2024.11.29 Bwana David Choquehuanca Cespedes, Makamu rais wa Bolivia. 2024.11.29 Bwana David Choquehuanca Cespedes, Makamu rais wa Bolivia.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na Makamu rais wa Bolivia

Papa Francisko alikutana na Bwana David Choquehuanca Céspedes,Makamu rais wa Bolivia katika Jumba la Kitume mjini Vatican.Katika mazungumzo na Sekretarieti ya Vatican,Kardinali Parolin na Askofu Mkuu Gallagher walijikita na mada za mchango wa Kanisa Katoliki kwa jamii ya Bolivia na baadhi ya masuala ya hali ya kisiasa,kijamii na kiuchumi nchini humo.

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko alikutana katika Jumba la Kitume, Alhamisi tarehe 29 Novemba 2024 na Makamu wa Rais wa Bolivia David Choquehuanca Céspedes. Baadaye, kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican, Bwana Choquehuanca Céspedes alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akiambatana na Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.

Mahojiano katika Sekretarieti ya Nchi

Kwa mujibu wa taarifa inasomeka kuwa “Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti ya Vatican, uhusiano mzuri kati ya Vatican, Bolivia na Kanisa mahalia ulisisitizwa na mchango wa mwisho kwa jamii ya Bolivia ulizingatiwa.” Zaidi ya hayo, wakati wa mazungumzo “hawakukosa kujikita na baadhi ya vipengele vya hali ya kisiasa, kijamii na kiuchumi  nchini Bolivia.”

Kushiriki katika semina huko Jumba la Mtakatifu Calist

Bwana Choquehuanca Céspedes alishiriki tarehe 28 Novemba 2024  katika semina Kwenye Jumba la Mtakatifu  Calisiti kuhusu “kushughulikia matatizo ya mgogoro wa mazingira katika nuru ya  Waraka wa  Laudato si' na Laudate Deum, uzoefu katika Amerika ya Kusini,” iliyandaliwa na Ubalozi za Bolivia, Cuba na Venezuela wanawakilisha nchi zao mjini Vatican  kwa ushirikiano na Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini. Katika hotuba yake, makamu wa rais alishutumu “ubepari wa kijani, sababu ya mgogoro uliovuka ambao unaathiri hasa wakazi wa kiasilia, na pia wasomi wa nchi ambazo, kwa kutumia maendeleo ya uhandisi, huzalisha kile tunachokiona leo hii: vita, njaa.”

 

29 November 2024, 15:33