2024.11.16 huko Scutari, nchini Albania, Misa ya kuwatangaza wenyeheri iliyoongozwa na Kardinali Semeraro. 2024.11.16 huko Scutari, nchini Albania, Misa ya kuwatangaza wenyeheri iliyoongozwa na Kardinali Semeraro. 

Wenyeheri wapya Paliq na GazulliSemeraro:kuuawa kwa uongo katika kuishi ukweli wa Injili

Kardinali Marcello Semeraro aliongoza Misa Takatifu huko Scutari (Albania), akimwakilisha Baba Mtakatifu Francisko, katika Misa ya kuwatangaza wenyeheri mashahidi Luigi Paliq na Gjon Gazulli, ambao walikashifiwa na kuhukumiwa kifo kwa njia ya uongo katika utawala 1913 na 1926.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika enzi ya baada ya ukweli, ambapo habari potofu na uwongo huharibu maisha ya wengine na ya watu kupita kwenye mitandao, hadi kuifanya kuwa tatizo sana kutenganisha ukweli na uwongo, bado tuko na nia ya ukweli”? Hili ndilo swali lililoulizwa na Kardinali Marcello Semeraro Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifun katika mahubiri yaliyotolewa tarehe 16 Novemba, 2024 huko Scutari nchini Albania, ambako akimwakilisha Baba Mtakatifu Francisko, alitoa tafakari kwenye misa ya kumtangaza Wenyeheri, wafia dini Luigi Paliq na Gjon Gazulli.

Luigi Paliq na Gjon Gazulli walikuwa wakina nani?

Kardinali aliyafuatilia tena maisha ya wale waliotangazwa kuwa wenyeheri wawili wapya: wa kwanza, Luigi Paliq, Padre mfransiskani wa  Ndugu Wadogo, aliyezaliwa mwaka 1877 huko Janievo, Kosovo;  na akajua hatari zilizokuwapo wakati wa vita vya kwanza vya Balkan, katika awamu ya ukandamizaji wa kisiasa dhidi ya watu wa kabila la Albania, alibakia katika wadhifa wake akiendelea na huduma yake kwa uaminifu wa utume wake na, kabla ya kuuawa mwaka wa 1913, alithibitisha nia yake kamili ya kufa kwa ajili ya Kristo na kwa ajili ya Kanisa. Mwingine, Gjon Gazulli, padre wa Jimbo aliyezaliwa mwaka wa 1893 huko Dajc, Albania: hata kama mapadre wengi waliondoka nchini, chini ya utawala ulioanzishwa na rais wa Jamhuri hiyo,  Ahmet Zogu, alibaki kati ya watu wake na alikamatwa, akiwa chini ya uangalizi, kuonesha kesi na kuhukumiwa mwaka wa 1926 kwa mashtaka ya uwongo.

Wengi wanaoteswa na kuuawa 

Kardinali Semeraro kwa njia hiyo alipata msukumo wa tafakari yake kutoka kwa Heri za Kiinjili, hasa zile za mwisho, ambazo zinarejea historia ya  maumivu waliyopata Wakristo wengi, tangu mwanzo hadi leo, na pia matukio ya  hawa Paliq na Gazulli kwamba: Wenyeheri wetu wawili  ​​walifanya mema na walikashifiwa na kulaumiwa kwa uwongo. Kwa wote wawili, maneno ya Yesu yalitimia yasemayo: “Watawatukana ninyi, watawatesa na kusema kila neno baya kwa uongo juu yenu kwa ajili yangu.” Katika hiyo aliripoti huku  akinukuu maoni ya Mtakatifu Jerome  kwamba hata ndiyo sababu ya Heri “Kwa sababu kuna wengi wanaoteswa na kuuawa, lakini sio Heri; kwa upande mwingine, wale ‘wanaolaaniwa’, yaani, kusingiziwa, kukandamizwa na kuuawa kwa sababu ya Yesu, anamalizia: pale ambapo Kristo anahusika, basi kulaaniwa kunamaanisha kubarikiwa.

Uongo ni mgawanyiko, ukweli unaunganisha

Hata Papa Francisko Kardinali Semeraro alikumbuka, katika muktadha wa wito wa utakatifu wa ulimwengu wote aliacha maoni juu ya Heri za Injili na kusasisha uwepo huu wa uwongo katika mateso kwa kuandika kwamba wakati mwingine pia ni suala la dhihaka kuharibu imani yetu na kutufanya tuonekane kama watu wa kejeli. Papa anachokusudia kutuambia ni kwamba “neno la heri ya kiinjili linafaa hata pale ambapo hakuna mateso, lakini kuna kutojali, au dharau, kiasi kwamba kwamba kukubali njia ya Injili kila siku ingawa inatuletea matatizo, huu ni utakatifu” alisema Kardinali. Kwa hivyo “aliweka mkazo juu ya umuhimu wa  mada ya uwongo, udanganyifu na uwongo, ambayo hutenganisha na umbali sio tu kutoka kwa Kristo, bali pia kutoka kwa ndugu, kutoka kwa wengine kwa sababu uwongo ni mgawanyiko, huunda uadui, mapigano, kifo,  wakati ukweli sio tu unatuunganisha sisi kwa sisi, lakini unatuunganisha na Bwana Yesu, ambaye ni Kweli na Uzima.”

Kardinali Semeraro kwa wenyeheri wapya wa Albania
18 November 2024, 13:48