Siku ya 98 ya Kimisionari,Video ya PMS:kupeleka tumani,imani na mapendo!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika ujumbe kwa njia ya video uliotolewa na Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa (PMS) kwa ajili ya Maadhimisho ya Siku ya 98 ya Kimissionari Ulimwenguni kwa mwaka 2024 inayoadhimishwa Dominika tarehe 20 Oktoba 2024, ikiongozwa na kauli mbiu: “Enendeni na alikeni kila mtu kwenye Karamu” (Rej. Mt. 22:9) inaanza na sauti kuwa: “Tunapoanza safari hii pamoja, tunawaomba msiwe watazamaji tu bali washiriki hai katika utume huu. Zaidi ya mwaliko ni Wito wa kuwa sehemu ya jambo kubwa zaidi. Huu ni wakati wetu: kwa pamoja tunaweza kuleta tumaini, imani na mapendo katika pembe zote za dunia."
Kwa mujibu wa maelezo yanayosindikiza video hiyo iliyoundwa kwa ushirikiano na Wasimamizi wa PMS waliotawanyika ulimwenguni kote ni kwamba: “Karamu ni sherehe ya jumuiya, mazungumzo ya wazi ya imani na ushuhuda wa kujitolea kwetu kuwakaribisha kaka zetu na dada, kwanza dada kutoka pembezoni mwa jamii.” Katika takriban dakika tatu za video, hiyo inayopatikana katika lugha tofauti, picha za kazi za utume wa kimisionari zilizotawanyika ulimwenguni kote, huku nyuso na sauti za wamisionari wanaume na wanawake, wakurugenzi wa kitaifa na walei wanaohusika na PMS na, kama mgeni wa kipekee, Kardinali Soane Patita Paini Mafi, Askofu wa Tonga, huko Polynesia zinasikika.
Katika uingiliaji kati mfupi, maneno ya enendeni, alikeni, kutangazeni Injili, sherehekea, shiriki, haki, furaha na udugu hujirudia kwenye mipaka ya uinjilishaji upya. Kwa upande wa rais wa PMS, Askofu Mkuu Emilio Nappa, alisema: “dhamira ni kwenda na kutangaza Injili. Kila kitu tunachofanywa husaidia kufanya hili kuwezekana. Injili ndiyo inayotuongoza na kazi ya Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa ni kukuza ufahamu wa utume na wakati huo huo kuvuna matunda ya kiroho na sadaka za fedha na kisha kuyagawanya upya kadiri ya mahitaji ya Makanisa mahalia.”
Wito huo, aliongeza Askofu Mkuu Nappa, “unatusukuma leo hii pia kwenye mpaka wa uinjilishaji mpya wa Makanisa ya Kikristo ya kale, hasa katika nchi za Magharibi ambako idadi ya Wakristo inapungua.” Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa, alisisitiza kwamba “Unjilishaji maana yake ya kweli ni kuzama katika utamaduni wa wengine ili kugundua tunu za Injili pamoja. PMS ni hazina kubwa, pia kutokana na sinodi ya asili na mapokeo yao, ambayo wanaendelea kufanya kazi katika huduma ya Kanisa la Ulimwengu wote na kwa jina na kwa niaba ya Papa.”