Kwa sababu ya baridi na mafua,Papa ataongoza sala ya Malaika wa Bwana katika nyumba ya Mt.Marta
Vatican News.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, Jumamosi tarehe 21 Desemba 2024, alifahamisha juu ya mawasiliano yaliyotolewa alasiri kupitia chaneli ya Telegram kuwa: “ Kutokana na baridi kali, pamoja na dalili za baridi zilizojidhihirisha katika siku za hivi karibuni, Dominika tarehe 22 Desemba 2024, Papa Francisko ataongoza sala ya Malaika wa Bwana akiwa katika Kikanisa cha Matakatifu Marta, pia kwa kuzingatia shughuli zijazo ja Juma.”
Hata hivyo Yeye mwenyewe, Ijumaa tarehe 20 Desemba 2024 akikutana na Shirikisho la Mchezo wa Mafute nchini Italia, alisema alivyokuwa na "baridi sana". Na si mara ya kwanza kwa Baba Mtakatifu anafanya tafakari na kusali sala Ya Malaika wa Bwana kutokea katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta mjini Vatican mahali ambapo alichagua kuwa makazi yake.
Inakumbwa hata mnamo Desemba 2023, kutokana na ugonjwa aliokuwa nao ambao ulimlazimu kubadili ratiba yake na kuacha ziara ya kwenda Dubai kwa ajili ya Mkutano kuhusu Mazingira wa au Cop28, alishiriki akiwa Ndani ya kikanisa hicho na zaidi hatuwezi kusahau Misa nyingi za asubuhi zilizoongozwa na Papa –akiwa ndani ya kikanisa hicho.
Tunawakumbusha kwamba, sala zitarushwa moja kwa moja(Mbashara) kwenye televisheni na kwenye skrini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,mjini Vatican pamoja na kurushwa kwenye tovuti za Vatican News.