Papa akutana na Bw.Sadyr Zhaparov,Rais wa Kyrgyzstan
Vatican News
Papa Francisko na Rais Sadyr Zhaparov,Rais wa Kyrgyzstan Ijumaa tarehe 4 Okotba 2024 walikutana mapema asubuhi kwa takriban dakika 20, mjini Vatican kisha kwa mujibu wa itifaki mkutano wa rais uliendelea katika Sekretarieti ya Vatican na Kardinali Pietro Parolin akiwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Wakati wa mazungumzo yao yalikuwa mazuri kama ilivyo wasilishwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican kwamba “mahusiano mazuri kati ya Vatican na Kyrgyzstan yaliakisiwa hasa juu ya ushirikiano wa pamoja katika nyanja za afya, elimu na kiutamaduni na katika nyanja kadhaa za maisha ya Kanisa mahalia.” Kisha kulikuwa na "mabadilishano ya maoni juu ya mambo ya sasa ya kimataifa, kwa kuzingatia migogoro inayoendelea na masuala ya kibinadamu, kuonesha umuhimu wa kujitolea kwa haraka kwa kukuza amani.”
Zawadi
Mbali na mapambo ya kiasili yaliyotengenezwa kiikolojia katika milima ya nchi hiyo, Rais Zhaparov alimpatia Papa mchoro unaoonesha Basilika ya Mtakatifu Petro iliyotengenezwa kwa pamba za rangi na huduma ya chai iliyotengezwa kwa ufundi, wa fedha kutoka katika migodi ya ndani.
Papa Francisko alijibu kwa kutoa sanamu yaudongo yenye kichwa "Upendo na Huruma," nakala ya kitabu cha picha kwenye Jumba la Kitume na kilichokuwa na ujumbe wa amani wa mwaka huu 2024.