sinodi, alitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Waandishi wa Habari katika  Ripoti hiyo  ambayo iliendelezwa na Bi Sheila Pires, Katibu wa Tume hiyo ya habari katika Ofisi ya Vyombo vya habari mjini Vatican.

Kufafanua upya dhana ya eneo

Majadiliano ya hivi majuzi yamejikita kwenye Sehemu ya III ya Instrumentum laboris, inayotolewa kwa  ajili ya "Maeneo." Dk. Ruffini alisisitiza kwamba uingiliaji kati mwingi ulisisitiza umuhimu wa makanisa mahalia, akibainisha kwamba hayadhuru, bali yanatumikia umoja kwa kuwa upekee wa utofauti wa  kila mmoja sio tishio bali ni zawadi maalum. “Mfano wa haya ni Makanisa ya Kikatoliki ya Mashariki, ambayo mapokeo yao lazima yalindwe kama hazina ya Kanisa Katoliki zima la ulimwengu wote na hivyo ni sehemu muhimu na ya lazima yake. Kwa hiyo, wengi walionesha haja si tu ya kuhakikisha kuendelea bali pia kuhuishwa kwa Makanisa Katoliki ya Mashariki, katika maeneo yao ya asili na katika diaspora. Wengine walibisha kwamba kumekuwa na uelewaji wa umoja katika historia ambao haukuwa sawa kabisa na kwamba nyakati fulani Kanisa la Kilatini lilitenda isivyo ya haki kuelekea Makanisa ya 'sui iuris' ya Mashariki, ikizingatia taalimungu yao kuwa ya pili." Leo hii, hata hivyo, mojawapo ya changamoto ni "kufafanua upya dhana ya eneo," ambalo "si nafasi tu ya kimwili." Kutokana na diaspora, "kuna Wakatoliki wa Mashariki wanaoishi katika maeneo ambayo Ibada ya Kilatini inatawala." Kuhusu suala lililojadiliwa sana la kusherehekea Pasaka katika tarehe moja swa na "Makanisa dada," Dk. alibainisha kuwa makubaliano yamefikiwa ili hili lifanyike mwaka ujao 2025. Hata hivyo, ombi liliibuka kutoka katika kusanyiko la "ujumbe kutoka katika Sinodi nzima kutaka tarehe ya pamoja ya kudumu."

Suala la Ugatuaji kutoka Roma hadi pembezoni

Ugatuaji kutoka Roma hadi pembezoni ulikuwa mada ya tafakari nyingi wakati wa vikao hivi vya sinodi, na kuvuta udadisi wa waandishi wa habari wakati wa mihutasari mbalimbali. Bi Pires alieleza kuwa vigezo vya kufafanua "ugatuaji wa madaraka kama afya unapoongozwa na kanuni thabiti" vilichanganuliwa, ikiwa ni pamoja na "ukaribu na sakramenti," ikimaanisha sakramenti. Jumuiya ndogo ndogo mahalia (mashinani) pia zilisisitizwa kama "nafasi za upendeleo kwa Kanisa la kisinodi." Kwa jumuiya hizi, ilibainishwa kuwa mazingira ya kidijitali yana umuhimu mkubwa, kwani yanaweza kuzisaidia kuziunganisha, "sio tu kiuhalisia bali pia kimaeneo."

Kutembea pamoja na walei

Hatua nyingi, ya Bi Pires aliyopoti, alihimiza kutoogopa sinodi, kwa sababu haidhoofishi karama na huduma mbalimbali wala umaalum wa maeneo. Kulikuwa na wito wa kuendeleza zaidi mada ya parokia, ambapo kazi za utawala huzuia shauku ya kimisionari, hivyo lazima tufikiri kwa ubunifu. Hasa, ni muhimu "kusikia vilio vya wale wanaoteseka, kama sinodi ya Kanisa  mahalia" pia inadhihirishwa katika "hali halisi inayooneshwa na mateso." Ili kupigana vita vizuri vya imani katika jamii zisizo na dini, kama alivyoshauri Mtakatifu Paulo, ni muhimu "kutembea pamoja na waamini," ilikumbukwa: "Ugatuaji mzuri wa Kanisa unaweza kuongeza mwelekeo wa uwajibikaji wa pamoja kati ya watu wa kanisa. Mungu," daima ndani ya mfumo wa umoja, "uaminifu kwa majisterio, ushirika wa kikanisa pamoja na mrithi wa Petro, heshima kwa Makanisa ya mahali, matawi madogo, na sinodi." Injili lazima "imwilishwe katika kila utamaduni na kila mahali, ikikaa na kuimarisha mwelekeo wa jumuiya ya harakati na ukweli mpya wa kikanisa." Uingiliaji kati ulioshangiliwa sana, Bi Pires alibainisha, ulisisitiza wito wa Kanisa wa "umoja katika utofauti," akielezea kuwa ni  kama  "kiumbe hai na Kristo na moyo wake, na anaishi kama mwili kwa kuwepo kwa watu wake."

Kuwakaribisha wanawake na vijana

Kuhusu suala la ushemasi wa kike, baadhi ya maoni yalisisitiza kwamba “Kanisa lazima lisiwe jambo la ‘wanaume pekee yake ’ na kwamba, ingawa wanawake wanaomba kushirikishwa katika mchakato wa kufanya maamuzi, hilo pekee halitoshi. Ikiwa vijana wanasema "wao ni wa kiroho lakini si wa kidini," hii inapaswa kuchochea Kanisa kuwa "wachungaji hata katika nafasi za digitali," ambapo vijana wa kiume na wa kike hutumia muda wao na kuingiliana. Akihitimisha, Dk. Ruffini alitangaza kwamba alasiti ya  tarehe 18 Oktoba, pamoja na mikutano ya vikundi kazi, kungekuwa na  kikao cha tume ya sheria ya kanuni na kingine cha SECAM, Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar, ambacho kina jukumu la kupambanua mambo ya kitaalimungu na kichungaji kuhusu mitala. Juma lijalo iltakuwa la maamuzi katika majadiliano juu ya rasimu ya hati ya mwisho, ambayo, kama Kardinali Mario Grech alivyosema asubuhi ya Okotba 18, kwamba “itahitaji kushughulikiwa katika hali ya maombi mamazitokali.Kwa sababu hii,” Dl Ruffini aliongeza, kikao cha Jumatatu 21 Oktoba kitaanza saa 2:30 asubuhi kwa Misa ya kujiweka katika Roho Mtakatifu katika  Madhabahu ya Kiti cha Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Changamoto za  Mediterania

Kutoka Mediterania hadi Afrika, na Amerika ya Kusini, maeneo ya mbali ya kijiografia yameunganishwa na changamoto zinazofanana na nia ya pamoja ya kuzitatua. Huu ndio ulikuwa mwongozo wa kawaida unaounganisha uingiliaji kati na maswali yaliyofuata yaliyoulizwa kwa washiriki wa mkutano huo. Kardinali Jean-Marc Aveline wa Marseille, Ufaransa, alikuwa wa kwanza kuzungumza. Amebainisha wajibu wake katika kuratibu juhudi za Kanisa katika eneo la Mediterania, utume aliopewa na Baba Mtakatifu Francisko. Kardinali alifuatilia ratiba ya ahadi yake, ambayo ilianza mwaka wa 2020 na maaskofu wapatao arobaini na kuendelea kupitia mikutano mingine, ikiwa ni pamoja na Septemba 2023, wakati Papa Francisko "alipoelezea nia yake ya kuendelea, kuratibu, na kuunga mkono kazi hii." Lengo limekuwa hasa katika kusikiliza matatizo ya jumuiya mbalimbali za kikanisa. "Bahari ya Mediterania sio tu mada ya kusoma," Kardinali Aveline alisema, "lakini eneo ambalo matukio ya kushangaza yanajitokeza: vita, ukiukwaji wa uhuru, ufisadi," bila kusahau uhamiaji, ambayo mitandao ya usaidizi iliyojitolea imeundwa. "Lazima tuelewe jinsi Kanisa linaweza kuchangia katika juhudi za haki na amani katika eneo hili," Kardinali Aveline alisisitiza, akikumbuka pendekezo lake la uwezekano wa Sinodi inayotolewa kwa ajili ya Mediterania.

Mateso na matumaini katika bara la Amerika Kusini

Kisha, Kardinali Luis José Rueda Aparicio wa Jimbo Kuu la Bogotá, Colombia, alizungumza kuhusu uzoefu wa imani katika nchi yake na Amerika ya Kusini yote,  kwamba ni "bara changa" lenye "mateso na matumaini." Kanisa mahalia linajitahidi kusitawisha “hali ya kiroho inayozidi kuwa karibu na maskini,” umaskini ukiwa ni suala linalochochewa sio tu na kuhama kuelekea Amerika Kaskazini bali pia na matatizo yanayohusiana na uuzaji  wa dawa za kulevya. Katika mazingira haya yenye changamoto, “Kanisa limeweza kuungana na kutafuta njia za kuukabili ukweli, likitafuta kuutazama kwa mtazamamo wa imani na matumaini. Matokeo yake, kwa maoni ya Kardinali, ni "uwepo wa Ufalme" madhubuti, unaolenga kupanua ili kufikia "uinjilishaji muhimu" katika bara zima.

Mapambano nchini Sudan Kusini

Kardinali Stephen Ameyu Martin Mulla, Askofu Mkuu wa Juba, nchini Sudan Kusini, alizungumza baadaye, changamoto zinazoikabili nchi yake na nchi jirani ya Sudan. Alisema watu wa Sudan Kusini wamepigana vita katika kutafuta uhuru, na kujikuta bado wako mbali na amani, wakikabiliwa na masuala mengi ambayo hayajatatuliwa. Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini nchini Sudan Kusini yamesalia kutekelezwa kwa sehemu tu- mada iliyoibuliwa na wajumbe wa ngazi ya juu katika mkutano wa kihistoria na Papa Francisko mwaka 2018. Tangu wakati huo, hata hivyo, kidogo imebadilika, hata baada ya ziara ya Papa katika nchi ya Afrika. Kwa sababu hiyo, Askofu Mkuu alisema, anaamini mazungumzo ya sinodi yanaweza kushughulikia masuala ya kijamii na kisiasa yanayotukabili. Janga jingine linalolikumba taifa hilo ni ongezeko la joto duniani. Kardinali Mulla alitoa mfano wa mji wa Bentiu, ambao sasa umejaa maji kabisa kutokana na mvua kubwa inayonyesha nchini Sudan Kusini. Katika ulimwengu unaozidi kuunganishwa, kulingana na Askofu Mkuu wa Juba, hakuna mtu anayeweza kusema kuwa shida kama hizo hazihusiani nazo.

Shauku inayozunguka sinodi

Mwisho, Askofu Luis Marín De San Martín, Augustino na Katibu Msaidizi wa Sekretarieti Kuu ya Sinodi na mjumbe wa Tume ya Habari, aliakisi changamoto zinazoukabili ulimwengu, kama ilivyoakiswa katika sehemu za  awali. Alieleza jinsi ambavyo  Sinodi "inajibu" kwa maswali haya, kwa kukuza Kanisa wazi na lugha wazi inayoweza kushughulikia masuala ya leo. Askofu alitaja nguzo nne za kimsingi ambazo Kanisa lazima lisimame juu yake: lazima liwe na msingi wa Kristo, wa kindugu, umoja (“Wale wanaoona ugomvi wa madaraka ndani ya Mkutano wa Sinodi wamekosea; kwani hili halipo,” aliongeza askofu huyo), na mwenye nguvu. "Laiti tungeweza kushirikisha shauku yetu katika ulimwengu uliojaa majanga." Majadiliano ya Sinodi, wakati huo huo, yamejikita katika mijadala kadhaa: sinodi na kusikiliza alama za nyakati, umoja na utofauti, katikati na pembeni. Wito wa mwisho wa Katibu mkuu haukupaswa kukatishwa tamaa na "tamaa ambayo wakati mwingine hutushika."

Majibu ya papo hapo

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, nafasi ya kawaida ilitolewa kwa maswali ya waandishi wa habari. Akihutubia katika utekelezaji wa dhana ya “umoja katika utofauti,” Kardinali Rueda Aparicio alidokeza kwamba dhana hii tayari inaakisiwa katika “mtindo mpya na wa kibunifu wa Sinodi,” ambapo uwepo wa wajumbe wa Sinodi wanawake ndiyo ishara inayoonekana zaidi ya “ubunifu na mambo mapya ya  maendeleo." Juu ya mada ya kujibu wale wanaodai majibu ya haraka kutoka katika Sinodi, Askofu Marín de San Martín alilinganisha na imani yenyewe ya Kikristo: "Ni uzoefu wa Kristo. Ikiwa hatuuishi, hatutaweza kuufahamu kikamilifu. " Hata hivyo, Askofu Magostino alisisitiza kwamba mchakato mzima wa sinodi lazima ubaki kuwa wa kufikirika bali "mzizi wenyewe katika uhalisia." Katika muktadha huu, parokia zinabaki kuwa muhimu kama "jumuiya za msingi."

Hati ya mwisho

Washiriki pia waliulizwa kuhusu majadiliano kuhusu jukumu na mamlaka ya maaskofu. "Imejadiliwa sana," alikiri Kardinali wa Colombia, akitaja imani ya Mtakatifu Yohane  XXIII kwamba amana ya imani inabaki "siku zote zile zile," lakini "lazima ibadilishwe kwa kila hali." Askofu Mkuu wa Bogotá pia aligusia matatizo yanayokabili nchi yake, ikiwa ni pamoja na "mgawanyiko wa sumu," ambao umesababisha jumuiya zenye maoni sawa kuwa "maadui" wa mtu mwingine. Kisha Kardinali Aveline alitoa ufahamu kuhusu uandikaji wa hati ya mwisho ya Sinodi. "Tume yake ya awali," alisema, inalenga "kuhakikisha kwamba maandishi yaliyopendekezwa ya kupiga kura hayaendi mbali sana na maoni yaliyotolewa wakati wa wmajuma haya ya kazi."

18 October 2024, 17:40