2024.11.20: Toleo jipya la "Ibada ya Mazishi ya Papa wa Roma." 2024.11.20: Toleo jipya la "Ibada ya Mazishi ya Papa wa Roma." 

Vatican imechapisha toleo jipya la ibada za mazishi ya Papa wa Roma

Papa Francisko aliidhinisha mnamo mwezi Aprili iliyopita, toleo jipya la kitabu cha kiliturujia kwa ajili ya ibada za mazishi ya Papa ambacho kiliandikwa na Ofisi ya Maadhimisho Makuu ya Liturujia za Kipapa.

Vatican News

Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa imetayarisha na kutekeleza toleo la pili la (Ordo Exsequiarum Romani Pontificis,) yaani kitabu cha Mazishi ya Kipapa)lililodhinishwa mnamo tarehe 29 Aprili 2024 na Baba Mtakatifu Francisko, ambaye alipokea nakala ya kwanza ya kitabu kilichochapishwa tarehe 4 Novemba 2024.

Idadi ya vipengele vipya vya mazishi ya upapa vimeanzishwa. Uthibitisho wa kifo hautafanyika tena katika chumba cha marehemu lakini katika Kanisa, na mabaki yake yatawekwa mara moja ndani ya Jeneza. Waamini wataweza kuheshimu mwili wa Papa ndani ya Jeneza wazi, na utamaduni wa kuwa na jeneza tatu za mbao ngumu (cypress, lead-Mwaloni na oak -risasi) zimeondolewa.

Kitabu hicho cha kiliturujia kiliwasilishwa kama toleo jipya kufuatia mtangulizi wake,  wa toleo la Ordo Exsequiarum Romani Pontificis, lililoidhinishwa mnamo mwaka 1998 na Mtakatifu Yohane Paulo II na kuchapishwa mwaka 2000, ambalo lilitumika katika mazishi ya Papa huyo huyo mnamo mwaka wa 2005  pamoja na marekebisho, katika yale yaliyofanyika kwa  Papa Benedikto XVI mnamo mwaka 2023.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Diego Ravelli, Msimamizi wa Sherehe za Kitume, alieleza kwamba: “Toleo la pili lilikuwa la lazima,   awali ya yote, kwa sababu Papa Francisko ameomba, kama yeye mwenyewe amevyoeleza mara kadhaa kuhusu hitaji la kurahisisha na kuzoea ibada fulani ili adhimisho hilo lifanyike la mazishi ya Askofu wa Roma  ambyo yanaweza kueleza vyema zaidi imani ya Kanisa katika Kristo Mfufuka." Askofu Mkuu Ravelli pia alibainisha kwamba "ibada iliyofanywa upya ilihitaji pia kusisitiza zaidi kwamba mazishi ya Papa wa Roma ni ya mchungaji na mfuasi wa Kristo na si ya mtu mwenye nguvu ya ulimwengu huu."

Toleo Jipya 2024 kuhusu mazishi ya kipapa
20 November 2024, 16:32