Tafuta

Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican 2-27 Oktoba 2024. Sinodi ya Maaskofu mjini Vatican 2-27 Oktoba 2024.  (Vatican Media)

Sinodi inawaombea wahanga wa vita,Kard.Grech:tuwasikilize wanaoteseka chini ya mabomu!

Tuko ukingoni mwa migogoro inayozidi kuongezeka,ndiyo maneno ya mwanzo wa salamu za Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu kwenye Mkutano Mkuu wa XVI,Oktoba 2 katika Ukumbi wa Paulo VI kwa uwepo wa Papa.Kardinali Hollerich:kikao cha I na II ni tofauti.Wawakilishi wa Vikundi 10 vya Utafiti vilivyoanzishwa na Papa viliwasilisha programu zao.

Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Mario Grech, katibu mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, alifungua mkutano mkuu wa kwanza wa mkutano mkuu wa XVI wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu, kuanzia tarehe 2 hadi 27 Oktoba 2024 , kwa kuangalia matukio ya sasa. Kwanza  ilikuwa ni kukaribishwa tena "kwa wajumbe wote 368, kutoka duniani kote, ambao walikutana baada ya mwaka mmoja kwenye meza za mduara za Ukumbi wa Paulo VI. Kisha, mara moja, wazo la kaka  na dada waliokandamizwa na migogoro.

Kuongezeka kwa mvutano kutokana na migogoro

“Tunapoadhimisha Mkutano huu, vita vinaendelea katika sehemu nyingi za dunia! Tuko kwenye ukingo wa kupanuka kwa mzozo”, alisema Kardinali huyo kutoka Malta akiwa mezani na Baba Mtakatifu Francisko, chini ya Mtazamo wa Nakala ya Picha ya Maria Salus Populi Romani. “Ni vizazi vingapi vitalazimika kupita kabla ya watu walio kwenye vita 'kuketi pamoja' tena na kuzungumza wao kwa wao, ili kujenga wakati ujao wenye amani pamoja? lilikuwa ni swali lake.

Zawadi ya amani

Kwa hiyo akina baba na akina mama wa Sinodi ungana na kaka na dada waliopo kwenye chumba kutoka maeneo ya vita au mataifa ambao wanaona uhuru wa kimsingi wa watu umekiukwa. Kupitia sauti zao tunaweza kusikia kilio cha wale wanaoteseka chini ya mabomu, hasa watoto, ambao wanapumua hali hii ya chuki”, alisema Kardinali Grech. “Kama waamini tunaitwa kutamani na kuomba kwa ajili ya zawadi ya thamani ya amani kwa ajili ya watu wote.”

Ushuhuda wa kuaminika

“Maombi haya yasiyokoma lazima yaunganishwe na ushuhuda wa kuaminika. Na Mkutano wa Sinodi yenyewe ni ushuhuda wa kuaminika: Ukweli kwamba wanaume na wanawake wamekusanyika kutoka katika sehemu zote za dunia ili kumsikiliza Roho kwa kusikilizana ni ishara ya kupingana kwa ulimwengu,” alisisitiza Kardinali. “Kanisa la kisinodi ni pendekezo kwa jamii ya leo na mang'amuzi ni daraja ambalo waamini na wasioamini wanaweza kusikilizana na kuelewana kwa kutumia sarufi ya kawaida,  aliongeza Kardinali Grech, akimnukuu Umberto Eco, mwandishi wa  vitabu wa Italia.

Sio mabadiliko ya kimuundo, lakini inasikiliza

Kardinali Grech aidha alijikita katika utume wa Mkutano huo kwamba: “Wengi wanafikiri kwamba madhumuni ya Sinodi ni mabadiliko ya kimuundo katika Kanisa na mageuzi. Huu ni wasiwasi unaozunguka Kanisa zima, lakini sio kila mtu ana wazo sawa la mageuzi na vipaumbele vyake.” Badala yake, ni mwelekeo wa kusikiliza, ni wa msingi, katikati ya hatua zote za mchakato: kutoka katika mashauriano ya Makanisa mahalia, hadi yale ya Mabaraza ya Maaskofu, kutoka katika Mabaraza ya Bara hadi kikao cha 2023 karibu na Baba Mtakatifu. Kwa kuorodheshwa kwa njia hiyo, hatua zinaonekana kusadikisha mchakato wa kipaumbele ambapo Watu wa Mungu huonekana mwanzoni tu, kutoa udanganyifu wa kushiriki katika mchakato wa kufanya maamuzi ambao hata hivyo unabaki kujilimbikizia mikononi mwa  walio wachache,”ndiyo ulikuwa ni mtazamo wa  Kardinali huyo. “Kama ndivyo hivyo aliendeleakusema, "ingekuwa hivyo, wale wanaoshikilia kwamba mchakato wa sinodi, mara ulipofika kwenye hatua ya utambuzi wa maaskofu, ulizima kila tukio la kinabii la Watu wa Mungu lingekuwa sahihi!”

Mchakato wa mviringo

Kiukweli makubaliano ya ulimwengu wote yanatokana na kusikiliza kila mtu. Katika kila hatua tumerudisha kwa Makanisa matunda ya kusikiliza. Kwa hivyo ilikuwa mchakato wa mzunguko kwa sababu Sinodi ni mchakato unaohusisha Kanisa zima na kila mtu ndani ya Kanisa, kila mmoja kadiri ya kazi yake, karama yake na huduma yake,” Kardinali Grech alisema. Kazi nzito inatungojea ...” Hitimisho halitakuwa taarifa ya kinadharia,  ya Hati ya mwisho, lakini ni maisha halisi ya Kanisa.”

Kikao cha pili, sio kurudia cha kwanza

Ilikuwa ni hasa juu ya maelezo ya Hati ya kitendea kazi, iliyotolewa tarehe 9 Julai 2024, na juu ya malengo ya kikao hicho cha pili, kwamba Kadinali Jean-Claude Hollerich, Msemaji  Mkuu, wa Sinodi ya Maaskofu, alizungumza katika ripoti ndefu ya wazi kwa matumaini kwamba,  wale wote waliohudhuria wanaweza kuhisi kuwa karibu. “Ni vizuri kukutana tena, ni ishara kwamba ujuzi na urafiki umekua kati yetu, na kwamba mwaka uliopita haujafuta.” Ndivyo alivyoanza hotuba yake katika Kikao cha pili, ambacho Kardinali wa Luxembourg alifafanua mara moja, kuwa “sio kurudia au hata mwendelezo rahisi wa kwanza.” “Ikiwa lengo la Mkutano wa  2023 ulikuwa kufahamiana na kupata ujuzi bora zaidi wa Makanisa ambayo wengine wanatoka, hata hivyo, katika awamu hii ya pili, washiriki wa Sinodi wanaitwa kuzingatia kwa mitazo yao juu ya njia zinazowezekana za ukuaji ambazo zitaalika Makanisa kutembea pamoja.” Kwa njia hiyo “Lengo ni kwamba utajiri huo usibaki umefungwa kwenye sanduku la hazina, bali uingie katika mzunguko wa ubadilishanaji wa zawadi zinazorutubisha ushirika wa Kanisa kwa ujumla”.

Katika Instrumentum laboris kuchuja safari ya miaka mitatu

Instrumentum laboris, yaani. Kitendeakazi kwa maana hiyo kinachuja(distillate),(kwa wale wanaojua tofauti kati ya divai na Konyagi... alitania Kardinali) ya kile ambacho Kanisa limejifunza katika miaka hii mitatu. Ni hati tofauti ikilinganishwa na ya kwanza kwa sababu kazi yetu ni tofauti: katika kazi iliyopita kulikuwa na maswali mengi, karibu 300; katika kitendea Kazi cha pili, hata hivyo, alama za maswali zinaonekana mara kumi tu na (ilikuwa ni shida kuhesabu,” alisema Kardinali Hollerich), kwa usahihi kusisitiza ukweli kwamba sasa hakuna maswali tena lakini kuna vitendo vya kwenda katika mwelekeo mmoja.” Kardinali Hollerich kwa hiyo alifafanua kuwa Kitendela Kazi “sio rasimu ya Hati ya mwisho ambayo inahitaji marekebisho tu, lakini ni mkusanyiko wa matokeo ya mchakato ambao ni kazi yetu kutambua.”

Mazungumzo na kufanya kazi na Vikundi vya Utafiti

Hatimaye, Kardinali wa Luxembourg alionesha mbinu za kazi na tofauti zikilinganishwa na kikao kilichopita, akianza na mazungumzo na Vikundi kumi vya Utafiti vilivyoanzishwa na Papa mwezi Februari 2024 kuchunguza na utafiti wa mada maalum pamoja na nyingine tatu kuhusu masuala maalum. “Tunao wasindikizaji wanaosafiri ambao ni waingiliaji kati yetu," alisema. Katika sehemu ya mwisho ya kutaniko la kwanza, mwakilishi wa kila Kikundi alisasisha programu ya kazi ya Kikundi chao katika siku na miezi iliyofuta, akieleza tafakari na mada. Mazungumzo ya mara kwa mara yanatarajiwa kati ya washiriki wa Sinodi na washiriki wa Vikundi: “Kwa mtindo wa sinodi kwa hivyo sitakuwa peke yangu nitazungumza wakati wa Ripoti ya Mwandishi Mkuu, ni nzuri kwako! Kardinali Hollerich alisema akimkaribisha mwingine.

Mwandishi mkuu wa Sinodi aliorodhesha mada zinazoshughulikiwa na Vikundi: safari ya kiekumene; mahusiano kati ya Makanisa Katoliki ya Mashariki na Kanisa la Kilatini; kilio cha maskini; huduma ya maaskofu, mapadre na mashemasi na uhusiano na Watu wa Mungu; mafunzo katika sinodi; mazingira ya kidijitali; mahusiano kati ya Makanisa mahalia, kazi ya kuanzishwa kwa Sinodi; huduma ya umoja ambayo ni ya Askofu wa Roma; masuala ya kutatanisha ya mafundisho, kichungaji na maadili katika Kanisa na uhusiano kati ya karama na huduma.

Wanawake

Katika suala hili la mwisho, Kardinali Victor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa alitoa ufahamu huku akifafanua kwamba, miongoni mwa mambo yatakayoshughulikiwa ni pamoja na nafasi ya wanawake katika Kanisa, michakato ya maamuzi inayohusishwa na uongozi wa jumuiya na ushemasi wa kike, kwa kuzingatia kwamba “tunajua nafasi ya umma ya Papa ambaye hafikirii suala hilo kukomaa.”

Majanga ya Makanisa ya Mashariki

Mbele yake, Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki, alileta mbele ya mtazamo wa  wale waliokuwepo kuhusu hali ya kushangaza ya siku hizi katika nchi hizo: mabomu, mizinga ambayo kila mahali na kwa kiasi kikubwa huharibu sio watu tu, bali pia matumaini na kugonga kategoria ndogo na dhaifu kama vile Makanisa ya Kikatoliki ya Mashariki katika maeneo ya vita. Kwa mjibu wake alishutumu kuwa: “Wako katika hatari ya kutoweka. Hasara yao haiwezi kurekebishwa kwa Kanisa.” Kwa hiyo, Kundi la Gugerotti linachukua jukumu la kuwaomba Walatini, ambao wana nguvu zaidi na waliojipanga zaidi, kuwasaidia ndugu zetu hawa kuishi  njia bora zaidi hasa baada ya uhamiaji mkubwa kutoka nchi zao za asili. Katika baadhi ya Makanisa, kwa hakika, “asilimia kubwa ya waamini wako ughaibuni na si katika nchi zao zilizoharibiwa na vita,” alisema Kardinali  Gugerroti.

Mazingira ya kidijitali

Katika hotuba nyingine, mtaalamu wa mambo ya kidijitali,  Kim Daniels alisimulia kazi ya kikundi inayoakisi uwepo katika mazingira ya kidijitali. Yeye alisema kuwa “digitali ni ukurasa mpya wa utume” na alizungumza juu ya “uwezekano wa kusaidia kwa wale wanaohitaji na kutangaza Neno la Mungu katika ulimwengu wa mtandaoni. Daniels pia alisisitiza umuhimu wa kuunganisha tena mkutano wa kidijitali na mkutano wa ana kwa ana, na kuleta ushuhuda wa Yesu Kristo katika kila nafasi ya mikutano.”

Swali la mitala

Katika Mkutano wa kwanza pia ulingiliwa na kuoneshwa kwa baadhi ya maelezo kwa njia ya video, ambapo miongoni alikuwa ni Askofu Mkuu wa  Jimbo Kuu la Kinshasa,  Congo (DRC), Kardinali Fridolin Ambongo, kuhusu mada ngumu ya mitala katika nchi nyingi za Kiafrika ambapo alisema ni “Changamoto ya kweli ya uchungaji.” “Kuna watu wameikubali imani ya Kikristo lakini katika mazingira ya kuoa wake wengi, lakini pia wapo waliobatizwa ambao wanaishi kwa mitala baada ya kujiunga  kwao ukatoliki,”alisema Ambongo. Kwa njia hiyo: "Ni aina gani ya huduma ya kichungaji inafaa zaidi kwa kuwasindikiza na watu katika mahusiano ya mitala?” Kuhusiana na hilo, Kardinali Ambongo ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar (SECAM) alisema imeandaa mpango wa awamu nne ambao unalenga kuzama katika aina za jambo hili, motisha, mafundisho na huduma ya kichungaji kwa watu walio na wake zaidi ya mmoja.

03 October 2024, 15:39