Tafuta

2024.12.25 Kardinali Krajewski akiwa Ukraine aliungana na viongozi wa Kanisa na waamini kusali misa ya Noeli. 2024.12.25 Kardinali Krajewski akiwa Ukraine aliungana na viongozi wa Kanisa na waamini kusali misa ya Noeli. 

Kard.Krajewski huko Ukraine: Kanisa liliungana katika kukabiliana na vurugu za vita

Katika ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo katika nchi inayoteswa na karibu miaka mitatu ya migogoro,aliweza kupeleka furaha kwa watu na kuonesha ukaribu wa Baba Mtakatifu Francisko.

Vatican News.

Noeli ya umwagaji damu nchini Ukraine ambayo, alfajiri ya tarehe 23 Desemba 2024  iliamka chini ya mashambulizi makubwa ya Kirusi. Kama ilivyoripotiwa na Wizara ya Ulinzi ya Moscow, silaha za masafa marefu za usahihi wa hali ya juu na ndege zisizo na rubani vilitumiwa. Lengo kuu la uvamizi ni miundombinu ya nishati ya Ukraine.

Shambulio kubwa la Kharkiv

Hasa, mji wa kaskazini mashariki wa Kharkiv ulilengwa, ambapo watu watatu walijeruhiwa. Meya wa eneo hilo, Ihor Terekhov, aliripoti hii kupitia ujumbe kwenye Telegram.  Kherson pia ilipigwa: kulingana na mamlaka mahalia kulikuwa na mwathirika mmoja. Katika chapisho kwenye mitandao ya kijamii, rais wa Ukrain, Volodymyr Zelensky, alitaja shambulio hilo kuwa  la "ukatili."

Miundombinu ya nishati imeathiriwa

Huzuni kwa kile kilichotokea ilioneshwa kwa vyombo vya habari vya Vatican na Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo ambaye hivi karibuni amekuwa nchini Ukraine kupeleka misaada kutoka kwa Papa Francisko kwa idadi ya watu, wanaosumbuliwa na karibu miaka mitatu ya vita. "Maneno yananishinda. Leo asubuhi saa sita, siku ya Noeli, Kharkiv ilipigwa bomu, robo tatu ya wakazi, kati ya idadi ya watu milioni moja, hawana umeme. Walilipua eneo ambalo chanzo cha nishati kiko. Kuna waliojeruhiwa," alisema.

Shukrani za watu kwa ukaribu wa Papa

Kardinali Krajewski kisha alieleza kwamba aliondoka Kharkiv "saa 4:45usiku, dakika 15 kabla ya amri ya kutotoka nje kwa treni ambayo ilikuwa imefunikwa kidogo, kwa usahihi ili kutoruhusu mwanga kupita, kwa hivyo madirisha yote yalifungwa.” Habari za shambulio hilo zilimfikia muda mfupi baadaye, wakati wa safari. "Ninasikitika, saa chache tu zilizopita nilikuwa pale na kusali na watu ambao pia walishukuru kwa jenereta zilizotolewa na Baba Mtakatifu na waamini wa Roma. Ni muhimu sana: halijoto iko chini ya sufuri na jenereta ni muhimu sana kwa kuokoa maisha na kuruhusu watu kuishi majumbani,"alisema kardinali.

Nguvu ya maombi katika Kanisa lenye umoja

Licha ya giza na kukata tamaa kulikosababishwa na vita, hata hivyo, Kardinali alikazia jambo moja kuwa: “Jinsi ilivyokuwa nzuri kuona Kanisa lililoungana, hatimaye Kanisa lililoungana. Labda hii ni ishara yenye nguvu kwetu sisi pia, kwa sisi sote: kuomba pamoja, kusali pamoja, kuwa na umoja kama Kristo alivyotaka siku zote. Tunapoungana tunakuwa na nguvu sana na hii ilionekana hasa huko Kharkiv. Kanisa lililoungana, Kanisa lililoungana,"alihimisha kusema Kardinali Krajewski.

27 December 2024, 13:57