Tafuta

2024.12.04 Askofu Mkuu Edgar Peña Parra Katika Basiliaka ya Matuamini ya Macarena nchini Hispania. 2024.12.04 Askofu Mkuu Edgar Peña Parra Katika Basiliaka ya Matuamini ya Macarena nchini Hispania.  

Peña Parra:sisi ni mashuhuda wa matumaini dhidi ya kutojali kwa ulimwengu!

Askofu mkuu Parra,Katibu Msaidizi wa Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican aliweka Waridi la Dhahabu lililotolewa na Papa Francisko kwa picha ya Maria katika Basilika ya Matumaini ya Macarena huko Seville nchini Hispania.Katika mahubiri alisema:“tunaangalia na kutenda kwa upendo kwa maskini,wazee,wahamiaji,wagonjwa na waathiriwa wote wa utamaduni wa kutupa.”

Vatican News

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi  wa  Masuala ya Sekretarieti ya Vatican, tarehe 3 Desemba 2024, wakati wa ibada ya misa  aliweka Waridi la Dhahabu lililotolewa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya Picha ya Bikira Maria katika Basilika ya Matumaini huko  Macarena. Ni katika muktadha wa kumwakilisha Baba Mtakatifu kama Mjumbe maalum katika maadhimisho ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Kimataifa la 'Udugu na Ucha Mungu wa Watu' tarehe 4 Desemba 2024 huko Seville nchini Hispania. Katika Tafakari, yake akiwa chini ya picha iliyobarikiwa ya Mtakatifu Maria wa matumaini ya Macarena , ilianza kutoka kwa kipindi cha harusi ya Kana huko Galilaya,  ambayo ni historia ya Mama anayeomba yaani Mama Maria, kwa kujali mahitaji ya wanandoa na mahitaji ya watoto wa kila zama. Nia ni kuchukua jukumu la kuishi kama Kanisa, kuzingatia mahitaji ya wengine, kwa mtindo wa Bikira.

Askofu Mkuu Edigar  Parra katika Basilika ya Mama Maria wa Matumaini  Macarena
Askofu Mkuu Edigar Parra katika Basilika ya Mama Maria wa Matumaini Macarena

Ni katia hilo ambapo Askofu Mkuu Peña Parra aliwaeleza kuwa “Muwe mashahuda wa matumaini ili, kwa kufuata mfano wa Maria, ibada isibaki ya kijuu juu bali ijibu kutojali kwa ulimwengu kwa njia ya maisha ya unyenyekevu, huduma na ushirika.” Mtindo unaojulikana, kwanza kabisa, na uwezo wa kuangalia kwa upendo na umakini katika hali halisi inayomzunguka: Mama wa Yesu hajafungwa ndani yake mwenyewe au kwa ustawi wake au masilahi yake na macho yake yanaelekezwa kila wakati, kuelekea utimilifu wa mapenzi ya Mungu na kwa wengine.” Alisisitiza. Huko Cana, Maria ndiye  alikuwa wa kwanza kugundua hitaji la familia ya mwenyeji mchanga: "Hawana divai". Mtazamo huu unatusukuma kuchunguza utayari wa kuona "mahitaji ya kaka na dada zetu, hasa maskini na wahitaji zaidi, na pia ya wale wanaoteseka kwa njia ya kimya", alisisitiza askofu mkuu.

Basilika ya Maria wa Macarena
Basilika ya Maria wa Macarena

Kwa hivyo, katika jamii ambayo mara nyingi ina alama ya kutojali, mfano wa Maria unaalika usikivu unaoweza kutambua kile kinacho kosekana katika maisha ya wale wanaotuzunguka: ukosefu wa tumaini, upendo, haki, ukosefu wa kile muhimu kwa maisha ya heshima. Kuangalia ukosefu wa divai huko Cana, Maria anaonesha jinsi ya kutenda katika uso wa umaskini, mateso na dhuluma ambayo yanaendelea katika jamii yetu. Leo ukosefu wa divai unaweza kujidhihirisha kwa njia nyingi kama vile: katika ukosefu wa fursa kwa wale wanaoishi katika umaskini uliokithiri, katika upweke wa wazee waliotelekezwa, katika uchungu wa wale ambao wamepoteza imani na matumaini, katika mateso ya wahamiaji, wagonjwa na wale wote wanaokabiliwa na kutengwa na kubaguliwa.

Askofu Mkuu Parra alihutubia pia katika Kongamano
Askofu Mkuu Parra alihutubia pia katika Kongamano

Kama Maria, akitenda kwa unyenyekevu na huruma katika mtazamo wa huduma yake unawezekana kuwa wapatanishi wa neema ya kimungu, tukileta mahitaji ya jirani zetu kwa Yesu kupitia mtu wa kwanza na na vitendo halisi; ambayo ina maana, kwamba imani yetu inapaswa kutafsiri katika kazi za huduma na upendo, hasa kwa wale wanaohitaji zaidi. Utoaji wa Waridi wa Dhahabu, ishara ya upendo na kujitolea kwa Papa kwa Bikira Maria, kwa hiyo unajumuisha wito wa kuishi imani kwa hisia ya kina ya ukasisi, na kutekeleza matumaini ambayo siyo udanganyifu au matumaini ya juu juu, lakini badala yake tumaini lenye mizizi ya imani katika Mungu. Tumaini tendaji ambalo linaonekana pale Cana Maria anapowaambia watumishi: "Fanyeni chochote atakachowaambia akionesha imani kamili kwamba Yesu atatenda, hata kama hajui jinsi gani". Mtazamo huu, alisema mjumbe maalum wa Papa Francisko, ni onesho la tumaini ambalo halisimami tuli, lakini linaanza, likiwachochea wengine kuchukua hatua. Kadhalika, alihitimisha kwamba, Kanisa zima linaalikwa kufanya kazi kwa pamoja ili kuruhusu huruma ya Mungu kubadilisha ‘maji’ ya mahitaji ya mwanadamu kuwa ‘divai’ ya matumaini.

05 December 2024, 11:55