Papa atatoa heshima katika Siku ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya sili katika Uwanja wa Hispania jijini Roma tarehe 8 Desemba 2024. Papa atatoa heshima katika Siku ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya sili katika Uwanja wa Hispania jijini Roma tarehe 8 Desemba 2024. 

Siku ya Bikira Maria Mkingiwa,Papa atatoa heshima ya kiutamaduni katika Uwanja wa Hispania

Dominika tarehe 8 Desemba 2024,siku nzima,itakuwa na matukio mbali mbali jijini Roma,ikiwa ni pamoja na Papa Francisko atakayetoa heshima kwa Picha ya Bikira Maria katika Uwanja wa Hispania.Katika Basilika ya Watakatifu Mitume XII kuanzia tarehe 29 Novemba hadi tarehe 7 Disemba inaendelea Novena kwa kusali Rozari na litania na kufuatiwa na Misa inayoongozwa kila siku na mmoja wa Makardinali wa Curia Romana.

Vatican News

Sherehe ya Mkingiwa dhambi ya Asili kwa Bikira Maria itaadhimishwa Dominika  tarehe 8 Desemba 2024. Katika hafla ya maadhimisho hayo, siku nzima raia wa Kirumi watatoa heshima zao kwa sanamu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili katika Uwanja wa Mignanelli, karibu na Uwanja wa Hispania Jijini Roma. bKulingana na maadhimisho haya ya kiutamaduni, wa kwanza watakuwa kikosi cha wazima moto, kwa heshima ya wenzao 220 ambao walizindua mnara huo mnamo tarehe  8 Desemba 1857: saa 11 alfajiri na mapema  watapanda juu ili kuweka shada la maua kwenye mkono wa Bikira Maria. Baba Mtakatifu Francisko pia atashiriki katika ibada ya kiutamadini  ambayo kanatarajia kuwasili katika Uwanja wa Hispania jioni saa 10.00 na  atasali mbele ya mnara huo wa Bikira Maria na wakati huo huo kuweka shada la maua kwenye mnara wake.

Pongezi kutoka kwa vikundi tofauti

Kabla ya Papa, vikundi na watu wengi wataacha mataji yao ya mau chini ya mnara wenye urefu wa mita 12, iliyoundwa na mbunifu Luigi Poletti, ambayo juu yake inasimama sanamu ya shaba ya Maria iliyoundwa na mchongaji Giuseppe Obici. Kikokosi cha Ulinzi cha Vatican pia watatoa heshima zao, huku bendi ya muziki ikiimba wimbo wa Maria; parokia ya Myakatifu Andrea dwa Fratte, Shirika la Kijeshi la Malta, Legio Mariae, Udugu wa Mtakatifu Pietro, Mfuko wa Padre Gnocchi na wengine wengi. Bila kusahau msafara mkubwa wa wafanyakazi kutoka kwa kampuni muhimu zaidi za Kirumi, pamoja na kampuni za manispaa zote , balozi wa Uhispania anayewakilisha Nchi yak Vatican akiwa na vikundi vya Hispania, na  Unitalsi(kikundi kinachojikita na usaidizi wa wagonjwa, wazee na walemavu Italia.

Nyimbo na sala kuongozwa na ndugu wadogo

Kuanzia saa kumi na moja alfajiri  na kutwa nzima, Ndugu Wadogo wa Kikonventuli wa Basilika ya Mitume watakatifu wa XII watakuwa uwanjani kukaribisha vikundi na waamini binafsi, wakihuisha kwa nyimbo na sala. "Siku ya tarehe 8 Desemba ni fursa nzuri ya uinjilishaji - anaelezea Padre wa Parokia na mkuu wa Basilica, Padre Francesco Celestino - kwa sababu una fursa ya kukutana na watu wengi. Ushiriki katika ibada huongezeka mwaka baada ya mwaka.” Zaidi ya hayo, novena kongwe zaidi kwa Mkingiwa Dhambi ya Asili  jijini Roma hufanyika katika Basilika ya   Mitume Watakatifu wa XII: kuanzia tarehe 29 Novemba hadi tarehe 7 Disemba 2024 na wakati huo huo kusali Rozari na kuimbaji  litania, ambapo inatarajiwa kuanzia saa 11.45 hadi saa 12.30 jioni kufuatia , Misa daima ikinaongozwa na Kardinali na wimbo wa Tota Pulchra, ambao ulitungwa na Padre Alessandro Borroni, mmoja wa ndugu wadogo walioishi katika karne ya kumi na tisa.”

Misa kuoongozwa na makardinali

Misa takatifu katika Novena kuanzia 29 Novemba hadi 7 Desemba 2024: Ijumaa tarehe 29, Kardinali João Braz De Aviz, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Maisha ya Wakfu; siku ya Jumamosi tarehe 30  2024 itakuwa ni zamu ya Kardinali Lazzarro You Heung-Sik, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya wakleri; wakati tarehe 1 Desemba 2024  itakuwa zamu ya Kardinali Mauro Gambetti, mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na Msimamizi wa Jiji la Vatican. Tena, Jumatatu tarehe 2 Desemba 2024, Kardinali Dominique Mamberti, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Saini za Kitume, ataadhimisha Misa; tarehe 3 Desemba, Kardinali Angelo De Donatis, Mkuu wa Toba ya kutume ; Jumatano tarehe 4 Desemba, Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Makanisa ya Mashariki.

Kardinali Fernando Vérgez Alzaga, rais wa Utawa wa Mji wa Vatican ataongoza misa tarehe 5  Desemba; Ijumaa  tarehe 6 Desemba, Kardinali Robert Francis Prevost, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Maaskofu; hatimaye Jumamosi tarehe 7 Desemba 2024 atakuwa Kardinali François-Xavier Bustillo, Askofu wa Ajaccio. Siku ya Dominika  tarehe 8 Desemba 2024, maadhimisho ya Siku kuu ya Mkingiwa dhambi ya Asili imepangwa kuadhimishwa  saa 3.00 na 10.30 asubuhi; saa 11.45 jioni kusali Rozari na uimbaji wa litaani; saa 12.30 jioni, maadhimisho ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu itayoongozwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, na Kardinali Dominique Joseph Mathieu, Askofu Mkuu wa Tehran-Isfahan wa Kilatini. Sherehe zote zitahuishwa na Waimbaji wa Muziki wa Konstantini ya Basilika.

Papa ataweka shada la Maua kwa heshima ya Bikira maria
29 November 2024, 16:37