Papa akutana na waziri Mkuu wa Barbados Bi Mia Amor Mottley
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka msemaji mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya habari kwa waandishi wa habari imetaarifu kuwa: “Asubuhi , Alhamisi tarehe 14 Novemba 024, katika Jumba la Kitume jijini Vatican, Waziri Mkuu wa Barbados, Bi Mia Amor Mottley, alipokelewa katika Mkutano na Baba Mtakatifu Francisko. Baadaye, alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akifuatana na Monsinyo Monsław Wachowski, Katibu Msadizi wa Mahusiano na Mataifa.”
Katika taarifa hiyo aidha imebainisha kwamba “Wakati wa majadiliano mazuri katika Sekretarieti ya Vatican , kuridhika kulioneshwa kwa uhusiano mzuri kati ya Barbados na Vatican. Kisha waliakisi baadhi ya mada zenye maslahi kwa pande zote mbili kama vile utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi, pamoja na masuala ya sasa ya kisiasa ya kijamii ya nchi na eneo. Mkutano huo ulihitimishwa kwa kuthibitisha dhamira ya pande zote ya kuendeleza manufaa ya pamoja ya watu wa Barbados.”
Wakati wa kubadilishana zawadi, Baba Mtakatifu Francisko amempatia kazi ya shaba ambayo ina kauli mbiu “Upendo wa kijambii ambayo inaonesha mtoto ambaye anamsaidiza mwingine kuamka ikiwa na andiko “ Kupenda Kusaidia.” Kama kawaida pia Papa amempatia hati za kipapa, zikiwemo Ujumbe wa amani kwa mwaka 2024. Zawadi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Barbados ni sanamu ya mogano, ambayo ni kazi ya msanii wa Barbados.