Maaskofu wa Uganda Maaskofu wa Uganda  

Papa amemteua Askofu mpya wa Jimbo la Nebbi,Uganda

Papa amemteua Padre Constantine Rupiny,kuwa Askofu wa Jimbo la Nebbi(Uganda)kutoka Jimbo hilo hilo ambaye hadi uteuzi alikuwa Gambera wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mashahidi wa Uganda huko Alokolum,katika Jimbo Kuu la Gulu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumanne tarehe 26 Novemba 2024, Baba Mtakatifu amemteua Padre Constantine Rupiny, kuwa Askofu wa Jimbo la Nebbi  nchini Uganda kutoka Jimbo hilo hilo ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni  Gambera wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mashahidi wa Uganda huko Alokolum, katika Jimbo Kuu la Gulu.

Wasifu wake

Padre Constantine Rupiny alizaliwa tarehe 10 Novemba 1974 huko Parombo, katika Jimbo la   Nebbi. Alimaliza masomo yake ya falsafa katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mashahidi wa Uganda ya Alokolum, katika Jimbo Kuu la Gulu (1996-1999), na masomo yake ya kitaalimungu katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Maria ya Ggaba, katika Jimbo Kuu la Kampala (2000-2004). Baadaye alipata Leseni ya Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana cha Roma (2009-2011) na Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya  Dogmatiki kutoka Chuo Kikuu cha Kardinali Stefan Wyszyński cha Warsaw, Poland (2018-2022).

Mnamo tarehe 28 Agosti 2004 alipewa daraja Takatifu la Upadre.

Nyadhifa nyingine

Alishika nyadhifa zifuatazo: Padre wa parokia ya Kango (2004-2005); paroko wa Akanyo (2005-2007); Mkufunzi na Profesa katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mashahidi wa Uganda huko Alokolum (2007-2009, na 2011-2018); Makamu wa Rais wa Baraza la Makleri wa Nebbi (2017-2018); Makamu Mkuu wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mashahidi wa Uganda huko Alokolum (Januari-Septemba 2023) na, kuanzia Septemba 2023, Gambera wa seminari kuu hiyo hiyo.

Askofu Mpya Nebbi Uganda
26 November 2024, 15:30