Askofu Mkuu Gallagher. Askofu Mkuu Gallagher. 

Ask.Mkuu Gallagher yuko Cameroon kwa maadhimisho ya miaka 10 ya Mkataba wa Mfumo

Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa kuanzia tarehe 14 hadi 18 Novemba 2024 atakuwa Yaoundé nchini Cameroon.Katika ziara hiyo atafanya Mikutano na rais na viongozi wa kisiasa na maaskofu wa ndani.Katika Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika ya Kati, Askofu mkuu atatunukiwa udaktari wa heshima.

Vatican News

Safari ya Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa  Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, nchini Cameroon wakati wa kuadhimisha miaka kumi tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Mfumo na nchi hiyo ya Kiafrika. Kwa mujibu wa programu hiyo, iliyotolewa kupitia chapisho la kwenye X kwenye akaunti ya Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, Askofu Mkuu Gallagher atakutana  na Waziri wa Mambo ya Nje, Lejeune Mbella Mbella, tarehe 15 Novemba; na hiyo itafuatiwa na ziara ya heshima kwa Waziri Mkuu, Joseph Dion Ngute. Siku hiyo hiyo Askofu mkuu atakutana na maaskofu wa Cameroon. 

Mkutano na viongozi wa nchi na pia chuo kikuu katoliki cha Cameroon

Jumamosi tarehe 16 Novemba 2024, Askofu Mkuu  Gallagher ataadhimisha Liturujia ya Ekaristi takatifu katika Kanisa dogo la Marie Reine des Apötres de Mvolye, katika mji mkuu Yaoundé. Siku ya Jumatatu tarehe 18 Novemba 2024,  Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa atapokelewa kwa Mkutano na Rais wa Jamhuri ya Cameroon, Bwana  Paul Biya. Tendo la mwisho ni mkutano katika Chuo Kikuu katoliki cha Afrika ya Kati Yaoundé, ambapo katika hafla hiyo, Askofu Mkuu Gallagher atatunukiwa udaktari wa heshima.

14 November 2024, 18:45