Mhutasari wa Sinodi: fursa katika utofauti!
Na Lorena Leonardi, Roberto Paglialonga na Angella Rwezaula - Vatican.
Kazi ya sinodi ilifunguliwa asubuhi katika Ukumbi wa Paulo VI kwa kuanza na kumkumbuka José Carlos de Sousa - mshairi wa Kibrazili aliyeishi katika umaskini chini ya nguzo ya Uwanja wa Mtakatifu Petro, aliyefariki mwezi Agosti na ambaye mazishi yake yaliadhimishwa Jumanne tarehe 15 Oktoba 2024. Hayo yaliripotiwa na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari, katika mkutano na waandishi wa habari ulioanza saa 7.30 mchana katika Chumba cha Waandishi wa Habari mjini Vatican na kutambulishwa na naibu Msemaji wa Vyombo vya habari Bi Cristiane Murray. Dk. Ruffini pia alikumbusha kwamba saa 12.30 za jioni kutakuwa na onesho, katika Ukumbi mpya wa Sinodi, wa filamu ya “Io Capitano”, iliyoongozwa na Matteo Garrone aliyepo na baadhi ya wahusika wakuu - kwa mpango wa Baraza la Kipapa la utamaduni na elimu. Na pia alitangaza kwamba alasiri Jumatatu tarehe 14 Oktoba na asubuhi ya Jumanne tarehe 15 Oktoba, kulikuwa na washiriki 347 kwenye Ukumbi, kila wakati wakiwa na shughuli nyingi za vikundividogo.
Maeneo ya uhusiano kama nafasi za mikutano
Asubuhi ya tarehe 15 Oktoba “hasa kulikuwa na sala na tafakari za zilizotolewa na Sr Maria Ignazia Angelini na ripoti ya Kardinali Hollerich” kwa mujibu wa Sheila Pires, katibu wa Tume ya Habari. Kuhusu kutafakari kwa mtawa wa Kibenediktini, Bi Pires alikazia baadhi ya mambo. Kwanza kabisa “mizizi ya kikanisa nayo ni kwamba Kanisa lazima limwilishwe katika mazingira halisi. Kwa hiyo,mabadiliko ya Injili, yenye mahali pa mahusiano yanayowakilisha nafasi za kukutana na wanadamu ambapo Injili inaweza kuishi na kutangazwa” ilikuwa katikati ya tafakari hiyo
Maono yenye nguvu
Kwa upnade wa Kardinali Hollerich katika ripoti yake alisisitiza “umuhimu wa Sehemu ya III ya Instrumentum laboris, iliyowekwa kwa Maeneo” Na, aliongeza Dk. Ruffini kwamba “ni mjadala katika uthabiti wa maeneo ya utume kwa kuangalia miji midogo na miji mikubwa, katika maono ambayo sio ya utulivu lakini yenye nguvu ambayo pia yanajumuisha uhamiaji.” Pamoja na tafakari ya maeneo ya kutembea pamoja, vifungo vinavyotoa sura ya umoja wa Kanisa na huduma kwa umoja wa askofu wa Roma vilikaziwa. Katika Vipengele hivyo, mwandishi mkuu Kardinali alisema katika hotuba yake, “vinatualika kuzingatia ukweli wa muktadha ambao uhusiano una uzoefu, dhidi ya wazo la ulimwengu wa kufikirika.” Kwa kupngeza Bi Pires alisema, “Kanisa haliwezi kueleweka bila kuwa na mizizi katika mahali na utamaduni. Na hatua nyingine muhimu ni utambuzi wa uhusiano kati ya mahali na tamaduni, kwani sio vyombo tofauti lakini vimeunganishwa.” Kwa kuhitimisha katibu wa Tume ya Habari alisema kwamba: “Kardinali Hollerich alitualika kutafakari juu ya uzoefu wa pamoja, akisisitiza jinsi ukuaji wa mahusiano ndani ya Ukumbi wa Paulo VI ulivyoboresha nyinyi nyote na pia aliwakumbusha wajumbe wa sinodi kutoweka uzoefu huu wao wenyewe bali kuhakikisha kwamba utajiri wa mkutano wa sinodi unapatikana kwa watu wa Mungu.”
Kutazama mbele na kuendelea na safari
Sr Nirmala Alex Maria Nazareth, Mkuu wa Shirika la Masista wa Karmeli wa Kitume, alisema wakati katikaka chumba cha waandishi wa habari kuhusu Sinodi kwamba “Ni utajiri unaokua katika utofauti ambao unashuhudiwa na kupumuliwa kwenye Sinodi: uzoefu wa kipekee. Huku Akihimizwa na naibu msemaji wa Vyombo vya habari Bi Cristiane Murray, mtawa wa Kihindi alizungumzia fursa ya ajabu ambayo inatolewa kwa washiriki katika mkutano wa sinodi ili kuweza kuingia katika uhusiano na wawakilishi wengi na washiriki wa Makanisa mahalia kutoka duniani kote. “Maneno tuliyoyasikia kwenye mafungo na katika tafakari za Padre Timothy Radcliffe na Sr Maria Ignazia Angelini yanatuhuisha katika roho ya sinodi. Sasa itakuwa muhimu kwetu kuelewa jinsi ya kuendana na Makanisa ya mataifa yetu, mara tutakaporudi nyumbani, hata ikiwa tayari tumefarijiwa na yale ambayo Mama Teresa wa Calcutta alisema, yaani, tunaitwa kushirikiana katika neema ya Mungu. Lakini tayari sasa, tunahisi tuna matumaini makubwa: tumeanza safari na hatuwezi kurudi nyuma, tu kuangalia mbele na kuendelea na safari. Changamoto ya kweli, kwa utambuzi, itakuwa kuelewa jinsi ya kuifanya bora,”.alihitimisha Sr Nirmala.
Kanisa lazima liweke mizizi
Kardinali Mfransiskani Leonardo Ulrich Steiner, wa Jimbo Kuu la Manaus, Brazili, alizungumza kuhusu “njia mpya zinazofunguka na zinazotusaidia kuelewa sinodi ni nini hasa. Kinachozaliwa ni njia mpya ya kuwa Kanisa kutangaza Ufalme wa Mungu na Injili. Na huu ni mchakato ambao tutaitwa kuishi pia na zaidi ya yote baada ya Sinodi. Nchini Brazili, kwa mfano, ni mchakato ambao tayari umeanza: wanawake wengi katika Amazonia tayari ni viongozi wa jumuiya zao, kuna mashemasi wengi wa kudumu, kwa ufupi, kila mtu anashiriki katika maisha ya jumuiya kwa njia hai. Kile tunachopitia hapa, kwa hiyo, hutusaidia kuelewa sinodi katika Kanisa letu mahalia vizuri zaidi. Kwa kumalizia, ninaamini kwamba tumeitwa kupata uzoefu wa tamaduni na dini zaidi na zaidi, kwa sababu Kanisa lazima liweke mizizi. Maeneo, ambayo yanajumuisha mada kipengle cha 4 ya kazi ya sinodi, kwa hivyo, ni yale "ambayo tunaishi maisha yetu ya kila siku na ambayo hutusaidia kuelewa jukumu letu ndani ya Kanisa: kwa mfano, hebu tujiulize mahali pa mikutano ya maaskofu ni nini, mahali pa wahamiaji...na kadhalika”, alitoa maoni yake” Kardinali huyo.
Uamsho wa Kiinjili
“Kuelewa jinsi ya kuzindua upya ujumbe wa Injili kwa uthabiti ni mojawapo ya changamoto kuu ambazo zinajitokeza na zitatokea wakati wa kazi ya siku hizi, na ambazo tutazipeleka kwa Makanisa yetu ya mahali. Hayo yaliungwa mkono na Kardinali mteule Roberto Repole, Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Torino na askofu wa Susa, ambaye aliibua siri katika Kanisa lake kwamba wanapitia mambo ya mabadiliko yanayohitaji kusomwa pia kwa kuzingatia sinodi yenye uzoefu hapa Roma, na ambayo kwa upande mwingine, hata hivyo, inamsaidia kuelewa zaidi kile kinachotokea katika Ukumbi wa Paulo VI.” Kardinali Mteule Repole, katika uzoefu wake, aliguswa hasa na baadhi ya vipengele: “Kwanza kabisa, wasifu wa kiroho wa washiriki: inajitokeza wazi kwamba tunatafuta sauti ya Roho pia katika sauti ya kaka na dada ambao wako karibu nasi. Pili, kuongezeka kwa ujuzi kati ya wajumbe, ambayo hutufanya kuelewa jinsi neno la kila mtu kweli lina kitu maalum, katika utofauti wake ikilinganishwa na lile ya wengine. Hatimaye, “Ukatoliki wa Kanisa unaweza kuonekana kwa vitendo, ambalo kwa hakika linapumua tamaduni zote na liko tayari kutoa Injili hata kwa tamaduni mbalimbali,” alihilimisha.
Hali ya tabianchi nchini Brazil
Nafasi ilitolewa kwa maswali kutoka kwa waandishi wa habari, ambao waliwauliza wageni hasa kuhusu mazingira, uhusiano na Sinodi ya Amazonia, nafasi ya wanawake ndani ya Kanisa na ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu. Akizungumzia hali ya dharura ya hali ya tabianchi, Kardinali Steiner aliripoti hali mbaya ambayo Amazonia inapitia kwa sasa kutokana na ukosefu wa mvua: “Tumekuwa bila maji kwa mwezi mmoja, mito mikubwa haiwezi kupitika tena na bila mzunguko wa mto unaotumika jamii nyingi zinaendelea kufikiwa. Zaidi ya hayo, uhaba wa maji pia una athari kwa maeneo mengine ya Brazili. Uvuvi wa kuwinda na uchafuzi wa maji kutokana na zebaki hukamilisha picha ya hatari ya mazingira ambayo inalemea mfumo wa ikolojia dhaifu ambao unahitaji kulindwa. Hata kama hatushughulikii hasa tunajua kwamba mazingira ni sehemu ya sinodi kulingana na Papa Francisko, ambaye katika Waraka wa Querida Amazonia anaelezea kwa undani hali ya kweli yake. Pia tunaishughulikia mada hiyo kwa umakini katika ngazi ya majimbo.” Akijibu swali kuhusu mwendelezo wa Sinodi ya Amazonia, Kardinali alisema kwamba iliweka misingi ya mkutano unaoendelea:”Sinodi haina faida, tunaingia katika harakati ambalo ni Kanisa letu, tukialikwa kushiriki katika njia ya kuwa kanisa kwa njia ya ubatizo, ambapo kila mtu lazima ajisikie kuwajibika kwa utume. Nimeishi Amazonia kwa miaka mitano na nimekuwa nikiishi mchakato huu kwa miaka 50: tumeshauriana zaidi ya jumuiya elfu moja ili kuelewa jinsi ya kuwa wamisionari zaidi, shukrani zaidi kwa mtikisiko wa waamini.”
Shughuli ya wanawake katika kanisa la Brazil
Kuhusu jukumu muhimu la wanawake katika Kanisa, Kardinali Steiner alisisitiza jinsi katika eneo la Brazil anakotoka ambako watu wameishi bila mapadre kwa zaidi ya miaka 100 , jumuiya zimejipanga na kuendelea kusali. Wanawake wamekuwa wa msingi katika mchakato huu. Wengi, katika jimbo kuu lisilo na kikomo lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba elfu 90, wanasimamia jumuiya, wanapokea huduma pia kwa ajili ya Ekaristi na neno la Mungu, wanafanya bidii katika Caritas, katika uchungaji wa gerezani, na watu mitaani.”Inakabiliwa na idadi kubwa ya waamini, katika jiji la Manaus pekee kuna milioni 2 na 300 elfu, ambapo elfu 30 ni Venezuela na 75 elfu wa asili - na haja kubwa ya kukutana na tamaduni tofauti, sehemu ya kike sio ya pili, wanawake, wanawakilisha Kanisa letu, ambalo lisingekuwa hivyo bila wao. Na juu ya mada iliyojadiliwa sana ya ushemasi wa kike alisema: “Tungependa ikiwa hata jumuiya za mbali zaidi zingeweza kusherehekea baadhi ya sakramenti, kama vile ubatizo. Wengi wa wanawake wetu ni mashemasi wa kweli, kwetu sisi ni mashemasi katika mambo yote hata kama sio rasmi.” Hatuna neno kwa jukumu, lakini wanafanya hivyo na inapendeza.
Kwa nini usirudishwe ushemasi wa kike aliyewekwa rasmi?
“Tayari tumekuwa na Kanisa lenye sura hii, shemasi wa kike anaweza kwenda sambamba na yule wa kiume.” Siamini kwamba suala hilo ni la jinsia, badala ya wito.” Kwa swali lingine juu ya uwezekano wa wanawake kuongoza mahubiri, Askofu mkuu alijibu kwamba “katika adhimisho la Neno la Mungu, tafakari, siku zote hufanywa na Mungu, sio mwanamume au mwanamke anayetafakari, ikiwa kuna kitu chochote kinachosaidia kufanya hivyo. Kwa upande wa Kardinali Mteule Repole alimuunga mkono katika mada: “Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican unaposhughulika na Ekaristi, unaifafanua kuwa ni “kilele cha maisha ya Kikristo.”Ikiwa tunazungumza juu ya mkutano wa kilele, inamaanisha kuwa kuna kitu chini yake. Kuna wataalimungu wengi, katekisimu iko mikononi mwa wanawake zaidi ya yote: hitaji sio la nafasi bali jukumu la pamoja kati ya kila mtu.”
Utajiri wa aina za huduma
Kwa swali juu ya useja wa mapadre - moja ya mada iliyojadiliwa zaidi mnamo 2019 katika Sinodi Maalum ya Kanda ya Amazoni, Askofu mkuu wa Brazil alibainisha juu ya ugumu wa kufanya kazi na mapadre 172 tu kwa jamii elfu, na hitaji la kukuza zaidi. uhusiano kati ya jumuiya na wahudumu. Kuhusu suala hilo, Kardinali mteule Repole aliongeza kwamba tayari katika mkutano wa sinodi, kutokana na uwepo wa maaskofu wa Makanisa ya Mashariki, walioolewa, kuna aina nyingi za huduma, huku mtawa wa Kihindi akidhania kwamba masuala katika nchi yao, muda zaidi unaweza kuhitajika. Katika kurejea ya hujumuishwaji wa walemavu ilitolewa na Dk. Ruffini, akijibu swali kwamba: "Angalau katika mzunguko wangu, inajadiliwa, tutaona ikiwa itajadiliwa katika mkutano mkuu katika siku chache zijazo. Mada hiyo hakika iko karibu na moyo wa kila mtu na mengi zaidi yanaweza kufanywa. Lakini tunapozungumzia watoto wadogo, waliotengwa, tunazungumzia pia watu wenye ulemavu." Hatimaye, swali kutoka kwa waandishi wa habari kuhusu mazishi ya mshairi asiye na makazi José Carlos de Sousa liliulizwa kwa Kardinali Steiner, ambaye aliadhimisha pamoja nao asubuhi ya tarehe 15 Oktoba 2024. "Niliposikia jinsi anavyoishi, sikuweza kujizuia kwenda. Niliguswa, wakati jeneza likiingia kwenye gari, kuona marafiki wa José Carlos, wasafiri wenzake, kila mmoja akikabidhi ua." Katika umaskini, karibu hakuna chochote, "udugu wa kina wa kiinjili upo. Uzima wa Mungu hustawi hata katika kifo" alihitimisha.