Papa akutana na Orbán,Waziri Mkuu wa Hungaria
Vatican News
Ilichukua dakika thelathini na tano mkutano wao kwa kuhitimisha na kubadilishana zawadi, pamoja na ile ya ramani ya karne ya 18 ya Nchi Takatifu, na mazungumzo ya faragha yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2024 kati ya Papa Francisko na Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Hungaria. Mara ya mwisho walikutano mnamo 2022. Kwa mujibu wa taarifa kutoka msemaji wa Vyombo vya habari ilibainisha kuwa "Waziri Mkuu wa Hungaria yuko mjini Roma ambapo kukutana pia na Waziri Mkuu mwenzake wa Italia Bi Giorgia Meloni na ambaye alipokelewa asubuhi katika ukumbi mdogo wa Paulo wa VI kabla ya Katekesi ya Baba Mtakatifu na ambapo aliwasili kwa miguu, akisalimiana na waliohudhuria katekesi ya Papa."
Mazungumoz katika Sekretarieti ya Vatican
Akiwa na msafara wake - akiwemo mkewe Aniko Levai na balozi wa Vatican mjini Vatican Eduard Habsburg-Lothringen - Orbán alipokelewa katika ukumbi mdogo wa Ukumbi wa Paulo VI, kabla ya Papa kuhamia kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, mahali ambapo alisubiriwa kwa ajili ya katekesi yake. Baadaye, kiongozi wa Hungaria, nchi iliyotwaa urais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU), mwezi Julai uliyopita, alikutana na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, akifuatana na Monsinyo Mirosław Wachowski, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa na Ushirikiano wa kimataifa.
Wakati wa mkutano huo,kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Habari ya Vatican ni kwamba "mahusiano thabiti na yenye matunda yalisisitizwa na shukrani kubwa ilioneshwa kwa kujitolea kwa Kanisa Katoliki katika kukuza maendeleo na ustawi wa jamii ya Hungaria.” Zaidi ya hayo, “lengo lilikuwa hasa katika vita vya Ukraine, kwa kuzingatia matokeo yake ya kibinadamu na jitihada za kukuza amani.” Pia mada zilizochunguzwa ni zile za maslahi ya kawaida, kama vile urais wa Hungaria wa Baraza la Umoja wa Ulaya, jukumu kuu la familia na ulinzi wa vizazi vijana.”