PAPA MONTINI - PAULO VI PAPA MONTINI - PAULO VI 

Paulo VI,Semeraro:aliunganisha mawazo na matendo ili kulipatia Kanisa sura mpya

Katika kuadhimisha miaka 10 kutangazwa mwenyeheri Papa Montini,Mwenyekiti wa Baraza la kutangaza Watakatifu alizungumza katika mkutano huko Concesio uliofunguliwa kwa ziara ya alipozaliwa Papa huyo.Katika ripoti kuhusu utakatifu wa Kikristo leo na kielelezo kilichotolewa na Paulo VI,ni kwamba hekima ya kichungaji,usikivu wa kisasa na uaminifu kwa Injili hujitokeza ndani yake.Alikuwa na Shauku ya Kristo kama kielelezo cha maisha yake yote ya duniani.

Na Tiziana Campisi – Vatican.

Utakatifu ni njia ya kujifananisha na Kristo na ni njia pekee kwa sababu ina kipimo chake na kigezo chake katika Kristo, lakini mifano yake katika historia imebadilika kwa hakika. Kuanzia msingi huu, Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa  Baraza la  Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, alieleza katika hotuba yake kwenye mkutano uliofanyika huko Concesio alasiri tarehe 29 Novemba 2024, wakati wa kuadhimisha miaka kumi tangu Papa Montini alipotangazwa kuwa mwenyeheri. Tukio hilo lilianza katika mahali Alipozaliwa Mtakatifu Paulo wa Sita kwa uzinduzi wa Ziara ya Kawaida ya Mahali pa Kuzaliwa kwa G.B. Montini- yaani Papa Paolo VI” na kisha kuendelea katika Ukumbi wa Vittorio Montini katika Taasisi ya Paolo VI.

Papa wa kisasa

Katika hotuba yake, yenye kichwa 'Utakatifu wa Kikristo leo hii, kielelezo cha Paulo VI,' Kardinali  Semeraro alikumbuka sifa zilizoakisiwa na Carlo Cardia, akimfafanua kuwa Papa ambaye katika usasa ametoa majibu mengi kwa maswali ya mwanadamu na ambaye ameunganisha zaidi fikra na hatua katika kulipatia Kanisa jipya uso, wenye uwezo wa kumkaribisha mtu wa kisasa na mahitaji yake. Lakini wakati huo huo, kutambua msingi, thamani, mashaka yake, kutokuwa na hakika kwake, kuifanya kuwa chombo cha kiroho, cha imani. Na maneno ya Kardinali Carlo Maria Martini, mnamo mwaka wa 84, katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, kuhusu imani yake wazi na kukomaa, ambayo iliweza kujieleza hata katika umri na utamaduni wa kutoamini, kutokuwa na dini, mtu wa umri wa  fahari kwa maendeleo yake au kukata tamaa kwa upweke wake.

Mtakatifu Paulo VI

Kardinali Semeraro alizingatia mambo matatu: utakatifu wa Paulo VI kama ulivyoainishwa katika mchakato wa kisheria ambao ulifikia kilele cha kutangazwa kuwa mtakatifu tarehe 14 Oktoba 2018; Majisterio, Kutoka Milano  na Roma,  juu ya mada ya utakatifu; maandishi ya Mtakatifu Paulo yasemayo:  "Siishi tena. Lakini Kristo anaishi ndani yangu” -yaliyozingatiwa na Romano Guardini kuwa kiini cha utakatifu wa Kikristo kama inavyoeleweka na Montini. Kuhusu jambo la kwanza, Kardinali alirudia, kwamba, kile ambacho Papa Francisko alisema kwenye sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 1 Novemba 2017 kuwa: “Watakatifu ni kaka na dada zetu ambao waliikaribisha nuru ya Mungu mioyoni mwao na kuisambaza kwa ulimwengu” na “kujitahidi kuondoa madoa na giza la dhambi, ili kuruhusu nuru ya upole ya Mungu ipite. Hili ndilo kusudi la maisha: kuruhusu nuru ya Mungu ipite. Msingi wa kutambulisha kile kilichojitokeza kuhusu Paulo VI katika mchakato wa kisheria: "hisia hizo zinapatikana ndani yake au kujitambua sisi wenyewe tunaopata ndani ya Yesu na kwamba kila mtu aliyebatizwa anapaswa pia kukumbuka, hasa kwa msingi wa kuwa kwake Kristo; katika nuru ya Kristo aliona na kupima maisha hapa chini."

Haya ni mambo ambayo pia yanajitokeza katika hotuba ya Montini mwenyewe kwa wanafunzi wa shule za Kikatoliki za Roma, tarehe 25 Februari 1978, alipowaambia watoto kwamba "suluhisho kali la matatizo yenu haliko katika mchanganyiko wa 'mambo' , lakini katika 'Mtu fulani. Mtu ambaye maadili yote mnayotafuta kwa siri yameunganishwa tena: Kristo, akihimiza, basi, kwenda kumlaki, Kristo aliye hai, ambaye sauti yake ingali inasikika katika Kanisa leo, bila kuacha juu na kukusanya ujumbe, ambao Kanisa ni mbeba hakika, kwa sababu linasaidiwa na Roho. Kwa ufupi, Kardinali alisisitiza kuwa: shauku ya Kristo ni kipauimbele cha maisha yake yote ya duniani.

Utakatifu kulingana na Montini

Kuhusu mafundisho ya Montini  ya mada ya utakatifu, Kardinali Semeraro alipendekeza kifungu kutoka katika Katekesi ya tarehe 9 Julai 1975, Mwaka Mtakatifu, ambapo Papa alielezea kwamba yeyote anayekubali kuwa Mkristo chanya anahisi, kwa wakati fulani zaidi zaidi. hitaji kali la ukamilifu, akiongeza kwamba kuwa na Mungu kama kielelezo cha ukamilifu ni kichocheo cha kuwa sawa katika uhalisi na Mungu huyo, ambaye sura yake isiyoelezeka imetiwa alama kwenye nyuso zetu na kwamba ni Kristo ambaye anatupa kimo hiki cha kweli cha mwanadamu, aina hii halisi ya mtu mkuu.

Kardinali Semeraro alisema kuwa wakati alipokuwa Askofu mkuu wa Milano, kwa ajili ya sikukuu ya Watakatifu Wote mwaka 1957, hata hivyo, Montini alisema kwamba utakatifu unawezekana na kwamba si wito wa kipekee na wa kipekee kwa baadhi ya roho kuu, bali ni wito kwa wote , ikionesha katika upendo kiini cha ukamilifu, mzizi wa matendo yote ya Kikristo, njia kuu ya utakatifu: njia ambayo kila mtu anaweza kufuata na kwamba Kanisa haliachi kamwe kuwasilisha watu wa utakatifu, kama wanariadha wa kitubio, mashujaa wa kifo cha kishahidi kwa pongezi na ibada ya waamini wanayotoa, hata hivyo, kwa kuiga kawaid,amifano inayopatikana zaidi. Miundo ya nje na njia za hiari ambazo roho hujizatiti ili kushinda ukamilifu zinathaminiwa kila wakati", alitamka kiongozi wa wakati huo, lakini upendeleo huenda kwenye kiini cha ukamilifu, upendo. Kwa Semeraro, maneno haya huleta pamoja uzoefu wa kibinafsi, hekima ya kichungaji, usikivu wa kisasa, uaminifu kwa Injili.  Haya yote yanarejelea kanuni inayojirudia ya Papa Francisko: utakatifu wa jirani, aliona kardinali.

"Kristo anaishi ndani yangu"

Hatimaye, kuhusu aya ya barua ya Paulo kwa Wagalatia isema "Mimi si hai tena, lakini Kristo yu hai ndani yangu," Kardinali Semeraro alionesha baadhi ya matukio mengi ambayo Paulo VI akisisitiza juu ya maana ya kauli ya mtume wa watu, ambapo katika Katekesi yake mnamo  tarehe 15 Januari 1964 inajitokeza, baada ya safari ya Duniani. Mtakatifu Paulo VI alisema: Sisi ni Wakristo, kweli; baada ya karne nyingi sana, na uzoefu mwingi wa kihistoria unaobadilika, bado tunafanana na Yeye alituumba na kututaka sisi, kwa neema yake, wanafunzi wake wa kweli, kwa hakika sisi ni mitume wake halisi, wawakilishi wake halisi."

Mtakatifu Paulo VI pia alifafanua kwamba: Kanisa la Kristo hutuzalisha sisi sawa na Yeye, ndugu zake, wafuasi wake, marafiki zake wapenzi, kwa njia ya "mani, neema, kuingizwa katika Mwili wake wa fumbo na kwa sababu hii kila mmoja wetu anaweza kusema, tena. pamoja na Mtakatifu Paulo asemaye: Naishi, lakini si mimi tena; Kristo anaishi ndani yangu Muungano huu na Kristo, ambao Montini, akiwaandikia mapadre katika Juma Takatifu la 1961, anaeleza kuwa ni uwepo ndani yetu pia una mawasiliano na ushuhuda uliotolewa katika mchakato wa kutangazwa kuwa Mwenyeheri na kutangazwa kuwa Mtakatifu. Kwa hiyo Kardinali Semeraro alihitimishwa akisema kwamba wakati ambapo mmoja wa watawa walioishi naye katika Jumba la kitume jijini Vatican alitangaza kwamba "alipokuwa katika Kanisa, macho yake yalikuwa yakitazama hema na, alionekana kama mtu anayevutiwa na mbinguni."

Sifa za Paulo VI
30 November 2024, 13:07