Jengo la Baraza la Kipapa kwa ajili ya Unjilishaji Jengo la Baraza la Kipapa kwa ajili ya Unjilishaji 

Papa amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji

Alhamisi tarehe 7 Novemba 2024,Papa amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji,katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya,Monsinyo Erwin José Aserios Balagapo,hadi uteuzi wake alikuwa Mkuu wa Ofisi ya Baraza hilo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Alhamisi tarehe 7 Novemba 2024,Papa amemteua Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji,katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya,Monsinyo Erwin José Aserios Balagapo,hadi uteuzi wake alikuwa Mkuu wa Ofisi ya Baraza hilo.

Wadhifa wake

Padre Balagapo alizaliwa huko Catbalogan (Ufilipino) tarehe 8 Machi 1971 na akapewa daraja la Upadre kwa Jimbo kuu la Palo tarehe 12 Julai 1996.  Katika masomo ya juu jijini Roma alipata Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu na Leseni ya Taalimungu ya Maadili kutoka katika Taasisi ya Kipapa  ya Yohane Paulo II ya wakati ule. Katika Jimbo Kuu la Ukasisi, pamoja na majukumu mengine, alikuwa pia Profesa wa Sheria ya Canon, Anayewajibika kwa malezi ya kudumu ya mapadre, Wakili wa Mahakama na Kansela. Afisa wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu la wakati huo tangu mwaka 2015 hadi Julai 2023 aliteuliwa kuwa Mkuu wa Ofisi katika Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mahususi mapya ya Baraza hilo la Uinjilishaji.

Na wakati huo huo kwa nafasi hiyo ya Ofisi katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, pia Baba Mtakatifu amemteua  Padre  Sergio Bertocchi, Mkleri wa Jimbo kuu la Bergamo nchini Italia, kuwa Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Uinjilishaji, Sehemu ya Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya.

07 November 2024, 15:43