2024.10.14:Sr Raffaella Petrini,Katibu Mkuu wa Masuala ya Jumla ya Mji wa Vatican katika  Kongamano la Kiwango cha Kimataifa 2024.10.14:Sr Raffaella Petrini,Katibu Mkuu wa Masuala ya Jumla ya Mji wa Vatican katika Kongamano la Kiwango cha Kimataifa 

Sr Petrini:Akili mnemba zana katika huduma ya binadamu!

Katibu wa Mambo ya Jumla ya Jiji la Vatican,akizungumza katika Kongamano la Kimataifa la Viwango vya juu huko New Delhi nchini India,alionesha matarajio ya kuanzishwa kwa sera za pamoja zinazoongoza maendeleo ya teknolojia mpya hasa Mapinduzi ya kweli ya utambuzi wa viwanda."Na aliongozana na Monsi.Ruiz kutoka Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Na Edoardo Giribaldi na Angella Twezaula – Vatican

Sista Raffaella Petrini, Katibu mkuu wa Masuala ya Jumla ya Mji wa Vatican alizungumza kwenye Kongamano la Kimataifa (GSS-24),mjini New Delhi, nchini India, katika mkutano wa ngazi ya juu ulioakisi mada ya “uongozi na wajibu wa AI katika kubuni mustakabali wa uvumbuzi.”Katika hotuba hiyo alisisitiza kwamba: "Ingawa inawakilisha matokeo muhimu ya maendeleo ya kiteknolojia, Akili Mnemba (AI) unasalia kuwa chombo katika huduma ya wanadamu." Sista Petrini katika afla hiyo aliongoza ujumbe wa Vatican akiwa na wajumbe kutoka Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakiongozwa na Monsinyo Lucio Adrián Ruiz, Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.

Maendeleo ya kiteknolojia na maendeleo ya binadamu

Katibu wa Masuala ya Mji wa Vatican katika hotuba yake alianza kwa kuunganisha dhana ya maendeleo ya kiteknolojia na maendeleo ya binadamu, huku akibainisha jinsi, gani kwa upande mmoja, zana za ubunifu zaidi huruhusu kupunguza hatari; kuboresha kazi zetu na hali zetu za maisha na jinsi gani kwa upande mwingine jamii inaitwa kuzitumia kuwajibika kimaadili. Hii inakuwa kweli kwa teknolojia “rahisi lakini lazima zaidi kuhusiana na matumizi ya  Akili Mnemba (AI), yenye uwezo wa kuwakilisha, kuchukua dhana iliyooneshwa na Papa Francisko wakati wa ushiriki wake katika kikao cha G7 juu ya mada, "utambuzi wa kweli na  mapinduzi ya viwanda."

Maendeleo ya kimaadili ya AI

Vigezo vilivyochaguliwa kufundisha teknolojia hizi ni, katika maono ya Sista Raffaella Petrini,  ni “mambo muhimu katika kuamua kama haki za kimsingi za binadamu zinaheshimiwa, ikiwa mifumo hii ni ya kutegemewa na ya kudumu na ikiwa ni kweli endelevu." Katika muktadha huo, "ushirikiano wa kimataifa, unaozingatia mazungumzo ya uaminifu, ni muhimu katika kuanzisha sera za pamoja zinazoweza kuongoza maendeleo ya miundo hii kulingana na viwango vya usalama na kanuni za maadili," alisisitiza. Aidha alisema “Kazi au  changamoto, hata hivyo ni muhimu kutoa tafakari za pamoja na masuluhisho ya kisiasa yenye lengo la kutafuta lililo jema na sahihi.”

Maadili ya algorithm ya teknolojia mpya

Wakati wa hotuba yake, katibu mkuu wa Masuala ya Jumla ya Mji wa Vatican hata hivyo alimnukuu tena Papa Francisko, ambaye katika ujumbe wake kwa Siku ya Amani ya Dunia kwa  2024 alibainisha  "haja ya mazungumzo ya taaluma mbalimbali yenye lengo la maendeleo ya maadili ya algoriti  ya maadili, ambayo maadili huongoza njia za teknolojia mpya." Mtawa huyo alikumbusha zaidi kwamba Teknolojia, ilizaliwa na kusudi, yaani, ile ya kubaki chombo cha kujenga mema ya kila mwanadamu na kesho iliyo bora kwa wote. Msukumo madhubuti katika utekelezaji wa matakwa haya inaonesha leo hii aina halisi ya mshikamano ambayo inaruhusu serikali kuanzisha vipaumbele na mashirika kuchukua jukumu kwa waingiliaji wao wote."

Pendekezo kwa shirika la kimataifa

Sr. Petrini alifafanua, kama alivyosema Papa Francisko kwamba "Ushirikiano kati ya mataifa, ni sera yenye afya ambayo, kwa kuhusisha sekta na ujuzi mbalimbali, unaweza kusimamia maendeleo ya teknolojia na kuunda mazingira ya kutumia vizuri teknolojia inawezekana na yenye matunda, pamoja na  Akili Mnemba (AI)." Katika majibu maswali  kando ya ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Masuala ya Jumla ya Mji wa Vatican alithibitisha pendekezo lililotolewa na Vatican la kuundwa kwa shirika la kimataifa linalohusiana na Akili Mnemba( AI), lenye lengo la "kutayarisha mfumo wa udhibiti na uendeshaji" juu ya matumizi yake ya "amani," alihitimisha Sr Petrini.

15 October 2024, 11:23