2019.11.05 Kardinali  Ayuso Guixot na hakimu Muhammad Abd al-Salam wakiwa na Hati ya Udugu wa Kibidamu na Katibu Mkuu wa UN(2019) 2019.11.05 Kardinali Ayuso Guixot na hakimu Muhammad Abd al-Salam wakiwa na Hati ya Udugu wa Kibidamu na Katibu Mkuu wa UN(2019) 

Kardinali Angel Ayuso Guixot:mazungumzo na Uislamu 1952-2024

'Ayuso alikuwa maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu na katika ulimwengu mwingine wa kidini.Alitafuta urafiki na huruma kwa watu na kujaribu kusambaza upendo ambao Kanisa linakiri kwa wanadamu wote'.Ni maelezo kutoka kwa Rais wa Shirika la Kipapa kwa ajili ya Tathmini na Ukuzaji wa Ubora wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vya Kikanisa(AVEPRO),kufuatia na kifo cha Kardinali Ayuso Guixot,Mwenyiti wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Angel Ayuso Guixot aliaga Dunia tarehe 25 Novemba 2024 akiwa katika hospital ya Gemelli Roma. Kiongozi  huyo, Mkomboni wa Majadiliano ya Kidini, kifo chake kimegusa hisia za watu wengi na wasifu wa maisha yake ambapo kati ya wengi ni ushuhuda kutoka kwa Monsinyo Padre Armand Puig i Tàrrech, Rais wa Shirika la Kipapa kwa ajili ya Tathmini na Ukuzaji wa Ubora wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu vya Kikanisa(AVEPRO)ambapo anamkumbuka Kardinali huyo wa majadiliano. Tunachapisha ushuhuda kamili  wake.

Padre Armand Puig i Tàrrech

Kardinali Angel Ayuso Guixot ni Kardinali wa mazungumza na Uislamu 1952-2024. Katika umri wa miaka 72, ulimwengu huu uliondoka ili kuungana na Mungu mtu mwenye roho nzuri, mwenye imani ya kina, uaminifu usio na shaka kwa Kanisa, aliyeishi Injili kama nuru kwa wanadamu wote na kwa dini zote. Ayuso alikuwa maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu na katika ulimwengu mwingine wa kidini. Alitafuta urafiki na huruma kwa watu na kujaribu kusambaza upendo ambao Kanisa linakiri kwa wanadamu wote. Kwa maana hii, alikuwa katika ushirika wa karibu na Papa Francisko. Alishiriki katika hisia zake na alikuwa sura iliyothaminiwa na viongozi wengi wa kidini ulimwenguni. Ayuso alikuwa Kardinali mwenye busara na mkarimu, akitokea kwenye msingi wa wamisionari wa Kanisa. Alikuwa na uwezo maalum wa kusuka mahusiano na kupata “mwingine” kwa wengine, bila kumpunguza au kumhukumu. Alijua jinsi ya kuchanganya njia yake na wengine na kuzingatia mawazo na imani zao. Siri yake ilikuwa ni maombi.

Alizaliwa huko Seville, nchi ya Maria, alijiruhusu daima kubebwa na yale ambayo Mungu alikuwa akimwomba, yaani bila yeye kuomba chochote, ili tu kuweza kutimiza mapenzi yake. Kardinali alikuwa mtu mkali lakini wakati huo huo alikuwa mtu wa kupendeza. Akiwa mwana mmisionari wa Daniel Comboni, hakusita kufanya huduma ya kichungaji huko Cairo, iliyojumuisha vijana wahamiaji  wa Sudan. Katika mji mkuu wa Misri na Sudan, Kardinali  Ayuso alijifunza kuhusu umaskini na usahili wa watu wengi ambao walimfundisha kuishi Injili ya Yesu kwa nguvu. Kardinali wa baadaye daima aliishi akijifunza kutoka kwa wale ambao Mungu aliweka kando yake. Muda ulipowadia, alirejea Roma ambako alimaliza masomo yake hasa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana PISAI (Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo  ya Kiarabu na Kiislamu). Katika kipindi cha pili akiwa Roma, Ayuso Guixot, Kardinali rafiki wa Waislamu, akawa Rais wa PISAI na kutoka hapo alianza kushirikiana na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini, ambapo alikuwa Katibu na hatimaye Mwenyekiti. Alichaguliwa kuwa Kardinali na Papa Francisko mnamo 2019, alihamasisha uhusiano na Waislamu.

Kwake yeye tuna deni la utendaji madhubuti katika ufunguzi mkuu wa Papa Francisko kwa ulimwengu wa Kiislamu, ambao ulifanyika katika mawasiliano na imamu mkuu wa Al-Azhar, Al-Tayyeb, na katika uchapishaji wa Waraka wa “Fratelli tutti” yaani “Wote ni ndugu” na mfululizo wa mipango ya kuunga mkono amani na udugu kwa wote. Al-Tayyeb amesisitiza katika taarifa rasmi kwamba, Kardinali Miguel Ángel Ayuso Guixot amekuwa “mfano mashuhuri wa huduma kwa wanadamu ... ambaye amefanya juhudi kubwa katika kukuza uhusiano na Waislamu.” Maneno haya yawe ni muhtasari wa maisha ya Kardinali wa Kanisa ambaye ameweka nguvu zake zote, licha ya afya yake kuwa tete, katika huduma ya wanaume na wanawake wenye mapenzi mema.  Apumzike kwa amani.

Kardinali Ayuso alikuwa mtu wa majadiliano
27 November 2024, 08:57