Kard.Krajewski aadhimisha Misa ya Noeli Ukraine iliyokumbwa na vita
Vatican News.
Akizungumza na Vatican News Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, kuhusiana na athari za utume wake mpya nchini Ukraine, sauti ya ilikuwa shwari kwa “Tunahitaji kukaa na watu hawa, kwa nafasi yetu Yesu angefanya vivyo hivyo.” Mjumebwa Papa kwa mara nyingine, ulikuwa ni utume ulioundwa kwa ajili ya kupeleka kambi ya matibabu kwa ajili ya Lviv kama zawadi kutoka kwa Papa Francisko na mashine sita za uchunguzi wa ultrasound zinazopelekwa katika hospitali zilizopigwa mabomu. Kwa hakika Yeye anajua hatari ya mpango huo katika nchi ambayo imekuwa na vita kwa miaka kadhaa sasa, hata Papa Francisko anaijua na kiukweli anafuatilia habari kila wakati.
Mjumbe wa Papa alisema kwamba: "Jioni moja, niliporudi kutoka Kyiv Baba Mtakatifu aliniita, alitaka kujua jinsi gani misheni hii inafanywa ambayo, kama tunavyojua, ni hatari kidogo." Baada ya safari ndefu, Kardinali Krajewski na balozi wa Vatican nchini Ukraine, Askofu Mkuu Visvaldas Kulbokas,tarehe 23 Desemba walifika katika eneo la vita "ambapo watu wanateseka." Hapa karibu na "kundi hilo dogo lililosalia" walidhimisha Misa ya Noeli.
Pamoja kuumega mkate
Katika picha zilizotumwa na Kardinali Konrad Krajewski, rangi za nguo za kiutamaduni zilionekana kuwa watoto wengi huko Fastiv, jiji lenye wakazi elfu 60, kilomita 80 kusini-magharibi mwa Kyiv, ambapo walivaa kuonesha maonesho ya Noeli, "iliyoandaliwa kwa moyo", ambayo walikuwa wameitayarisha. Miongoni mwao, alisema Kardinali, watoto wengi kutoka shule ya muziki ambao walikuwa yatima kutokana na vita.
Watoto hao Walipewa midori ya (teddy bears). Muda mfupi kabla, Kardinali Krajewski alikuwa amekwenda kwenye jengo linaloitwa "nyumba ya kijamii" ambapo wazee wengi wanaishi, aliwatembelea wagonjwa kwa kumega mkate mweupe, ambayo ni "desturi ya kutamani ya Noeli.” Katika Fastiv Kituo cha Mtakatifu Martino de Porres kinafanya kazi, ambacho kinachosimamiwa na Mapadre Wadominikani. "Ni hapa ambapo wakimbizi wengi wamepata makazi, ni hapa ambapo wanaojitolea wengi hufika ambao huleta chakula, kuanzia Kherson, hadi miji mingine. Watawa hutunza idadi ya watu ambao wamebaki katika maeneo haya." Kituo hicho kimekuwa kikifanya kazi kwa miaka 19, kikihifadhi watoto wagonjwa kutoka katika familia zilizovunjika, wazee, akina mama wasio na waume na wasio na makazi.
Hebu iwe Noeli ya mwisho wa vita
Mwishoni mwa siku, jiko la supu lilizinduliwa kwa ajili ya maskini ambalo lilikosekana tangu 2009 wakati Wadominika niwalipofungua jiko la kijamii. "Hapa ni mahali pa umuhimu maalum kwa maskini na wakimbizi. Kardinali alielezea kuwa “ Pensheni ni kama dola mia moja, watu hawa hawawezi kumudu chochote, kwa hivyo Wadominikani pamoja na watu wa kujitolea, ambao wengi wao wanatoka Poland, walisababisha kuundwa kwa kantini hii. Papa alinituma kusafiri kilomita elfu 3 ili kushiriki nanyi furaha ya kuzaliwa kwa Mungu, tunatumaini kuwa hii itakuwa Noeli ya mwisho wa vita. Imani na maombi vinaweza kuhamisha milima. Kwa hivyo, ikiwa tunamtumaini Mungu, vita hivi vya kipuuzi vitakwisha,” Alisema Kardinali.
Miujiza ya leo
"Katika nyakati hizi, siku zote ninakumbuka Injili (Mt 14,13-21) wakati wanafunzi walipoogopa walimwendea Yesu na kumwambia kwamba kulikuwa na watu elfu tano wenye njaa ambao hawana chakula na mikate michache tu yaani mkate mmoja na samaki wawili, na Yesu akasema: 'Wapeni chakula.' Kwa njia hiyo “Hii nini”… ina maana sisi. Sisi kama Kanisa, sisi kama waamini, sisi kama watu wa Injili. Na hiki ndicho kinachotokea hapa Fastiv." Msimamizi wa Huduma ya Upendo alikumbusha kuwa kuna ukarimu mkubwa, kwamba kila siku mtu analeta mkate, analeta mchele, analeta pasta, nyama, hadi sasa hakuna kitu kinachokosekana. Hii ndiyo miujiza ya leo,” alihitimisha.