Mtazamo wa vijana kwenye michezo ni shindano la vijana la kupiga picha!
Na Giampaolo Mattei
"Sport in Motion - muhimu inabakia isiyoonekana kwa macho:" ndio mada ya shindano la kimataifa la upigaji picha linalohamaishwa na Baraza la Kipapa la utamaduni na elimu, kama sehemu ya Jubilei 2025, na kulenga vijana wenye umri chini ya miaka 25. "Mchezo na matumaini" ndiyo mada iliyopendekezwa, ikiwa na "kategoria" nne: "Mchezo na familia", "Michezo na ikolojia", "Michezo na ulemavu" na "Michezo na siasa." Hadi tarehe 30 Aprili 2025 itawezekana kuwasilisha picha ambazo hazijachapishwa - ambazo hazijarekebishwa kwa matumizi ya akili bandia zilizopigwa baada ya 2020 - kwa kutmia barua pepe: sportinmotion@dce.va.
Taarifa zaidi na sheria za mashindano - ushiriki ni bure na wazi kwa wote, hata wasio wataalamu - zinapatikana kwenye tovuti ya Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu (Dicastery for Culture and Education): www.dce.va. Kwa hiyo picha 13 zilizotunukiwa (moja kwa mada ya Michezo na Tumaini na tatu kwa kila kategoria nne) zitatangazwa Jumamosi tarehe 4 Juni 2025, kwa hafla ya Jubilei ya Michezo. Washindi kwa mujibu wa Taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu- watawasilishwa kwa Papa, watatembelea Makumbusho ya Vatican, hasa katika mtazamo wa uzoefu wa kisanii, na wataona picha zao zikisambazwa kupitia vyombo vya habari vya Vatican. Wanaounga mkono shindano hili kama washirika ni “Osservatore Romano”, Mkataba wa Kielimu Ulimwenguni, Mfuko wa Kipapa wa Gravissimum educationis na Athletica Vaticana.”
Baraza la majaji linaundwa na wawakilishi wa ukweli huu, pamoja na Giovanni Zenoni, mpiga picha kijana wa michezo, na Arturo Mariani, mwanasoka wa zamani wa timu ya taifa ya watu waliolemazwa na viungo na sasa ni kocha na mkufunzi wa akili. "Lengo la shindano ni kuchanganya maneno matatu ambayo si mara zote yanakaribiana kama inavyopaswa: sport-youth-art" kwa maelezo ya Kardinali José Tolentino de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya utamaduni na elimu.
Mkuu huyo amebainisha kwamba "Mpango huo wa upigaji picha unapendekezwa kama jukwaa la kisanii ambalo vijana wanaweza kuzungumza juu ya tumaini na katika mchezo", wakipitia "kama mahali pa matumaini". Na pia kuonesha "mwelekeo wa elimu, umoja kati ya utamaduni na elimu". Kwa hivyo, shindano hili ni pendekezo kwa vijana - hasa wanaohusika katika mazoezi, lugha na picha za michezo - ili "wawe wazalishaji wa sanaa na sio watumiaji wa sanaa tu" na “wanaweza kusema ukweli kupitia macho yao, kuona kile ambacho watu wazima hawawezi kuona kila wakati, kuonesha kwamba "muhimu ambayo haionekani kwa macho" kama ilivyoandikiwa kwenye kitabu cha (The Little Prince - Antoine de Saint-Exupéry).
Aidha amesisitiza kuwa "Mada zilizomo hasa kwenye mada kuu ya "tumaini", "kategoria" nne za mashindano (familia, ikolojia, ulemavu na siasa) zinapendekeza maono kamili, yenye pande nyingi ya uzoefu wa michezo. Imefumwa kwa maadili yaliyojumuishwa katika historia za wanadamu za ukombozi na udugu, za sadaka na uaminifu, roho ya kikundi na ushirikishwaji, kama vile katika Wimbo wa sifa kwa viumbe (Cantico delle creature) ambao ni pendekezo la amani. Lakini pia kudhoofishwa na "rushwa, vurugu, matumizi ya dawa za kulevya na ubaguzi wa rangi".