Tafuta

Wamisionari na waamini wenye mapenzi mewa wanakufa kwa ajili ya kutetea imani yao katika Kristo aliyekufa Msalabani na kufufuka. Wamisionari na waamini wenye mapenzi mewa wanakufa kwa ajili ya kutetea imani yao katika Kristo aliyekufa Msalabani na kufufuka. 

Wamisionari na wahudumu 13 wa kichungaji waliuawa mwaka 2024

Mnamo mwaka 2024,kulingana na tawimu iliyothibitishwa na Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari Fides,katika ripoti yake ya kila mwaka ni kwamba: wamisionari 13 wa Kikatoliki waliuawa ulimwenguni,ambao ni mapadre 8 na walei 5.Mwaka huu pia,idadi kubwa zaidi ya wahudumu wa kichungaji waliouawa ilirekodiwa katika bara la Afrika na Amerika:watano katika mabara yote mawili.Katika miaka ya hivi karibuni,Afrika na Amerika zimepishana katika nafasi ya I katika nafasi hii ya kutisha!

Osservatore Romano

"Tunaweza kuuliza: mliwezaje kustahimili dhiki nyingi hivyo? Watatuambia yale tuliyosikia katika kifungu  kutoka Waraka wa Pili kwa Wakorintho:“Mungu ni Baba mwenye huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye ndiye aliyetufariji!” Tulichagua maneno ambayo Papa Francisko aliyotamka katika Kanisa Kuu la Tirana wakati wa Ziara yake ya Kitume nchini Albania mwaka 2014 ili kutambulisha ripoti ya kawaida ya mwaka ya Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari(Fides) kuhusu wamisionari na wachungaji waliouawa duniani mwaka 2024. Kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa muda sasa, orodha ya kila mwaka iliyopendekezwa na Fides haijumuishi wamisionari wa ad gentes tu kwa maana nzito, bali inazingatia tafsiri za mmisionari wa kike na kiume katika upeo mpana zaidi na inalenga kurekodi Wakatoliki wote wanaohusika kwa namna fulani katika kazi za kichungaji na shughuli za kikanisa waliokufa kutokana na jeuri ambalo, hata kama si waziwazi "kwa kuchukiwa imani yao.” Kwa sababu hiyo  tunapendelea kutotumia neno "mashahidi", isipokuwa katika maana yake ya asili ya "mashahidi", ili tusiingie katika hukumu ambayo Kanisa linaweza kutoa kwa baadhi yao kupitia michakato ya kutangazwa kuwa watakatifu.

Idadi

Mnamo  mwaka 2024, kulingana na tawimu iliyothibitishwa na Shirika hili la  Fides, "wamisionari" 13 wa Kikatoliki waliuawa ulimwenguni, ambao ni mapadre 8 na walei 5. Mwaka huu pia, idadi kubwa zaidi ya wahudumu wa kichungaji waliouawa ilirekodiwa katika bara la Afrika na Amerika: watano katika mabara yote mawili. Katika miaka ya hivi karibuni, Afrika na Amerika zimepishana katika nafasi ya kwanza katika nafasi hii ya kutisha. Kwa undani zaidi, jumla ya watu 6 waliuawa barani Afrika (2 Burkina Faso, 1 Cameroon, 1 Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na 2 Afrika Kusini), 5 Amerika Kusini (1 Colombia, 1 Ecuador, 1 Mexico na 1 Brazil) na 2 barani Ulaya (1 huko Poland na 1 Hispania). Kama ilivyoakisiwa na habari fulani na iliyothibitishwa juu ya wasifu wao na hali ya kifo chao, wamisionari na wachungaji waliouawa hawakuwa katika uangalizi wa kazi au ahadi za kusisimua, bali  walifanya kazi kwa kutoa ushuhuda wa imani yao katika utaratibu wa maisha ya kila siku ambayo si tu katika miktadha iliyo na vurugu na migogoro. Habari kuhusu maisha na hali ambapo vifo vya kikatili vya watu hawa vilitokea hutupatia taswira ya maisha ya kila siku, katika miktadha ambayo mara nyingi huakisiwa na vurugu, umaskini na ukosefu wa haki. Hawa mara nyingi ni mashuhuda na wamisionari ambao wametoa maisha yao kwa Kristo hadi mwisho, bila malipo.

Edmond Bahati Monja, mratibu wa Radio Maria/Goma

Miongoni mwa wahudumu wa kichungaji waliouawa mwaka  2024 pia ni Edmond Bahati Monja, mratibu wa Radio Maria/Goma, na Juan Antonio López, mratibu wa huduma ya kijamii ya kichungaji ya Jimbo katoliki la Truijllo na mwanachama mwanzilishi wa huduma ya kichungaji ya ikolojia Fungamani huko Honduras. Edmond, ambaye aliishi katika eneo la Kivu Kaskazini aliyetikiswa na kusonga mbele kwa kundi la uasi la M23, lenye silaha, aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la watu waliokuwa na silaha karibu na nyumba yake katika wilaya ya Ndosho, viungani mwa Goma, DRC. Jeshi la kawaida la Congo, ili kuongeza ulinzi wa mji huo, limefanya ushirikiano wa muda na makundi mengine yenye silaha na pia limesambaza silaha kwa baadhi ya wanamgambo wanaoitwa “Wazalendo.” Hata hivyo, kuwepo kwa makundi yenye silaha kinyume cha sheria kumeongeza uhalifu wa kivita ndani ya Goma, huku matukio ya ujambazi na mauaji yakiwa yameenea siku hizi. Kesi ya mauaji ya Edmond Bahati, inayohusika katika uchunguzi wa masuala ya ndani na makundi haya yenye silaha, pia inahusishwa na mapendo ambayo yaliendesha kazi yake. Katika muda wa miaka miwili, angalau wafanyakazi wa  vyombo vya habari wameuawa ndani na karibu na Goma. Bahati alikuwa amefanya uchunguzi kuhusu ghasia za makundi yenye silaha katika eneo hilo.

Juan Antonio López, Truijllo- Honduras

Juan Antonio López, kwa upande mwingine, alijulikana kwa kujitolea kwake kwa haki ya kijamii, na akapata nguvu na ujasiri kutokana na imani yake ya Kikristo. Uhalifu huo ulitokea saa chache baada ya mkutano wa waandishi wa habari ambapo, pamoja na viongozi wengine wa jumuiya, alishutumu uhusiano unaodaiwa kati ya wanachama wa utawala wa manispaa ya Tocoa na uhalifu uliopangwa. Mauaji ya López yanakuja huku kukiwa na ongezeko la ukandamizaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini Honduras.

Imani ya kujitoa kwa ajili ya wengine

Papa Francisko, wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana mnamo tarehe 22 Septemba 2024, alisisitiza umuhimu wa kuwalinda wale wanaotetea haki. Papa alisema: "Ninaungana  na kuomboleza na  Kanisa hilo  na kukemea aina zote za vurugu. Niko karibu na wale wanaoona haki zao za msingi zikikanyagwa na wale ambao wamejitolea kwa manufaa ya wote kwa kujibu kilio cha maskini na dunia,” Papa  aliongeza huku  akikumbuka urithi wa López “kama mtu wa imani ambaye alitoa uhai kwa ajili ya wengine.” Kuanzia  mwaka 2000 hadi 2024, jumla ya wamisionari na wachungaji waliouawa ni 608. “Hawa ni kaka na dada wanaweza kuonekana kuwa wameshindwa, lakini leo tunaona kwamba sivyo. Sasa kama wakati huo, kiukweli, mbegu ya sadaka  zao, ambayo inaonekana kufa, inakua, na kuzaa matunda, kwa sababu Mungu kupitia kwao anaendelea kufanya maajabu, kubadilisha mioyo na kuokoa watu "alisema hayo (Papa Francisko mnamo tarehe  26 Desemba 2023, katika sikukuu ya kiliturujia ya Mtakatifu Stephen shahidi wa kwanza).

Ripoti ya Fides kuhusu wamisionari na wachungaji waliouawa 2024
31 December 2024, 11:28