Jubilei 2025:ibada ya kutambuliwa Mlango Mtakatifu katika Basilika ya Mtakatifu Petro
Alessandro De Carolis na Angella Rwezaula - Vatican
Ilikuwa sherehe fupi ya kusisimua ambayo iliyofanyika jioni ya tarehe 2 Desemba 2024, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican ambayo iliwasilisha kwa nguvu zaidi katika kukaribia kile kitakachotokea katika mkesha wa Noeli. Kwa njia hiyo, ilikuwa Sala nzito na kisha kuona nyundo na patasi vya kugonga ili kufungua pengo katika ukuta na kurejesha sanduku ambalo, pamoja na mambo mengine, kumehifadhiwa funguo katika sanduku ambapo mnamo tarehe 24 Desemba 202424 katika Mkesha wa Noeli itamruhusu Papa Francisko kufungua Mlango Mtakatifu na kuanza rasimi Jubilei.
Sherehe hiyo
La recognitio yaani Utambuzi, ndilo jina la Kilatini la ibada hiyo, iliyofanywa ili kuhakikisha kwamba Mlango Mtakatifu uliofungwa wakati wa Jubilei ya mwisho (2016) ni mzima, na sasa ni tayari kufunguliwa tena kwa Mwaka Mtakatifu mwingine. Ibada hiyo iliongozwa usiku kwa maombi na Kardinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kisha ilionekana "mawe juu ya mawe" yakibomolewa katika ukuta unaoziba Mlango Mtakatifu kutokea sehemu ya ndani ya Basilika na kutoa sanduku la chuma lililokuwa limezungushwa ndani ya ukuta mnamo tarehe 20 Novemba 2016, katika siku ile ya kufunga Jubilei ya mwisho ya Huruma ya Mungu. Kardinali Gambetti aliongoza msafara huo, huku wakiimba litania za watakatifu, hadi kwenye Altare ya Maungamo, ambapo walisimama kwa muda wa sala, kisha wakafika kwenye Ukumbi, ambapo sanduku la chuma lililotolewa kwenye Mlango Mtakatifu uliokuwa wazi.
Yaliyomo kwenye sanduku
Mbali na ufunguo, ndani ya sanduku hilo lilileta mwanga wa mipini ya Mlango Mtakatifu, ngozi ya hati iliyothibitisha kufungwa kwake, matofali manne ya dhahabu na baadhi ya medali zikiwemo za Papa Francisko Benedikto XVI na Yohane Paulo II. Maaskofu mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, na Diego Ravelli, mkuu wa maadhimisho ya kiliturujia ya Kipapa, ambao walichukua hati na malengo ya utambuzi, ambayo yataletwa kwa Baba Mtakatifu Francisko.
Utambuzi katika mabasilika mengine ya kipapa
Alasiri hiyo sherehe hiyokama hiyo ilifanyika katika Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Yohane huko Laterano. Ibada ya "recognitio" itafanyika pia tarehe 5 Desemba 2024 huko Mtakatifu Paolo Nje ya Ukutana na tarehe 6 Desemba 2024 huko Mtakatifu Maria Mkuu.