Tafuta

Burkina Faso ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vatican tarehe 14 Juni 1973. Burkina Faso ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vatican tarehe 14 Juni 1973.  

Vatican na Burkina Faso Watia Saini Itifaki ya Pili ya Nyongeza 2024

Itifaki ya Pili ya Nyongeza, ambayo ina Dibaji, vifungu saba na kiambatisho, inasimamia zaidi utaratibu wa kutoa utambulisho kwa viongozi wa Kanisa wanaotambuliwa kisheria na Serikali ya Burkina Faso. Lengo ni kuwawezesha viongozi wa Kanisa kuteleza vyema dhamana na wajibu wao wa uinjilishaji wa kina na hivyo Kanisa kuendelea kujikita katika kukuza na kudumisha ustawi na mafao ya wengi, kama yalivyobainishwa katika Makubaliano yal 12 Julai 2019.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Burkina Faso ilianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vatican tarehe 14 Juni 1973. Itifaki ya Pili ya Nyongeza ya Makubaliano kati ya Vatican na Burkina Faso kuhusu Hadhi ya Kisheria ya Kanisa Katoliki nchini Burkina Faso ilitiwa saini mjini Ouagadougou, tarehe 11 Oktoba 2024, katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Burkina Faso. Askofu mkuu Michael F. Crotty, Balozi wa Vatican nchini Burkina Faso ameongoza jopo la wawakilishi kutoka Vatican wakati ambapo Burkina Faso imewakilishwa na Mheshimiwa Karamoko Jean Marie Traore, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Raia wa Burkina Faso walioko nje ya nchi.

Vatican na Burkina Faso Wametia Saini Itifaki ya Pili ya Nyongeza
Vatican na Burkina Faso Wametia Saini Itifaki ya Pili ya Nyongeza

Itifaki ya Pili ya Nyongeza, ambayo ina Dibaji, vifungu saba na kiambatisho, inasimamia zaidi utaratibu wa kutoa utambulisho kwa viongozi wa Kanisa wanaotambuliwa kisheria na Serikali ya Burkina Faso. Lengo ni kuwawezesha viongozi wa Kanisa kuteleza vyema dhamana na wajibu wao wa uinjilishaji wa kina na hivyo Kanisa kuendelea kujikita katika kukuza na kudumisha ustawi na mafao ya wengi, kama yalivyobainishwa katika Makubaliano yaliyotiwa saini tarehe 12 Julai 2019 na kuanza kutumika tarehe 7 Septemba 2020. Itifaki ya Pili ya Ziada imeanza kutumika tarehe 11 Oktoba 2024.

Burkina Faso
12 October 2024, 15:40