Tafuta

Mkutano wa Baraza la Makardinali washuari wa Papa (C9). Mkutano wa Baraza la Makardinali washuari wa Papa (C9). 

C9:Mkutano wa Baraza la Makardinali washauri wa Papa unaendelea

Katika kikao cha 4 cha Mkutano wa Makardinali washauri wa Papa kwa mwaka huu kinachoendelea kilitanguliwa na kile cha mwezi Februari,Aprili na Juni.Kikao cha mwisho pamoja,kiliwaona pia uwepo wa mtawa mmoja na walei wawili wanawake.

Vatican News

Jumatatu tarehe 2 Desemba 2024 asubuhi kwa uwepo wa Papa walikutana mjini Vatican Baraza la Makardinali wajulikanao kama C9, ambacho ni kikundi kazi kichoundwa na Makardinali 9 washauri wa Papa Francisko na ambao walipyaishwa tena  Papa mwenyewe kunako Machi 2023. Kikao kinachoendelea mwaka huu,  ni cha nne baada ya kile kilichofanyika kunako mwezi Februari kuanzia 5-7; Aprili kuanzia 15-16 na Juni kuanzia  tarehe 17-18.

Kikao cha mwisho kilihusisha hata wanawake 3

Katika mkutano wa mwisho wa mwezi Juni, nafasi ya kutosha ilitolewa kwa masuala ya Ulinzi wa Watoto wadogo na nafasi ya wanawake katika Kanisa, shukrani pia kwa uwepo na uingiliaji kati wa Mtawa mmoja Sr Linda Pocher, na walei wawili, walimu Valentina Rotondi na Donata Horak.

Mkutano wa Papa na Makardinali washauri C9
03 December 2024, 09:32