Papa Francisko akutana na Rais wa Slovakia
Vatican News
Mazungumzo ya faragha yalichukua muda wa dakika 25 kati ya Baba Mtakatifu Francisko na Rais wa Jamhuri ya Slovakia, Bwana Peter Pellegrini, aliyepokelewa asubuhi ya Jumatatu tarehe 9 Desemba 2024, katika Jumba la kitume mjini Vatican. Baadaye, Mkuu wa Nchi hiyo ya Slovakia alikutana na Kardinali, Pietro Parolin, Katibu wa Vatican akiambatana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
Katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imearifu kuwa: “Wakati wa mkutano wa ukarimu katika Sekretarieti ya Vatican marejeo yalifanywa kwa uhusiano thabiti wa nchi mbili, ikisisitiza mchango wa Kanisa katika neema ya jamii ya Slovakia.” Hatimaye, “kuakisi muktadha wa kimataifa, kwa kuzingatia hasa migogoro ya Ukraine na Mashariki ya Kati.”
Kubadilishana kwa zawadi
Mwishoni mwa mazungumzo ya faragha hata hivyo kulikuwa na ubadilishanaji wa zawadi za kiutamaduni, ambapo kutoka kwa Baba Mtakatifu alitoa zawadi ya kazi ya shaba yenye kauli mbiu:"Upendo wa Kijamii", inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na kuandikwa "Usaidizi wa Upendo" Pamoja na hili, hati za upapa, Ujumbe wa Amani wa mwaka 2024, kitabu cha Statio Orbis cha (Njia ya Msalaba) ya tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Wakati huo huo Rais wa Slovakia alijibu kwa kazi ya pande tatu iliyoundwa na msanii wa Kislovakia, Juraj Králik.