Vatican katika UN:Umuhimu wa chakula,kazi na familia dhidi ya umasikni!
Vatican News
Askofu mkuu Gabriele Caccia, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani katika taarifa yake aliyoitoa tarehe 18 Oktoba 2024 kwenye Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa alisisitza kuwa "Umaskini unaendelea na kudharau hadhi ya binadamu,huku ukizidisha ukosefu wa usawa na kuwanyima mamilioni ya watu fursa ya kustawi."
Mtazamo juu ya wanawake na watoto
Katika hali halisi ambapo asilimia tisa ya watu duniani wanaishi katika hali ya umaskini uliokithiri, Askofu Mkuu Caccia alisema ni wazi kwamba si tu ukosefu wa rasilimali za kifedha bali ni janga ambalo, , huzuia kufurahia kikamilifu haki za binadamu na kuwanyima watu fursa na njia za kushiriki kikamilifu katika jamii. Kwa hiyo inaathiri kila nyanja ya maisha ya mtu, kuanzia upatikanaji wa elimu na huduma ya afya hadi nafasi za kazi zenye heshima na ina athari zisizo sawa kwa wanawake na watoto hasa. Kwa hivyo unahitajika uharaka wa juhudi za pamoja zinazozingatia kwanza kabisa mahitaji ya lishe ya wanawake, hasa wajawazito au wanaonyonyesha, na kwa maendeleo na ukuaji wa watoto wadogo.
Mshikamano na hatua ya pamoja
Kwa upande mwingine, kutokuwa na uhakika wa ulimwengu katika miaka ya hivi karibuni kumefikia viwango visivyo na kifani Askofu Mkuu Caccia alisisitiza katika taarifa nyingine. Tahadhari ilielekezwa katika nchi za visiwa vidogo zinazoendelea, nchi zenye maendeleo duni na nchi zinazoendelea zisizo na bandari. Ni wao, alibainisha, ambao wanakabiliwa na athari zisizo sawa za mabadiliko ya hali ya hewa na tete ya kiuchumi, licha ya kuchangia kidogo kwa matatizo haya. Ili kukuza ustahimilivu wa kudumu, aliendelea, “ni muhimu kukabiliana na changamoto hizi ana kwa ana, kupitia hatua za pamoja na mshikamano, kuhakikisha kwamba ukweli huu unapokea rasilimali muhimu, teknolojia na usaidizi.
Kuuimarisha miundo ya kijamii kwa usalama na utulivu
Ni muhimu vile vile kuimarisha miundo ya kijamii ambayo hutoa usalama na utulivu. Kuanzia familia, ambao ni msingi wa jamii, kipaumbele cha ulinzi dhidi ya mgogoro wowote." Ajira, pia ilisisitizwa, ambayo inasalia kuwa "njia ya kimsingi ambayo watu wanaweza kujiondoa kutoka kwa umaskini". Kazi yenye heshima pamoja na mishahara ya haki, katika hali dhabiti na kwa usaidizi wa mifumo ya ulinzi wa kijamii" huwapa watu binafsi na familia usalama wanaohitaji ili kustawi na kuwezesha ukuaji wa uchumi endelevu na shirikishi.