Kard.Semeraro: Mwenyeheri Carmen del Niño Jesús ni mfano wa upendo kwa maskini
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mwanamke ambaye alitaka zaidi ya yote kusaidia wale walio na shida na kuwasaidia wale ambao walikuwa peke yao, hawakuwa na uwezo wa kujiondoa kutoka kwa umaskini na ndiyo sifa ya Mwenyeheri Carmen del Niño Jesús González Ramos, (wa mtoto Yesu), mwanzilishi wa Shirika la Wafransiskani wa tatu waitwao Mioyo ya Yesu na Maria. Ni katika ibada ya misa iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, Kardinali Marcello Semeraro, Dominika tarehe 10 Novemba 2024, kwenye Kanisa la Mama Yesu wa Malipizi huko Antequera, Hispania na kwa ajili ya kufunga Mwaka wa Jubilei ya miaka 125 tangu kifo cha mwenyeheri huyo.
Katika mahubiri yake, Kardinali alirejea juu ya maisha ya mtawa wa Kihispania na pia alisisitiza kujitolea kamili kwa ukuaji na uimarishaji wa familia mpya ya maisha ya wakfu iliyoundwa naye na unyenyekevu wake wa kina, alijifunza kutokana na kutafakari kwa (Niño Jesús) yaani mtoto Yesu ambaye alitaka kuhusishwa na jina lake la kitawa. Hata sifa za takwimu mbili za kike katika usomaji wa kiliturujia ilikuwa ya Dominika ambapo Somo la kwanza na Injili: kwanza mjane ambaye Eliya alimuomba chakula na kinywaji na yule anayetupa sarafu mbili kwenye hazina ya hekalu, akichangia kila kitu alichokuwa nacho kwa kukumbuka yule Maria wa Mlima Karmeli, wa Mtoto Yesu, Kardinali Semeraro alisema, “kinachowaunganisha ni umaskini na mapendo.”
“Kurasa za kibiblia zilizotolewa kwa wanawake hawa zinafundisha kwamba ili kutathmini mtu hatupaswi kujiruhusu kutekwa na mtazamo wao wa nje peke yake, sio kutoka nje ambapo tunahitaji kutathmini. Angalau Mungu hafikirii hivyo na pia kwamba hakuna mtu aliye maskini sana hata asiweze kutoa kitu,” Alisistiza Kardinali Semeraro akimnukuu kila mbacho Papa Francisko alikitaja wakati wa tafakari ya kabla ya sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 4 Novemba 2018 kwamba: “Walio na njaa hawahitaji sahani ya supu tu, lakini pia tabasamu, kusikilizwa na hata sala na mpango huu sio tu kwa uharaka wa ndugu maskini zaidi, lakini zaidi ya yote kuwa umakini na mahitaji yao ya udugu na ukaribu.” Kwa Wafransiskani hao wa Mioyo Mitakatifu ya Yesu na Maria, Kardinali Semeraro alionesha ushuhuda wa kielelezo wa mwanzilishi wao ambaye ana sifa ya upendo kwa maskini zaidi na wahitaji zaidi akiakisi kama Papa alivyosema, tarehe 1 Novemba 2015, kwamba “kuiga ishara za upendo na huruma za watakatifu ni sawa na kudumisha uwepo wao katika ulimwengu huu.” Pia ni kwa njia hii ambapo maadhimisho ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa Carmen del Niño Jesús González Ramos inapaswa kuadhimishwa.