Askofu Mkuu Ettore Balestrero. Askofu Mkuu Ettore Balestrero. 

Vatican:hatua za ujasiri katika biashara na nchi zilizoendelea kidogo

Ushiriki wa Nchi zilizoendelea kidogo(LDCs)katika mabadilishano ya kimataifa pia unahusisha maendeleo fungamani na endelevu ya kidijitali.Ndiyo yaliyosemwa na Askofu Mkuu Ettore Balestrero,Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa,katika hotuba yake kwenye kikao cha 76 cha Baraza la Biashara na Maendeleo la Unctad.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya kimataifa lazima ichukue hatua za ujasiri, kwa kuzingatia ahadi zilizopo, kuongeza ushiriki wa nchi zilizoendelea kidogo katika biashara ya kimataifa, kubadilisha bidhaa zao nje na kujenga uwezo wao wa uzalishaji. Huu ndio msimamo wa Vatican  uliotolewa na Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu  Ettore Balestrero, katika hafla ya kikao cha 76 cha Baraza la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD) kilichofanyika  njini Geneva Alhamisi 31 Oktoba 2024.

Mshikamano na nchi zilizoendelea kidogo

Tukio hilo, katika maono ya Askofu Mkuu Balestrero, liliwakilisha fursa ya kutafakari juu ya kazi ya Unctad katika kusaidia zile zinazoitwa nchi zenye maendeleo duni zaidi (LDCs), yaani mataifa yaliyoathirika zaidi na umaskini. Usaidizi unaohitaji mshikamano zaidi na kuimarishwa"kwa ushirikiano wa kimataifa.

Maendeleo ambayo sio ya kiuchumi tu

Mjumbe wa Vatican alipendekeza baadhi ya maeneo yanayoweza kuingilia kati. Kwanza kabisa, msaada ambao haukomei katika kuzingatia masuala ya kiuchumi pekee, ukisisitiza jinsi utekelezaji huo, ukichukua mawazo ya Papa Francisko katika waraka wa Fratelli tutti, umethibitika kuwa na ufanisi kwa ukuaji, lakini si sawa kwa maendeleo muhimu ya binadamu.

Kupambana na umaskini na ukosefu wa usawa

Vatican aidha imea imepongeza juhudi za UNCTAD katika kuchunguza athari za sera za kijamii na kiuchumi katika kuendeleza umaskini na ukosefu wa usawa, na kubainisha haja ya wazi ya kuzingatia hasa athari zinazotokana na wao, hasa kuhusiana na upatikanaji wa huduma na huduma ya elimu.

Maendeleo yanayoagizwa na biashara ya kimataifa

Pili, Askofu Mkuu Balestrero alikumbusha jinsi ambavyo biashara ya kimataifa  ikiwa ina mwelekeo mzuri, inakuza maendeleo. Hata hivyo, LDCs bado zinaitwa kukabiliana na changamoto kubwa ili kufaidika kikamilifu na faida, kwa mfano, ya uwekezaji kutoka nje. Ili kuongeza faida ya kibiashara kwa LDCs, baadhi ya sera zinapendekezwa, kuanzia uwezeshaji mkubwa wa biashara hadi mikataba ya upendeleo ya biashara.

Ujumuishaji na uendelevu wa teknolojia

Sehemu ya tatu na ya mwisho ya kuingilia kati inahusishwa kwa karibu na maendeleo ya maendeleo ya kidijitali. Askofu Mkuu alibainisha kuwa inaleta ahadi kubwa za maendeleo fungamani na endelevu. Hata hivyo, lengo la dunia iliyounganishwa, lisilowezekana kufikiwa bila upatikanaji wa mtandao wa bei nafuu  bado liko mbali na kufikiwa, kutokana na mzigo wa gharama, ukosefu wa ujuzi na miundombinu katika LDCs. Bila ya utekelezaji wa teknolojia mpya ambayo ni fungamani, endelevu na inayowajibika, kulingana na Holy See, kuna hatari ya kuyumba kwa soko la ajira na kuzorota zaidi kwa ukosefu wa usawa.

02 November 2024, 12:43