Vatican:Mada ya matumaini ndiyo tafakari ya Mafungo ya kipindi cha Majilio 2024
Vatican News
"Milango ya matumaini. Kuelekea ufunguzi wa Mwaka Mtakatifu kupitia unabii wa Noeli,” ndiyo mada ya mahubiri ya Ijumaa tatu katika kipindi cha Majilio yatakayofanyika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, mbele ya Baba Mtakatifu na kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2024 na mhubiri mpya wa Nyumba ya Kipapa aliyeteuliwa hivi karibuni mnamo tarehe 9 Novemba 2024, Padre Mapuchini Roberto Pasolini(OFMCap). Katika Ukumbi huo utawaona washiriki katika Ijumaa hizo tatu kabla ya Noeli tarehe 6, 13 na 20 Desemba 2024 saa 3.00 kamili asubuhi majira ya Roma. Tafakari hizo zinapendekezwa kwa Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu, na walei wa familia ya kipapa, pia kwa wafanyakazi wa Curia Romana, Wenyeviti wa Mabaraza ya Kipapa na Vicarieti ya Roma kwa ujumbla pamoja na wakuu na wasimamizi wa Mashirika ya Kitawa na wale wa Kikanisa cha Kipapa.
Milango ya mshangao, ya uaminifu, ya udogo
"Mwaka huu katika kipindi cha Majilio sio tu kwamba unatutayarisha kwa ajili ya Noeli, lakini pia unatusindikiza kuelekea Jubile ijayo" kama alivyoandika Padre Pasolini katika mwaliko kwa Nyumba ya Kipapa katika Ijumaa hizo za kutafakari huku akiongeza kuwa: “kipindi hiki cha kiliturujia ni fursa ya neema ya kufanya upya uzoefu hai wa upendo wa Mungu, unaoamsha moyoni tumaini hakika la wokovu katika Kristo, kama Papa alivyoandika katika Spes non Confundit ambayoni hati ya kutangaza Mwaka Mtakatifu wa 2025.”
Padre Pasolini anaandika kuwa "Sauti za manabii, zilizopo na zenye kusisitiza katika kipindi hiki cha kiliturujia, zinatuhimiza kwa nguvu tusipoteze mwelekeo wa njia kuelekea Ufalme wa Mungu" kwa sababu manabii wanatualika kusikiliza sauti hizi "kutambua kile ambacho katika milango ni wale ambao hututambulisha kwa fumbo la ubinadamu wetu kwa matumaini mapya." Kwa mujibu wa mhubiri wa Nyumba ya kipapa anaeleza kuwa Milango hii ni ile ya "mshangao, kuweza kustaajabia mbegu za Injili zilizopo ulimwenguni na katika historia ya uaminifu, kutembea na wengine kwa heshima na uwazi wa moyo, na hatimaye ile ya udogo, ili tusiwe na hofu ya kuwa sisi wenyewe."
Hatua ya mabadiliko ya ndani
Katika kukaribia Mwaka Mtakatifu, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa anapendekeza tena maneno yaliyotamkwa na Paulo VI katika ufunguzi wa Jubilei ya 1975 kuwa: "Sherehe ya Jubilei, pamoja na nidhamu yake ya kiroho iliyo rahisi lakini ya kina, na kwa ufunguzi wa mfano wa milango yake ya huruma na msamaha, inataka kuashiria hatua ya mabadiliko ya ndani, hatua ya ujasiri ya ukweli wa maadili (...) na hatua ya uongofu wa moyo.” Hayo ni maneno yanayotuhimiza kutafakari maana ya Mwaka wa Neema na jinsi ya kuuishi.