Kuona Basilika ya Mtakatifu Petro:kwa Uzoefu ulioimarishwa na Akili Mnemba

Basilika ya Vatican inakuwa ya kidijitali na kufungua ulimwengu.Kwa ushirikiano na kiwanda cha Mtakatifu Pietro na Microsoft wamewasilisha mradi wa “Uzoefu Ulioimarishwa wa(AI)Pacha wa kweli wa kidijitali katika hekalu,moyo wa Ukristo,ambao pia unaweza kutembelewa na wale ambao hawawezi kufika Roma kwa ajili ya Jubilei 2025.

Vatican News

"Kuamua kwa ajili ya mtu wa leo, kwa msaada wa teknolojia ya dijitali, ufumaji wa historia, sanaa na hali ya kiroho ambayo hufanya Basilika kuwa ya kipekee ulimwenguni," ni maneno yaliyosemwa na Kardinali Mauro Gambetti, mkuu wa Basilika  ya Mtakatifu Petro na rais wa (Fabbrica di San Pietro,) yaani Kiwanda cha Mtakatifu Petro yaliyotolewa katika Chumba cha Waandishi wa Habari, Jumatatu tarehe 11 Novemba 2024, ikiwa ni matunda ya ushirikiano kati ya wasimamizi wa Basilika, moyo wa kiroho wa Ukristo na Microsoft, mojawapo ya makampuni muhimu zaidi ya IT duniani.

Kardinali Gambetti akieleza mfumo wa kidijitali wa kuona Basilika ya Mtakatifu Petro

Ni Picha laki nne za pacha wa kidijitali

Kwa muda wa majuma matatu, ndege zisizo na rubani, Camera na leza zilinasa zaidi ya picha 400,000 za mwonekano wa juu na ndani ya Basilika ambazo zilitumiwa kuunda kielelezo sahihi kabisa cha ufundi huo(3D) cha kanisa maarufu zaidi katika Ukristo. Maabara nzuri ya Akili Mnemba ya   Microsoft ilichakata data ya upigaji picha kutoka kwa timu ya Iconem ya Ufaransa, na kuboresha pacha wa kidijitali kwa usahihi wa milimita. ‘Algorithms’ za akili Menmba  zilijaza mapengo, ziliboresha maelezo na kuunda uundaji upya wa mtandaoni usio na mshono. Ni nakala ya Mtandao  ya Basilika iliyojengwa juu ya kaburi la Mtakatifu Petro, kazi bora ya sanaa ya ulimwengu na usanifu, pamoja na ishara ya Roma.

Msaada kwa mahujaji lakini pia kwa wasomi

Picha zinazozalishwa na akili Mnemba (IA) zitawaruhusu wale wanaounganisha kwenye tovuti shirikishi ya Basilica kutazama mambo ya ndani na nje kuanzia tarehe 1 Desemba 2024,  ijayo, wakifurahia uzoefu wa kina kupitia miundo ya kina ya (3D) na mpango wa elimu uliorekebishwa kwenye muundo wa “Minecraft.”  Ni Pacha ya kidijitali ambayo itasaidia wageni na mahujaji, lakini pia itaruhusu wasomi na wakarabati kuchunguza ulimwengu wa (polichrome) wa mnara huo kwa usahihi na undani usio na kifani.

Kardinali Gambetti pamoja na Brad Smith wakati wa uwakilishi wa Mpango mpya wa IA
Kardinali Gambetti pamoja na Brad Smith wakati wa uwakilishi wa Mpango mpya wa IA

Mfano wa "milele"

"Akili Bandia” inaturuhusu kufurahia Basilika hii kwa njia ya kipekee na ya ubunifu ambayo haijawahi kuonekana," alisema Brad Smith, makamu mwenyekiti na rais wa Microsoft, katika Chumba cha Waandishi wa Habari. "Ushirikiano huu, ambao unaunganisha taasisi na uvumbuzi wa kiteknolojia, umeunda uzoefu wa kukumbukwa kwa wale wote ambao wanataka kuzama zaidi katika historia na maana ya mahali hapa pa kushangaza. Tumeunda, pia kwa vizazi vijavyo, mfano wa Basilika ya Vatican ambayo itaishi milele,” alisisitza Bwana Smith kwa waandishi wa habari.

 

11 November 2024, 17:55