Tafuta

2024.10.31 Askofu Mkuu  Gallagher akiwa huko Montreal katika Mkutano kuhusu mtindo wa amani kwa ajili ya Ukraine. 2024.10.31 Askofu Mkuu Gallagher akiwa huko Montreal katika Mkutano kuhusu mtindo wa amani kwa ajili ya Ukraine. 

Ukraine,Gallagher:Vatican imejitolea kurudisha watoto,askari na raia

Katibu wa Uhusiano na Mataifa ameshiriki huko Montreal Kongamano la Mfumo wa Amani:“Kesi zilizokabidhiwa Vatican zilikuwa ngumu,matokeo hayakukidhi matarajio.Maelfu ya majina ya wafungwa yaliwasilishwa ili kuachiliwa.Baloziwa Vatican huko Kyiv amebainisha taasisi za Kikatoliki ziko tayari kukaribisha familia zilizo na watoto waliorudishwa makwao.Askofu mkuu alihimiza kuepuka unyonyaji wowote wa masuala ya kibinadamu na kutafuta mema ya waathirika

Na Salvatore Cernuzio – Vatican

Kwa bahati mbaya, matokeo hayakukidhi matarajio, labda kwa sababu kesi zilizokabidhiwa ni ngumu zaidi, hata hivyo Vatican  inaendelea katika ahadi yake ya kibinadamu ya kuachiliwa kwa watoto waliowekwa kizuizini, wanajeshi wa Ukraine na raia. Ili kuthibitisha hili kwa kuchanganya hili na kutoa wito ili kuepuka unyonyaji wa masuala ya kibinadamu, ndivyo alisisitiza Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican anayeshughulikia Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, wakati akizungumza huko Montreal, nchini Canada, katika Mkutano wa Mawaziri kuhusu mada ya 'Mwelekeo wa Binadamu wa Mfumo wa Amani wa Ukraine.' Huo ulikuwa ni mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu Mtindo wa  amani uliopendekezwa na rais wa Ukraine ,Bwana Volodymyr Zelensky, ambao unafuatia mkutano nchini Uswiss wa mwezi  Juni 2023.  Hili lilikuwa ni tukio la siku mbili nchini Canada kuanzia tarehe 30-31 Oktoba 2024 uliojikita na mada “Pendekezo namba 4” kati ya vipengele kumi vinavyounda Mfumo: “ukombozi wa wafungwa wote na wahamishwaji.” Na hiyo ndiyo misheni ambayo Vatican  imefanya tangu kuzuka kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine,  kwa kukaribisha  maombi ya mara kwa mara ya mamlaka ya Ukraine,”  alikumbuka Askofu Mkuu Gallagher. 

Rais wa Ukraine aliomba msaada kwa Papa 

Rais Zelensky, kama inavyojulikana, alisisitiza ombi lake la msaada kutoka kwa Papa kwenye Mkutano wa tatu jijini Vatican  mnamo tarehe 11 Oktoba 2024. Aina hii ya usaidizi wa kibinadamu wakati huo ilikuwa “lengo kuu la utume wa Kardinali Zuppi huko Kyiv na Moscow,, alisisitiza  Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa, akimaanisha safari ya rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI) huko Ukraine na Urusi katika msimu wa joto wa 2023 (pia alikwenda Marekani na China)kama mjumbe wa Papa kutafuta “njia za amani ya haki kwa nchi iliyoteswa.” Karidnali Zuppi kisha akarudi Moscow mnamo 14 na 15 Oktoba 2024. Misheni hii, ilisisitizwa na Asofu Mkuu Gallagher huko Montreal, kwamba “imesababisha kuundwa kwa mfumo wa kuwarudisha watoto makwao na kubadilishana habari mara kwa mara kati ya pande hizo mbili. Hii pia ilijumuisha mikutano ya mtandaoni na ushiriki wa mabalozi wa kitume katika nchi hizo mbili”, Visvaldas Kulbokas nchini Ukraine na Giovanni d'Aniello nchini Urusi.

Msaada wa Mabalozi  wawili wa kitume

Hata kama matokeo hayaridhishi, Askofu mkuu alisema, hata hivyo "mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande zote, hasa na uwepo wa wajumbe wawili wa kitume, ni muhimu kwa kuwezesha mazungumzo". Kulbokas, hasa ametambua taasisi za Kikatoliki tayari kukaribisha familia zilizo na watoto waliorudishwa makwao". Na wakati huu Vatican inasisitiza maombi yake ya orodha mpya za watoto. Si hivyo tu, Vatican pia kilisambaza maelfu ya majina ya wafungwa, wakiomba kubadilishana na kuachiliwa. Pia iliunga mkono pendekezo la kuanzisha tume za matibabu za pamoja kwa wafungwa walio na hali mbaya ya kiafya na iliunga mkono ombi la familia za wafungwa wa Ukraine kupeleka misaada ya kibinadamu kwao. Mwishowe, aliuliza upande wa Urusi kuhamisha askari wa Ukraini waliokufa.

Hali ya wafungwa wa Urusi huko Ukraine

Balozi wa Vatican huko  Kyiv nchini Ukraine alifahamisha Askofu Mkuu Monsignor Gallagher, kuwa “alitembelea baadhi ya wafungwa wa Kirusi huko Ukraine, akibainisha hali zao nzuri.” Uhakikisho kama huo, kuhusu hali ya wafungwa wa Kiukreni, ulitolewa na Ombudswoman wa Shirikisho la Urusi (mchunguzi wa kesi wa Urusi, aliyeteuliwa rasmi Kamishna wa Haki za Kibinadamu, ed.), lakini bila uwezekano wa Vatican kuthibitisha  hali yao.”

Hapana kwa unyonyaji

Kwa kumalizia, Katibu wa Uhusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa alialika "wahusika kujiepusha na unyonyaji wowote wa masuala ya kibinadamu" na akasisitiza "haja ya kujitolea kutafuta suluhisho kwa dharura za kibinadamu, pia kama njia ya nia njema kuelekea amani" .

02 November 2024, 13:26