Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa sasa wazo la kuwa na Mashemasi Wanawake ndani ya Kanisa Katoliki, bado ni changa sana na wala hakuna uwezekano wa kuwapatia wanawake Daraja Takatifu ya Ushemasi kwa sasa. Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa sasa wazo la kuwa na Mashemasi Wanawake ndani ya Kanisa Katoliki, bado ni changa sana na wala hakuna uwezekano wa kuwapatia wanawake Daraja Takatifu ya Ushemasi kwa sasa.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Tamko Kuhusu Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kwa sasa wazo la kuwa na Mashemasi Wanawake ndani ya Kanisa Katoliki, bado ni changa sana na wala hakuna uwezekano wa kuwapatia wanawake Daraja Takatifu ya Ushemasi kwa sasa. Tume ya Kuchunguza Kuhusu Dhamana na Wajibu wa Mashemasi Wanawake ndani ya Kanisa Katoliki imefikia uamuzi huu na utachapishwa wakati muafaka utakapo wadia. Lakini dhamana na utume wa wanawake ni muhimu sana ndani ya Kanisa.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mama Kanisa anasema, utume na dhamana ya Mashemasi katika maisha ya Kanisa ni kwamba, wao ni wasaidizi wa karibu wa Maaskofu mahalia. Mashemasi ni wahudumu wa Neno la Mungu, Mafumbo ya Kanisa kadiri ya daraja lao na hasa zaidi wadau wakuu katika utekelezaji wa matendo ya huruma kwa maskini, na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii. Maskini ni watu ambao Kristo Yesu aliwapatia kipaumbele cha kwanza katika maisha na utume wake. Huu ni wito wa kujitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya Mungu, Kristo Yesu na Kanisa lake. Wito huu ni kwa ajili ya mafao ya Kanisa na wala si fursa ya mtu kujitafuta mwenyewe. Mashemasi wawe na huruma na wenye bidii wakienenda katika ukweli wa Bwana Yesu Kristo aliyejifanya mtumishi wa watu! LG 29.  Mashemasi wanawekwa wakfu kwa ajili ya huduma ya upendo kwa watu wa Mungu; ni mashuhuda wa utakatifu wa watu wa Mungu unaopata chimbuko lake katika maisha ya Sala za Kanisa; tafakari ya Neno Mungu na nidhamu katika maisha ya utii, useja na ufukara. Kuna aina mbili za Mashemasi. Mosi ni Mashemasi wa mpito kuelekea Daraja Takatifu ya Upadre na pili kuna Mashemasi wa kudumu. Baba Mtakatifu Francisko kunako mwaka 2016 alikutana na kuzungumza na Mama Wakuu wa Mashirika ya Kitawa Kimataifa wapatao 900 waliokuwa wanahudhuria mkutano wao mkuu wa Kimataifa uliokuwa unafanyikia mjini Roma.

Tamko Kuhusu Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki
Tamko Kuhusu Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki

Masista hao walijadili pamoja na Baba Mtakatifu mambo mbalimbali katika maisha na utume wa Kanisa mintarafu nafasi ya wanawake. Kuhusu uwepo wa Mashemasi wanawake katika Kanisa la Mwanzo, Baba Mtakatifu alisema, uelewa wa Kanisa haukuwa bayana sana na hivyo alikubaliana na Masista hawa kuunda Tume ya kuchunguza kuhusu dhamana na wajibu wa Mashemasi wanawake katika maisha na utume wa Kanisa la Mwanzo. Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika maadhimisho ya Sinodi XVI ya Maaskofu, Jumatatu tarehe 21 Oktoba 2024, amesemsa Baba Mtakatifu Francisko, anasema kwamba, kwa sasa wazo la kuwa na Mashemasi Wanawake ndani ya Kanisa Katoliki, bado ni changa sana na wala hakuna uwezekano wa kuwapatia wanawake Daraja Takatifu ya Ushemasi kwa sasa. Tume ya Kuchunguza Kuhusu Dhamana na Wajibu wa Mashemasi Wanawake imefikia uamuzi kwamba, huu si wakati muafaka na kwamba, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa litachapisha muhtasari huu kwa wakati muafaka. Baba Mtakatifu anaitaka Tume hii chini ya uongozi wa Kardinali Giuseppe Petrocchi kuendelea na kazi yake.

Dhana ya Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki ni changa sana
Dhana ya Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki ni changa sana

Hata hivyo, Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kukazia umuhimu wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa hata kabla ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu na ndiyo maana amelikabidhi Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kuangalia tena dhamana na nafasi ya wanawake katika maisha na utume wa Kanisa, bila kujiingiza sana katika Daraja Takatifu. Uhaba wa miito katika Kanisa ni changamoto kubwa, kumbe, kutoa Daraja Takatifu ya Ushemasi hakuwezi kufua dafu na kwamba, kuna idadi kubwa sana ya wanawake, ambao bado hawajatumika kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa, hasa katika Katekesi. Hata pale Baraza la Kipapa la Ibada, Nidhamu na Sakramenti na Sakramenti za Kanisa lilipoomba ushauri kutoka kwa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki, sehemu mbalimbali za dunia, Mabaraza mengi ya Maaskofu bado yalisita kuwahusisha wanawake katika huduma ya Katekesi.

Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki wazo bado ni changa sana
Ushemasi wa Wanawake Ndani ya Kanisa Katoliki wazo bado ni changa sana

Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa Kitume mara baada ya Sinodi unaojulikana kama “Querida Amazonia” yaani “Amazonia Mpendwa” anaelezea maana ya wosia huu kuwa ni muhtasari ya mambo mazito yaliyojadiliwa katika Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Ukanda wa Amazonia unaoziunganisha nchi tisa. Lengo ni kusimama kidete kulinda na kudumisha utu, heshima na haki msingi za binadamu. Kulinda na kuendeleza utunzaji bora wa mazingira bora nyumba ya wote. Ni ndoto yake kutaka kuona kwamba, Ukanda wa Amazonia unalinda uoto wa asili sanjari na kujikita katika ukarimu wa watoto wa Ukanda wa Amazonia ili kulipyaisha Kanisa na kulipatia watoto wapya. Baba Mtakatifu anagusia kuhusu ndoto za kijamii zinazokita ujumbe wake katika msamaha na ujenzi wa jumuiya ya watu wa Mungu Ukanda wa Amazonia. Ameelezea pia kuhusu umuhimu wa Makatekista wanao wahudumia watu wa Mungu, bila ya uwepo wa Mapadre. Hata huku ni idadi ndogo sana ya wanawake waliojitokeza kwa ajili ya huduma ya Ukatekista na kwamba, kuna baadhi ya Mapadre hawaoni sababu ya kuwatambulisha wanawake hawa kwa Maaskofu mahalia, ili waweze kupewa Daraja katika huduma hii.

Mchango wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa ni mkubwa.
Mchango wa wanawake katika maisha na utume wa Kanisa ni mkubwa.

Kumbe, Daraja ya Ushemasi si sera wala mbinu mkakati muafaka wa kuwaendeleza na kuwaenzi wanawake katika maisha na utume wa Kanisa. Kardinali Víctor Manuel Fernández, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa amewataka Mababa wa Sinodi kama mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu, kupeleka kwenye Baraza lake shuhuda mbalimbali za wanawake ambao wanaoongoza Jumuiya za waamini kwenye Makanisa mahalia, ili kusaidia kupata mawazo yatakayoliwezesha Kanisa kuwashirikisha kikamilifu zaidi wanawake katika maisha na utume wa Kanisa kama viongozi. Ikumbukwe kwamba, hakuna kizuizi chochote kinachokwamisha wanawake kuchukua dhamana na wajibu mpana zaidi katika maisha na utume wa Kanisa.

Mashemasi Wanawake
22 October 2024, 16:18