2024.12.05 Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Caritas Jimbo la Toledo. 2024.12.05 Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Caritas Jimbo la Toledo.  (Vatican Media)

Papa kwa Caritas Jimbo la Toledo:muwe stadi wa hekima inayohitajika sana ulimwenguni!

Katika Mkutano na Caritas ya Toledo,Baba Mtakatifu alikumbusha kanuni za upendo na haki ili kuamsha dhamiri ya kidugu katika jamii.Utumishi kwa wengine si hisia za kiraia tu,bali ni kazi ya ufundi kuleta nuru ya Injili kwa wale wasiopata kuungwa mkono na kukubalika.Papa amesisitiza kuwa upendo ni injini ya mabadiliko ya kijamii na siyo uhisani tu.Ujinga unavutiwa.Unauza na kununua ujinga na bei sio ofa na kufilisi ni bei za msimu na ghali.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alikutana mjini Vatican, tarehe 5 Desemba 2024 na takriban washiriki mia moja wa Caritas  Jimbo la Toledo, nchini Hispania, katika Ukumbi wa Uchaguzi mjini Vatican. Tukio la mkutano  wao ni katika kumbukizi ya miaka 60 ya shirika la kutoa misaada, lililoanzishwa mnamo tarehe 2 Juni 1964. Katika hotuba yake aliwakaribisha na kuungana nao  katika shukrani zao kwa miaka sitini ya huduma ya upendo  katika Kanisa la Toledo. Ahadi ambayo, kama alivyoweza kusisitiza  kwamba inakwenda mbali zaidi ya mema madhubuti yanayoweza kufanywa kwa mtu, kukubali changamoto ya kuwa kichochezi cha mabadiliko katika jamii kwa kueneza moyo wa upendo na haki,  ili kuamsha dhamiri ya kidugu zaidi kwa watu wote wenye mapenzi mema. “Yaani udugu wetu wakati fulani unalala au haukui. Na dhamiri ya kidugu inapochochewa ni kuiamsha tena na kuifanya ikue."

Papa na Wajumbe wa Caritas Toledo nchini Hispania
Papa na Wajumbe wa Caritas Toledo nchini Hispania

Kwa kufanya hivyo, Papa aliongeza, wao wanakuwa siyo  kielelezo cha ustaarabu tu  na uhisani, bali  pia wanakuwa vyombo vya uinjilishaji, kupitia lugha ya ulimwengu ya kazi za upendo. "Inashangaza, kazi za upendo mara kadhaa hazihitaji mfasiri, hakuna kamusi ya kutafsiri, lugha ya ulimwengu wote, lugha ya ulimwengu ya kazi za upendo kila mtu anaielewa." Kwa sababu hiyo ni lugha inayoeleweka kwa wote, iliyoandikwa kwa ushuhuda na juhudi za mawakala wote wa Caritas, waliokabidhiwa kwa Yesu Kristo na Injili yake, Papa Francisko alisisitiza. Ni lengo la juu bila shaka, ambalo linafikiwa kupitia kazi ya ufundi ya kila mmoja wa wale wanaohusika na hatua ya usaidizi wa kijamii, kuanzia malezi ya kibinadamu na ya kiroho ambayo inawaruhusu kushughulikia kwa uthabiti shida za kijamii zinazobadilika kila wakati, kwa kuzingatia hali ya kijamii na mafundisho ya Kanisa. Bila kusahau moyo wa ushirikiano na sinodi pamoja na ukweli mwingi wa kichungaji unaounda Kanisa zima la kijimbo.

Papa na Jimbo la Toledo
Papa na Jimbo la Toledo

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko aliwatia moyo wasonge mbele katika juhudi hiyo, wakijifunza daima, kutoka kwa Bwana, katika kitabu hai cha sala na usomaji wa Neno lake, katika kitabu hai cha uzoefu wa sakramenti na kusikiliza kwa makini sauti ya wachungaji wake na kwa uwepo wake katika Ekaristi na katika wale wanaowahudumia. Baba Mtakatifu kwa kuhitimisha alisema: “Kitu kimoja ninachowaomba ni kwamba muwe walimu wa hekima, wa hekima hiyo ambayo ulimwengu unahitaji sana. Ujinga unashangaza. Unauza na kununua ujinga, na bei sio ofa, ya kufilisi, ni bei za msimu, bei ghali. Na tafadhali, nawaomba mniombee. Kwa Yesu, ambaye kwa  kila mtu hasiye na pa kulaza kichwa chake, awabariki, na Bikira Mtakatifu, katika wale ambao hawajapata mtu wa kuwakaribisha, daima awasindikize.

05 December 2024, 12:29