Kard.Parolin:nchini Syria kunaweza kuwa na mustakabali wa heshima kwa kila mtu
Na Salvatore Cernuzio –Vatican.
Wasiwasi juu ya kile kilichotokea haraka huko Syria, ambapo serikali ilionekana kuwa thabiti ilifutwa. Matumaini ni kwamba yeyote anayechukua mamlaka anaweza kuunda utawala unaoheshimu kila mtu. Hizi ndizo hisia ambazo Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alieleza akitazama hali halisi ya Syria, baada ya kuanguka kwa Rais Assad mikononi mwa waasi na wakati wa kuunda serikali mpya ya mpito. Kardinali akiwa huko Milano katika mkutano huko Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu, ambao uliongozwa na mada ya utatafi wa mazungimzo tarehe 10 Desemba 2024. Tuzo ya Utafiti itatolewa kwa ajili ya Masomo ya Kiarabu-Kiislam”, ambayo itawakilishwa na utafiki Mkubwa wa uliohamasishwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu ya Waislamu Muhammad Al-Issa, iliyokusudiwa kwa watafiti vijana kwa tafiti zinazolenga kuchunguza mada ya utamaduni wa Kiarabu-Kiislam.
Huko Syria kila kitu kilifanyika haraka
"Nafasi nzuri ya kuendelea kujenga madaraj" na ulimwengu wa Kiislamu, alisema Kardinali Parolin akiwa na waandishi wa habari ambao, kando ya tukio hilo, walimuuliza kuhusu mambo ya sasa duniani. Kwanza kabisa misukosuko ya saa 72 zilizopita nchini Syria. "Nadhani sote tuna wasiwasi kuhusu kile kinachotokea nchini Syria pia kwa sababu ya kasi ya matukio haya. Ni vigumu kuelewa kinachoendelea. Inanivutia sana kwamba serikali ambayo ilionekana kuwa na nguvu sana, thabiti sana, imefagiliwa mbali kabisa kwa muda mfupi." Alisema Kardinali.
Utawala wazi ambao unaheshimu kila mtu
Kardinali Parolin alihimiza tahadhari: "Hebu tuone sasa ni matukio gani yanafungua... Labda ni mapema kidogo kutarajia", alisema, huku akisisitiza kwamba "tumekuwa na maonyo ya mapema kuhusu heshima kwa jumuiya za Kikristo, kwa hivyo tunatumaini kuwa kuna inaweza kuwa mustakabali wa heshima kwa kila mtu." Matumaini ni kwamba wale wanaochukua nafasi pia watajaribu kuunda serikali iliyo wazi kwa wote na yenye heshima ya kila mtu." Wakati huo huo,Vatican, linaendelea na kazi yake ya mazungumzo na diplomasia, licha ya kutokuwa na "majukumu rasmi.” Nchini Ukraine, kwa mfano, "hakuna aina ya mazungumzo rasmi ambayo yameanzishwa, lakini tunachukua fursa ya hali zote kutafuta hali zinazotuwezesha kuanzisha mazungumzo na kutatua tatizo kwa maana ya usitishaji vita, kwa maana ya kuachiliwa kwa mateka huko Mashariki ya Kati, kwa maana ya misaada ya kibinadamu nk. Haya yote ni maeneo ambayo tunahamia."
Umuhimu wa mazungumzo
Miongoni mwa vipaumbele, kama kawaida, ni mazungumzo. Na tukio hilo la Mkutano huo ni fursa ya kuimarisha madaraja kati ya tamaduni tofauti za kidini lakini zinazoshiriki maisha ya mwanadamu wa kisasa. Kardinali Parolin alibainisha kuwa: "Ni nafasi inayofaa, kwa nimefurahishwa sana kwamba taasisi kama Chuo Kikuu cha Kikatoliki imeendeleza mpango huu ambao unaturuhusu kuelewana, kuongeza ujuzi wa pamoja na ushirikiano wa pamoja. Ninaamini kwamba leo changamoto ni ile ya kushirikiana pamoja ili kutoa jibu kwa shida na shida nyingi ambazo ulimwengu unajikuta unapitia. Kuna haja ya kurejesha harambee, kuna haja ya kurejesha ushirikiano."
Uteuzi wa kadinali huko Milano
Kardinali Parolin alizungumza katika mkutano huo katika Chuo Kikuu cha Milano pamoja na mkuu wa chuo hicho Bi Elena Beccalli, pia walikuwepo Muhammad Al Issa na Wael Farouq, profesa msaidizi wa lugha ya Kiarabu na fasihi katika chuo kikuu. Asubuhi sana tarehe 10 Desemba 2024 Kardinali aliadhimisha Misa kwa kwa mtazamo matarajio ya Noeli wakati Alasiiri alishirishi uwasilishaji wa kitabu: Kwa uchumi mpya na Gambera Beccalli ambacho kinachunguza mipaka ya dhana ya sasa ya kiuchumi na kupendekeza mtindo mpya kulingana na maadili, uaminifu na ushirikiano. Katika mkutano huo kulikuwa na salamu kutoka kwa Askofu mkuu Mario Delpini wa mji mkuu wa Lombardia. Miongoni mwa wengine, ni Alberto Quadrio Curzio, rais mstaafu wa Chuo Kikuu cha Elimu.