Jubilei:Kitambulisho cha huduma kwa mahujaji kinapatikana kwenye mtandao
Vatican News
Takriban mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa Jubilei ya 2025 inayoongozwa na kauli mbiu: "Mahujaji wa Matumaini", tangu Jumanne tarehe 26 Novemba 2024, Kitambulisho kinapatika kupitia mtandao. Hiki ni kitambulisho cha Huduma, ambacho kinashughulikiwa na kitengo maalum cha kuandaa Kitambulisho cha Mahujaji ambacho kitatoa punguzo na manufaa yote yatakayotolewa kwa wale watakaoshiriki katika sherehe na matukio mbalimbali ya Jubilei. Huu ni mpango mpya wa kuhimiza mapokezi kwa mahujaji wengi wanaotarajiwa kufika jijini Roma kwa Mwaka Mtakatifu.
Kitambulisho cha huduma kurahisha utaratibu
Kitambulisho cha Huduma ni cha bure ambacho kitatolewa kwa mfululizo, kwa ajili ya manufa katika maeneo tofauti kwa mfano: bima, ili kuishi uzoefu wa hija kwa usalama; makaribisho, kuhakikisha suluhishi zinazowezesha kukaa na kulala; chakula, pamoja na matoleo mengini kuhusu milo na mambo yanayohusu vyakula kwa ujumla; bidhaa rasmi, zinazotoa punguzo kwa bidhaa zilizounganishwa na Jubilei; usafiri na kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine, na viwango vilivyopunguzwa vya usafiri kwa ujumla na usafiri wa ndani; mawasiliano, kupitia huduma za kujitolea ili kuendelea kushikamana kila wakati.
Jiandikishe katika tovuti ya IUBILAEUM25
Katika tovuti rasmi ya Jubilei kama inavyotoa taarifa, ili kufikia Kitambulisho cha Mahujaji, kwa hiyo Kitambulisho cha Huduma ni muhimu kujiandikisha kwenye tovuti rasmi:( https://www.iubilaeum2025.va/en.html). Baada ya usajili kukamilika, kila mhujaji atapokea Msimbo wa QR uliobinafsishwa ambao utamruhusu kushiriki katika hafla za Jubilei na upatikanaji wa manufaa ya kipekee ya Utambulisho. Pia inawezekana kutumia Utambulisho wa Huduma kupitia Tovuti Rasmi ya Iubilaeum25 ambapo ni: muhimu kusasisha kila wakati programu hadi toleo jipya zaidi litakalopatikana.