Papa amekutana na Mswati III, Mfalme wa Eswatini
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Mfalme Mswati III, Mfalme wa Eswatini mjini Vatican Ijumaa tarehe 18 Oktoba 2024. Alifika saa 4.25 asubuhi na kumaliza mazungumzo yao yote saa 4.45 asubuhi na kuondoka saa 4.55.
Zawadi
Wakati wa kupeana zawadi, Baba Mtakatifu amempatia sanamu yenye sura ya Mtakatifu Petro anayebariki, huku ikionesha paa la Basilika ya Mtakatifu Petro. Ujumbe wa amani kwa mwaka 2024, vitabu vya hati za kipapa, kimoja chenye katekesi za Papa kilichohaririwa na Mkuu wa Nyumba ya Kipapa.
Kwa upande wa Mfalme: Chessboard ya mbao na kioo, kazi ya ufundi wa ndani. Sanamu ya chuma ya dhahabu inayoonesha simba, Vikombe viwili vya glasi na fedha na baadhi ya bidhaa za asili za utunzaji wa kibinafsi, zilizotengenezwa nchini Eswatini.