Tafuta

Askofu Laurent Birfuoré Dabiré, wa Jimbo la Dori ametueuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Bobo-Dioulasso (Burkina Faso). Askofu Laurent Birfuoré Dabiré, wa Jimbo la Dori ametueuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Bobo-Dioulasso (Burkina Faso). 

Papa amemteua Askofu Laurent Birfuoré Dabiré kuwa Askofu Mkuu wa Bobo-Dioulasso,Burkina Faso

Baada ya kung’atuka kwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dioulasso(Burkina Faso)kufuatia na umri,Baba Mtakatifu tarehe 18 Desemba 2024 amemteua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu hilo hilo,Mwashamu Laurent Birfuoré Dabiré,ambaye hadi uteuzi alikuwa ni Askofu wa Jimbo la Dori.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 18 Desemba 2024, amekubali maombi ya kung’atuka katika shughuli za kichungaji za Jimbo Kuu Katoliki la Bobo-Dioulasso nchini Burkina Faso lililowakilishwa na Askofu Mkuu Paul Yembuado Ouédraogo.  Na wakati huo huo Baba Mtakatifu  akamteua kuwa  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu hilo, Mwashamu Laurent Birfuoré Dabiré  ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Askofu wa  Jimbo la Dori, na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Burkina Faso na Niger.

Wasifu

Askofu Dabire alizaliwa tarehe 17 Septemba 1965 huko Dissin, Jimbo la  Diébougou. Alipewa Daraja la Upadre mnamo tarehe 29 Desemba 1995 kwa ajili ya Jimbo la Diébougou.

Ameshikilia nyadhifa mbali mbali na kufanya masomo zaidi kama: Profesa katika Seminari Ndogo ya Mtakatifu Tarcisius ya Diébougou (1996-1998); Shahada ya Uzamivu katika Utroque Iure huko Roma (1998-2005); na Padre wa Mahakama  ya Kanisa pamoja na Kansela (tangu 2005); Afisa wa Mahakama ya Kikanisa ya Jimbo kuu la Bobo Dioulasso (tangu 2006); Profesa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji (2007-2008); Profesa wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Bamako, Mali (tangu 2011). Tarehe 31 Januari 2013 aliteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki  la Dori, na kuwekwa wakfu wa kiaskofu mnamo tarehe 4 Mei 2013. Tangu 2019, amekuwa Rais wa Baraza la Maaskofu la Burkina Faso na Niger.

18 December 2024, 16:04