2024.12.06 Tafakari ya I ya Majilio kwa uwepo wa Papa. 2024.12.06 Tafakari ya I ya Majilio kwa uwepo wa Papa.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Vatican,Tafakari I ya kipindi cha Majilio:Tufungue mioyo kwa mshangao wa mapya ya Mungu

Katika Ukumbi wa Paulo VI,Ijumaa tarehe 6 Desemba 2024 imefanyika tafakari ya I kati ya 3 kuelekea Noeli na Mhubiri mpya wa Nyumba ya Kipapa,Padre Pasolini(OFMCap)kuhusu mada ‘Mlango wa Mshangao.’Kusikiliza sauti za manabii,mfano wa Maria na Elizabeti na kutambua mbegu hizo za Injili ambazo tayari zipo katika uhalisia zinaleta matumaini katika Ulimwengu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika tafakari ya kwanza ya Majilio kutoka kwa Padre Roberto Pasolini,Mfansiscan Mkapuchini, ambaye ni  Mhubiri mpya wa Nyumba ya Kipapa  alipendekeza kwa Papa na washirika wake wa Curia Romana  asubuhi tarehe 6 Desemba 2024 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican moja ya   Mada iliyochaguliwa kwa tafakari hizo tatu ni “Milango ya matumaini. Kuelekea ufunguzi wa Mwaka Mtakatifu kupitia unabii wa Noeli. Padre alisema kuwa “Kushangazwa na upya wa Mungu, kwa fumbo la Umwilisho ni mwendo wa kwanza wa moyo kuamshwa tena ili kuanza kuelekea Kuzaliwa kwa Bwana na kuuvuka mlango wa Jubilei kwa matumaini changamfu. Mshangao kama ule wa Maria, baada ya tangazo la Malaika Gabrieli, ambaye alijiruhusu kuvutiwa na uasilia uliokithiri na mpango wa Mungu na alitaka kuwa mshiriki huru na mwenye ufahamu ndani yake. Ili kufanya hivyo, hata hivyo, ni lazima kwanza tulegeze ugumu wa moyo, tukisema hapana'kwa kila kitu kinachohatarisha kutufunga na kutulemea kama vile: woga, kujiuzulu, wasiwasi.” Ni kwa njia hiyo alisema kwamba tutaweza kutazama kila kitu kwa macho mapya, tukitambua mbegu hizo za Injili ambazo tayari zipo katika uhalisia, tayari kuleta tumaini la Mungu ulimwenguni.

Tafakari ya I ya Majilio
Tafakari ya I ya Majilio

Baada ya maneno ya dhati ya shukrani kwa mtangulizi wake, Padre Raniero Cantalmessa, mhubiri  wa furaha na nuru ya  Injili kwa ajili ya Nyumba ya Kipapa ambaye kwa miaka 44, Padre Pasolini alitualika kuufungua Mlango wa Mshangao, ambayo kwa hakika ndiyo mada iliyochaguliwa kwa ajili ya tafakari yake ya kwanza, ambao kabla alitoa ya sauti ya manabii, kisha kwa Elizabeti na ujasiri wa kutokubaliana, na hatimaye kwa Maria unyenyekevu wa kukubaliana. Manabii, wale ambao wanajua jinsi ya kuelewa kwa undani maana ya matukio ya historia, wanatuonesha sisina changamoto ambayo itakabiliwa katika kipindi cha  Majilio ya kutambua uwepo na utendaji wa Mungu katika historia na kuamsha maajabu katika uso wa kile ambacho Yeye sio tu anaweza, lakini juu ya yote bado anatamani kutimiza katika maisha yetu na katika historia ya ulimwengu.

Akisisitiza kwamba katika wakati huu liturujia inatufanya tusikilize maandiko mengi ya kinabii, Padre Pasolin alisisitiza kwamba sauti yao haiwezi kamwe kutuacha bila kujali, kwa sababu, kama Yeremia anavyodai, inaleta athari mbili ndani yetu: kuonya na kufungua kwa matumaini, kwa sababu Mungu anathibitisha uaminifu wa upendo wake na kuwapa watu fursa mpya. Haya ni maneno ambayo tunaona kuwa magumu kuyasikia, hasa sauti ya Mungu inapojaribu kufungua tena njia za matumaini”, kwa sababu kukaribisha habari njema si jambo rahisi, hasa wakati ukweli umekuwa kwa muda mrefu ukiwa na mateso, kukatishwa tamaa na kutokuwa na uhakika. Kishawishi cha kuamini kwamba hakuna kitu kipya kinaweza kutokea mara nyingi na huingia ndani ya mioyo yetu, alisisitza mhubiri huyo. Lakini sauti kama ile ya Isaya, isemayo: “Tazama, ninafanya jambo jipya; linachipuka sasa hivi, je! inatufikia hapa hapa?, ambapo tunajaribiwa kuamini kwamba ukweli hauwezi tena kutupa miali mipya ya nuru.” Changamoto basi ni kuamsha tena mshangao mbele ya kile ambacho Mungu bado anatamani kukamilisha katika maisha yetu na katika historia ya ulimwengu.

Papa Francisko katika tafakari ya Majilio
Papa Francisko katika tafakari ya Majilio

Ili kututayarisha kusikiliza sauti hizi za kinabii, Padre Pasolini alionesha mfano wa watu wawili wa kike, Elizabeth na Bikira Maria, ambao mitazamo miwili ya kimsingi imefupishwa ili kuzalisha ndani yetu nguvu ya wokovu: Elizabeti aliweza kusema ‘hapana’ kwa mwendelezo unaoonekana wa mambo na vifungo, huku kwa upande wa Maria wa Nazareti tunaona haja ya kujua jinsi ya kusema ‘ndiyo-tazama mimi hapa kwa upya wa Mungu, tukitengeneza kibali cha bure na cha furaha kwa mapenzi yake. Katika kutafakari kwake, mhubiri wa Nyumba ya Kipapa aidha alirejea historia ya  Elizabeti na mumewe Zekaria, kama ilivyoelezwa na mwinjili Luka, pamoja na kuhani mzee asiyeamini kukaribisha kwa ujasiri tangazo la tukio lililotamaniwa kwa muda mrefu, lakini labda halikuzingatiwa kuwa inawezekana ambalo nikuzaliwa kwa mtoto. Kwa sababu ya ukosefu wake wa imani, atakaa kimya mpaka kutahiriwa kwa Yohane, jina lililooneshwa na Malaika. Wakati jamaa wanauliza kwamba mtoto apewe jina la baba yake, Zaccaria, mama yake Elisabetta aliingilia kati: "Hapana, ataitwa Yohane.” Padre Pasolini alisisitiza kuwa Zakaria, maana yake Mungu anakumbuka, wakati Yohane anamaanisha Mungu anatumia rehema. Jina, ambalo linabadilisha umakini kwa leo hii, na linapendekeza kwamba historia, ingawa inaathiriwa na urithi wake, daima ina uwezo wa kushinda yenyewe na kufungua uwezekano mpya, ikiwa kuna hatua ya Mungu. Zakaria aliandika kibali chake kwa jina Yohane kwenye kibao, na kurudisha sauti yake.

Mahubiri ya Kipindi cha Majiio na Padre Pasolini(OFMCap)

Kwa njia hiyo Padre Pasolini alisema, mwitikio wa Elizabeth unapendekeza kwamba, wakati mwingine, ni muhimu kukatiza mtiririko wa mambo ili kufungua mapya ya Mungu. Leo hii kuliko wakati mwingine wowote, katika wakati usio wa kawaida katika historia ya mwanadamu  tunahitaji kurejesha aina hii ya mtazamo wa kiroho juu ya ukweli, ambapo pamoja na ukosefu mkubwa wa haki, vita na vurugu ambazo zinakumba kila kona ya dunia, uvumbuzi na njia zinazoahidi za ukombozi, alieleza Padre huyo. Kujilimbikizia jinsi tulivyo sasa, kiukweli, tunajitahidi kuwekeza katika siku zijazo na huwa na kufikiria ya kesho kama nakala ya leo. Wakati 'Hapana' ya Elizabeth, hata hivyo, ambayo inaweka hatima ya mwanawe Yohane mikononi mwa Mungu inatukumbusha kwamba hakuna chochote na hakuna mtu anayewekwa tu na historia yake binafsi na mizizi, lakini pia hurekebishwa daima na neema ya Mungu. Kuna wengi wanaosubiri kutamkwa  na sio tu wale wanaopinga maovu ya wazi, lakini pia wale wanaopinga uovu wa hila ambao ni tabia ya kuendeleza mambo bila kuwa na ujasiri wa kuyatafakari upya na kufanya hivyo pamoja.  Lakini kutamka haya  ya hapana ya ujasiri, lazima uamini kwamba Mungu anafanya kazi ndani ya historia na kwamba bora zaidi bado.

Tafakari ya <kwanza ya majilio katika Nyumba ya kipapa
Tafakari ya

Hatimaye, ili kuzungumzia itikio la Maria kwa wito wa Bwana, Padre Pasolini ali soma tena kipengele cha  Injili katika sehemu  mbayo inaweza kutusaidia kupata mshangao kidogo kuelekea fumbo la Umwilisho. Alifafanua kwamba katika Injili ya Mtakatifu Luka, kazi ya Malaika Gabrieli inaonekana kuingia moyoni mwa Maria, bila kulazimisha kwa njia yoyote, milango ya kupatikana kwake, kwa sababu mazungumzo kati yao, lazima yafanyike kwa uhuru kamili na katika hali ya kuaminiana.  Bikira anaamriwa kufurahi, yaani, kutambua kitu ambacho tayari kipo: Bwana yu pamoja naye. Na hii, ni neema ya kipindi cha Majilio, yaani, ile ya kutambua kwamba kuna sababu nyingi za kufurahi kuliko kuhuzunika, si kwa sababu mambo ni rahisi, bali kwa sababu Bwana yu pamoja nasi kwa  lolote lile ambao bado linaweza kutokea. Kwa maneno ya Malaika, hata hivyo, Maria alifadhaika sana. Kwa angalau sababu mbili, kulingana na Padre Pasolini. Ya kwanza ni kwamba mtu anapotuonesha upendo wake huwa ni mshangao. Upendo sio tukio la kutabirika na tunahitaji kujisikia kutambuliwa na kukaribishwa kwa jinsi tulivyo.  Sababu ya pili ya hofu ya Maria ni kwa sababu moyo wake unahisi kwamba wakati umefika wa kujiruhusu kufafanuliwa kikamilifu na neno la Mungu. Padre Pasolini alieleza kuwa ni kana kwamba, neno la Mungu lingeandikwa kwenye karatasi ambapo matamko mengine mengi tayari yamekusanywa na kupangwa kwa muda, yakiacha nafasi ndogo ya taarifa zaidi. Lakini katika Majilio, kungoja na kusikiliza hutufanya kweli, kuruhusu sauti ya Mungu iingie ili kusema tena kile tulicho nacho na tunaweza kuwa mbele ya uso wake.

Tafakari ya Majilio
Tafakari ya Majilio

Hatimaye, mwito wa kupata mimba isiyowezekana kulingana na vigezo vya kibinadamu unamweka Maria kwenye hatari ya kutoeleweka na mtu yeyote, kwa hakika kuhukumiwa na kila mtu kuwa mzinzi kulingana na maagizo ya Sheria ya Musa. Kwa nje ya mfano huo , Padre Pasolini, alifafanua kuwa hii ina maana kwamba kila tangazo kutoka kwa Mungu lazima liweke mtu kwenye kifo, kwa sababu lina ahadi ya maisha kamili, yaliyotolewa kabisa kwa Mungu na ulimwengu. Na hofu mbele ya aina hii ya wajibu inaweza kushinda tu kwa kuzingatia uzuri na utukufu wa kile kinachotungoja. Lakini ili kujifunua kwa haya yote hatuwezi kujiwekea kikomo kwa kusema 'ndiyo' ambazo hazitugharimu chochote na ambazo hazitunyimi chochote, alibainisha. Kila uamuzi halisi kulingana na Injili, kiukweli, hugharimu maisha yote na hutuweka kwenye hatari ya kupoteza mapendeleo na uhakika. Kusema tazama mimi hapa kwa Mungu, hutuweka kwenye hatari ya kufa katika usawa ambao tumeupata na ambao tunajaribu kubaki. Walakini, hii ndiyo njia  inayotufanya tujipate sisi wenyewe, alikumbusha Padre Pasolini.

Bikira alijibu Malaika kwa mshangao mtakatifu, akiuliza hii inawezaje kutokea, kwani sijui mwanamume?. Yeye hakutaka kuelewa mpango wa Mungu kwa undani, lakini alikuwa mshiriki ndani yake kwa njia ya bure na ya ufahamu. Na Malaika hakumweleza jinsi ataweza kumzaa  Mwana wa Mungu bali alimtangazia tu kwamba Roho Mtakatifu atakuwa mlezi wake mwaminifu. Pamoja naye: Tazama mimi ni mtumishi wa Bwana: Nitendewe kama ulivyonena, na ndiyo ya Maria  alitangaza shauku yake yote kwa wito ambao aliupokea mara moja. Ni kana kwamba alikuwa akimwambia Malaika kuwa Ulichonipendekeza nikubali, kiukweli, sasa mimi ndiye ninayetaka na ninachagua. Kwa upande wa Padre Pasolini, alisisitza kuwa matangazo yote tunayopokea katika safari ya maisha yanaweza kumalizika  kwa njia hii tu. Nuru ya Mungu inapofanikiwa kutuonesha kwamba ndani ya hofu ya kile kinachotungoja kuna uaminifu wa ahadi ya milele, ajabu hutokea ndani yetu na tunajikuta tunaweza kusema  tazama mimi hapa.

Mahubiri ya Pd Pasolini

 

06 December 2024, 17:27