Tafuta

2024.12.13 Tafakari ya Pili ya Majilio katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. 2024.12.13 Tafakari ya Pili ya Majilio katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Katika Majilio tugundue tena imani kwa Mungu na wengine ili kufufua tumaini

Ijumaa tarehe 13 Desemba 2024 katika Ukumbi wa Paulo VI,tafakari ya pili kati ya tatu kuelekea Noeli ilitolewa na mhubiri wa Nyumba ya Kipapa,kuhusu mada ya 'Mlango wa uaminifu'.Chaguo la ujasiri na si matumaini tu,bali imani huweka tumaini hai hata katika majaribu na ni dawa ya ubinafsi.Padre Pasolini alikazia juu ya mfano wa Mtakatifu Yoseph,shuhuda angavu wa ukarimu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika enzi iliyo na mwelekeo wa pamoja kuelekea ubinafsi, tunaweza kuzungumza juu ya uaminifu? Na katika nyakati ngumu za maisha, katika nyakati hizo muhimu ambazo tunaogopa kupoteza kitu muhimu sana, bado tunaweza kuamini kitu au mtu? Haya ni maswali ya msingi yaliyowekwa katikati ya tafakari ya  II ya Majilio ya Padre Roberto Pasolini,(OFMCap) Mfransiskani Kapuchini, mhubiri wa Nyumba  ya Kipapa, iliyopendekezwa kwa Papa na washirika wake wa Curia Romana asubuhi tarehe  13 Desemba 2024 katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican. Mada iliyochaguliwa kwa tafakari hizo tatu ni “Milango ya matumaini. Kuelekea ufunguzi wa Mwaka Mtakatifu kupitia unabii wa Noeli."

Uaminifu, msingi wa mahusiano ya kibinadamu

Baada ya tafakari ya kwanza ya tarehe 6 Disemba 2024 iliyojikita na mada ya  “Mlango wa mshangao”, katika tafakari hii,  Padre Pasolini anatualika kuvuka “mlango wa uaminifu” yaani, mtazamo huo msingi unaounga mkono mahusiano ya kibinadamu, unaostawisha ujasiri wa changamoto za kila siku na kufungua mlango wa imani ili kutazama  siku zijazo. Kuaminiana si matumaini yasiyo na maana, alisisitiza mhubiri, bali ni chaguo la ujasiri linalotokana na maono ya kina ya ukweli, na kuweka matumaini hai hata katika nyakati ngumu.

Mfalme wa Yuda, Ahazi

Kama ushuhuda huo, Padre Pasolini alitaja watu watatu: mfalme wa Yuda Ahazi, akida wa Kirumi asiyejulikana na Mtakatifu Yoseph. Wa kwanza ni mfalme ambaye, wakati wa vita vya Siria na Efraimu, hakumtumaini Bwana na, badala ya kubaki imara katika Yerusalemu kama alivyooneshwa na nabii Isaya, alipendelea kushirikiana na Ashuru, hata hivyo akaishia kuwa kibaraka. Ahazi, kimsingi, hakuamini katika majaliwa ya Mungu, lakini licha ya hilo, Mungu hakuzuia mtazamo wake kutoka kwake, kinyume chake: wakati wa kutoaminiana kwa mfalme ulifungua kwa unabii wa Emmanuel kuwa: "tazama Bikira atachukua mimba na atamzaa mwana ambaye atamwita Imanueli” (Isaya 7:9).

Mtazamo wa Mungu unaturudisha njiani

Uaminifu huu ambao Mungu anabaki kuwa karibu nasi hata tunapojionesha kuwa hatutegemeki, alifafanua Padre Mkapuchin, kwamba huenda zaidi ya matumaini rahisi, kwa sababu Bwana anasadiki kwamba sauti yake ni "kama mvua na theluji" ambayo haishuki kutoka mbinguni bila kuleta matokeo duniani. Si hivyo tu: kuwa Upendo tangu mwanzo na kuwa ametuumba huru, Mungu anasadikishwa kwamba uaminifu daima ni mtazamo wa kupendelewa na kudhaniwa, kwa sababu "ni imani pekee inayokomboa." Na ni mtazamo wake hasa kwamba, wakati wa majaribu na kukata tamaa, huturuhusu kushinda magumu na kurudi njiani. Padre Pasolini aliongeza kusema: "Mungu anaheshimu uhuru wetu na anafurahi tunapoutumia kufanana naye. Kwa hiyo “heshimu uhuru huu hata tunapoamua kujifungia ndani na kwa ubinafsi.” Hata hivyo, tukigeuka kutoka kwenye mtazamo wa macho yake, Mungu hawezi kugeuza macho yake kutoka kwetu. Anaendelea kututambua kama watoto wapendwa, akionesha imani katika uwezo wetu wa kurudi Kwake na kwetu sisi wenyewe."

Akida wa Kirumi

Mtu wa pili aliyetajwa na Padre Pasolini ni akida asiyejulikana wa jeshi la Kirumi aliyeelezwa katika Injili ya Luka kwa hiyo: “Licha ya kuwa mpagani, mtu huyu anaamua kumwamini Yesu na kumwomba amponye mtumishi wake mgonjwa. Akizingatia maisha na mahitaji ya wengine, akida pia alijaribu kutomweka Mwokozi katika shida, kumzuia asiingie nyumbani, akijua kwamba Myahudi mwangalifu kama Yeye angejitia unajisi kwa kuingia katika nyumba ya mpagani. Kwa hakika, alizungumza na Yesu kwa “maneno ya ajabu” kiasi kwamba baadaye yaliingizwa katika liturujia ya Kikristo ambayo alisema: “Ee Bwana, mimi sistahili kushiriki katika meza yako, lakini sema neno tu, nami nitapona." Maneno haya, alieleza mhubiri, kwamba yanaonesha imani kuu katika Bwana Yesu na kuwa kwake Neno la hakika la wokovu kutoka kwa Mungu.

Uhusiano kati ya imani katika Mungu na kuwajali wengine

Padri Mkapuchini pia aliakisi kipengele kingine: akida wa Kirumi alionesha kwamba imani katika Mungu na uangalifu kwa wengine "haviwezi kutenganishwa" au "sio sawa." Hakika: "Imani yetu kwa Mungu ni ya kweli kwa kiwango ambacho tunaamini kwamba uaminifu na fadhili hazizidi kamwe katika mahusiano tunayoishi." Si suala la kuonesha urafiki kidogo tu, bali ni “kila mara kutafuta wakati na njia ya kujiweka katika viatu vya mtu mwingine”, katika kumfuata Bwana ambaye hutufanya tusijisikie vibaya bali vizuri, “hata tunapoingia dhambini "kwa sababu "ni upendo unaokaribia mwingine, nuru inayoangaza daima, hata gizani".

Kuwa waamini kunamaanisha kupanua ubinadamu wetu

Jemadari anayeamini kila kitu na kila mtu, hata katika hali ambayo hakuna upungufu wa shida, ni udhihirisho wa ubinadamu "wazi, wazi, wenye afya, unaoonekana," ni "ukumbusho wenye nguvu kwetu na kwa njia zetu za imani "ambapo mara nyingi tunajikuta tumefungwa, kutokuwa na imani na ubinafsi." Padre Pasolini alisisitiza tena kuwa, “Tukiwa waamini, maana yake ni kupanua na kuongeza ubinadamu na kupendwa kwetu, vinginevyo tunajidanganya katika kukimbilia kwenye uvuli wa Mungu ili tupewe mamlaka ya kuwa na imani kidogo"kwake, kwa wengine na ndani yetu wenyewe.”

Mtakatifu Yoseph, sura ya uaminifu

Padre Pasolini kadhalika alijikita  kufafanua sura ya  Mtakatifu Yosefu  ambaye Papa Francisko aliweka hata Waraka wa Kitume kwa ajili yake uitwao Patris Corde, yaani Moyo wa Baba,  akimfafanua kama "sanaa ya uaminifu" kwani yuko tayari "kujifafanua mwenyewe sio kutoka kwake mwenyewe, bali pia kutoka katika  hali halisi." Sio kwa bahati mbaya kwamba katika jamii ambapo wanawake walifafanuliwa na wanaume, kwa hiyo Yoseph aliitwa "mume wa Mariamu." Ijapokuwa alichanganyikiwa na ujauzito usiofikiriwa wa Maria, yeye hakujibu kwa hasira, yeye hakumkimbia, lakini alikaa na kubaki kwa upole karibu na wadhaifu zaidi kwa mantiki hiyo: Bikira na mtoto. Yoseph hakuomba au kuchukua haki mikononi mwake, Padre Pasolini alisisitiza tena, lakini alijirekebisha kukubali hali ambayo alijikuta. Mbali na mtazamo wowote wa kutojali au kushindwa, yeye ni mfano wa kuwa mstari wa mbele wa ujasiri.”

Kuzidisha katika Upendo

Kumwamini Bwana, kama baba mlezi wa Yesu aliingiza jambo muhimu ambalo ni muhimu kupenda zaidi kuliko vile alivyofikiria. Funzo halali kwetu pia ni pale  tunapojikuta katika hali ngumu, tukiwa na hofu au hasira, hatuachi kufikiria, lakini tunajaribu tu kuliepuka tatizo hilo, tukiwa na woga kwani tuna "kutazama ukweli usoni, kwa sababu tusingependa kulazimishwa kutambua ndani yake wito wa  kujihusisha zaidi na maisha ya wengine." Kwa hiyo tunapopigwa kona, hapo unaelekea kutaka kubadilisha hali,"Padre Pasolini alisisitiza.

Nuru ya Mungu huangaza hata katika nyakati za giza

Hata hivyo, alikumbuka Padre Pasolini, kuwa “tendo la haki kabisa halimaanishi kamwe kurekebisha yale yanayotuudhi au tusiyopenda, bali ni kujaribu kujibadilisha, kurekebisha matazamio yetu kulingana na mahitaji au magumu ya wale wanaokaa karibu nayo." Kama Mtakatifu Yosefu, kwa hivyo, katika vifungu muhimu na vya giza zaidi vya maisha yetu, tunapoonekana kupoteza kitu muhimu sana, Mungu huwasha taa kila wakati, akichochea ubunifu wetu na kutufundisha tusikate tamaa, bali tuishi ndani yake lakini tofauti.

Padre Pasolini kisha alisisitiza jambo lingine zaidi la  utayari uliojumuishwa na Mtakatifu Yosefu wa kukaribisha ukweli si mwingine ila uchu wa kimwili, unaoeleweka si kwa maana ya kimwili bali, kwa maana pana zaidi, kama kujiepusha na ubinafsi na uwezo wa kubaki katika uhusiano na kila mmoja na mwingine  kuheshimu midundo na nyakati zake,kwa kubadilishana kujali na umakini. Katika enzi iliyo na umakini mkubwa kwetu, tukiepuka sadaka zisizo na maana na zenye madhara za ubinadamu wetu, hatari ya pamoja inaweza kuwa ile ya kuteleza katika ubinafsi ambapo nyingine inachukua nafasi ya pili. Kwa mujibu wa Padre Pasolini alisema “Hii inaelezea ni kwa nini njia nyingi za upendo na wa wakfu hukatizwa kwa urahisi." Walakini, hasa katika wakati huu wa kihistoria, sote tunahisi shauku kubwa ya "mahusiano ya kweli, yaliyosimikwa katika moyo huru, kama ule wa Yoseph", ambao ni "shuhuda wa mwangaza wa kujitoa bure.”

Kukumbatia ukweli wa kumtumaini Bwana

Katika wakati wa Majilio, mhubiri Pasolini alihitimisha, kwa  mwaliko ambao ni kuvuka "mlango wa uaminifu" uliooneshwa na manabii, akida wa Kirumi na Mtakatifu Yosefu, kwa sababu ni  kuelekeza macho yetu tu kwa Mungu na kugundua tena imani ndani yake, ndani yetu na ndani yetu wengine ndipo tutaweza kuona kweli mema yanayotuzunguka na kukumbatia ukweli hata wakati ni wasiwasi na karibu kuchukiza, ambapo tusijaribu kutafuta haki, bali kurekebisha mioyo yetu, kuelewa jinsi ya ukweli wenyewe unaweza kuwa nafasi ya furaha, kwa sababu ni mahali ambapo Bwana amechagua kuwa pamoja nasi, milele."

PADRE PASOLINI
14 December 2024, 13:39