Tafuta

Nyanyaso juu ya watoto na ulinzi wao unahitajika. Nyanyaso juu ya watoto na ulinzi wao unahitajika.  (©JenkoAtaman - stock.adobe.com)

Ulinzi wa Watoto:ripoti ya kila mwaka ya majibu ya nyanyaso iko njiani!

Chapisho hilo lililotangazwa wakati wa kikao cha wajumbe wote wa Tume ya Kipapa kilichofanyika kuanzia 7-11 Oktoba 2024.Lengo la hati hiyo lililombwa na Papa 2022 ni kutoa tathmini ya sera na taratibu zilizopitishwa ndani ya Kanisa na kutoa mapendekezo ya uboreshaji endelevu:Uimarishaji wa mipango ya ndani na uthibitishaji na urekebishaji wa sera ndani ya Mfumo wa Miongozo ya Ulimwengu pia ulijadiliwa.

Vatican News

Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto wadogo na watu wazima walio katika mazingira magumu ilitayarisha uchapishaji wa Ripoti ya Majaribio ya Mwaka ya Sera na Taratibu za Ulinzi katika Kanisa Katoliki. Ripoti hiyo ilijadiliwa wakati wa mkutano wa majadala wa majira ya vuli uliofanyika Roma kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba 2024, ambao vikao vyake vya kazi vilijitolea pia kuimarisha uwezo wa ulinzi wa ndani kupitia Mpango wa Kumbukumbu na uthibitishaji na marekebisho ya sera ndani ya Mfumo wa Miongozo ya Ulimwenguni.

Madhumuni ya Ripoti ya Mwaka

Katika taarifa yake, Tume ya Kipapa inaeleza kwamba, lengo la Ripoti ya Mwaka, iliyoombwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2022, ni kutoa tathmini ya asili na ufanisi wa sera na taratibu za ulinzi ndani ya Kanisa na kutoa mapendekezo ya uboreshaji endelevu. Wakati wa kikao hicho, Instrumentum Laboris pia ilichunguzwa, yaani, mpango wa ripoti inayofuata inayohusu mwaka 2024/2025, ambayo kwa matumaini itatumika kama utaratibu wa mabadiliko endelevu na yanayoweza kuthibitishwa katika mtazamo wa Kanisa Katoliki kwa huduma ya ulinzi.

Ushirikiano na Makanisa mahalia

Kuhusu uundaji wa Mfumo wa Miongozo ya Kiulimwengu, maoni yaliyopokelewa kutoka katika Makanisa mahalia hadi sasa na awamu ya majaribio inayoendelea kwa ushirikiano na Makanisa nchini Costa Rica, Zimbabwe, Poland na Togo yalichunguzwa. Hatua inayofuata itakuwa kuunganisha matokeo ya awamu hii katika mfumo wa ulinzi ulioimarishwa, ambao unasalia kuwa lengo kuu la kimkakati la muda mrefu. Mkutano huo pia ulitathmini kile kilichojitokeza kutoka katika mikutano hiyo na mikutano 13 ya maaskofu ambayo ilifanyika katika miezi sita iliyopita, wakati wa ziara ya Kitume ya ad Limina jijini Roma. Mikutano hii inawakilisha fursa ya kujifunza kuhusu taratibu za ulinzi wa ndani na kutambua Makanisa ya mahali ambayo hayana rasilimali zinazohitajika kutoa msaada wa kutosha. Kwa kuzingatia haya yote, kusanyiko lilitathmini mpango wa kuimarisha uwezo wa ulinzi, Mpango wa Kumbukumbu, na upatanishi wake na mahitaji yaliyooneshwa katika Waraka wa Kitume "Vos estis lux mundi." Mpango huu, unaolenga kusaidia Makanisa mahalia kuunda miundo ya kupokea na kusimamia malalamiko kwa njia ya uwazi na uwajibikaji na kutoa huduma za usaidizi wa kitaalamu kwa wale ambao wameteswa na dhuluma, kwa sasa unafanya kazi katika mabaraza kadhaa ya kitaifa ya maaskofu na mabaraza ya kitawa huko Amerika Kusini, Afrika na Asia. Mpango huo pia utaanza hivi karibuni na Makanisa mengine 12 ya ndani.

Kufanya kazi na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Hatimaye, Wajumbe wa Tume walifahamishwa kuhusu mikutano mbalimbali ya kitaasisi iliyofanyika katika kipindi cha miezi ya kiangazi katika Kanisa Kuu la Kirumi ikiwa ni pamoja na ile ya Baraza la Kipapa la Makleri, Baraza la Kipapa la Maaskofu, Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha na Baraza la Kipapa la Maisha ya Wakfu na Vyama vya Maisha ya Kitume. Mkutano huo, uliohudhuriwa na wajumbe 30 wa wataalamu na wafanyakazi kutoka mabara matano, ulikuwa mkutano wa kwanza chini ya uongozi wa Askofu Luis Manuel Ali Herrera, katibu wa Tume, na Teresa Kettelkamp, ​​katibu msaidizi, aliyeteuliwa na Papa Francisko msimu wa masika uliopita. Askofu mkuu John Kennedy, katibu wa Kitengo cha Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, naye alishiriki katika kazi hiyo, akisindikizwa na Padre Robert Geisinger, mtetezi wa haki, na Padre Brian Taylor, ofisa wa Baraza hilo, ambaye alizungumza  kuhusu taratibu za sasa za kushughulikia nyanyaso za kijinsia katika Kanisa na juu ya maendeleo ya miongozo ya ulinzi.

'Ulinzi lazima uwepo daima'

Ushiriki huo uliwakilisha ishara ya umoja katika juhudi za kuzuia na kutoa fursa ya kuchunguza ushirikiano unaoendelea kati ya Mabaraza ya Kipapa na  Tume. "Tumehakikisha kwamba ulinzi ni uwepo na utakuwepo daima katika maisha ya Kanisa," Kardinali O'Malley aliawaeleza Mkutano huo na kwamba: “Wakati malengo yetu yote bado hayajafikiwa, tutaendelea kusukuma mageuzi pale tunapobaini mapungufu ya kimfumo. Juhudi zetu zimefanya mabadiliko makubwa - alisema kardinali - na labda, muhimu zaidi, ni ishara ya matumaini na mshikamano kwa wale ambao wameteseka vibaya na kwa wapendwa wao."

Ripoti ya Tume ya Baraza la Kipapa la Ulinzi wa Watoto
21 October 2024, 11:40