Papa amepokea hati za utambulisho wa Balozi kutoka kwa Umoja wa Ulaya
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 3 Oktoba 2024 amepokea hati za Utambulisho kutoka kwa Bwana Martini Selmayr, ambaye ni Balozi wa Umoja wa Ulaya(UE), kuuwakilisha Umoja huo mjini Vatican. Alizaliwa tarehe 5 Desemba 1970 huko Bonn nchini Ujerumani. Ameoa.
Masomo
Alisomea sheria katika Chuo Kikuu cha Passau (Ujerumani), katika Chuo cha Mfalme London na Chuo Kikuu cha Geneva(Uswiss) (1990 - 2000). Alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria mwaka 2001 kutoka Chuo Kikuu cha Passau.
Alishikilia, kati ya nyadhifa nyingine zifuatazo:
Mshauri wa kisheria katika Benki Kuu ya Ulaya (1998 - 2000),Mkuu wa Ofisi na Makamu wa Rais wa Bertelsmann AG, Bruxessels, Ubelgiji (2001 - 2004). Msemaji wa Tume ya Ulaya kwa Jumuiya ya Habari na Vyombo vya Habari (2004 - 2010). Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya na Kamishna wa Haki, Haki za Msingi na Uraia wa Umoja wa Ulaya (2010 - 2014). Mkuu wa Baraza la Mawaziri la Rais wa Tume ya Ulaya (2014 - 2018); Katibu Mkuu wa Tume ya Ulaya (2018 - 2019), hadi uteuzi alikuwa Mkuu wa Uwakilishi wa Tume ya Ulaya nchini Austria (2019 - 2024).