Miaka 30 tangu kuchapishwa kwa Waraka:'Evangelium vitae’:Maisha ni mazuri daima!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tarehe 25 Machi 2025 ni maadhimisho ya Miaka 30 tangu kuchapishwa kwa Waraka wa ‘Evangelium vitae’, yaani Injili ya Maisha uliochapishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuhusu “Thamani na maisha ya binadamu yasiyokiukwa.” Katika hafla hiyo Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha lilichapisha katika mkesha huo Machi 24, nyenzo au mwongozo kuhusu jinsi gani ya kuanzisha michakato ya kikanisa ili kuhamasisha Utunzaji wa Kichungaji wa Maisha ya Mwanadamu na ili kuyatetea, kuyalinda na kuhamasisha mwandamu katika miktadha mbalimbali ya kijiografia na kiutamaduni, katika wakati huu wa ukiukwaji mkubwa sana wa utu wa mwanadamu. Mwongo huo wenye kichwa: "Maisha ni mazuri daima," umetolewa katika Waraka huo wa Evangelium vitae, kifungu cha 31. Kwa maneno haya, Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, alitanguliza uchapishaji wa nyenzo au mwongozo muhumu.
Mwongozo wa utunzaji wa kichungaji wa maisha ya mwanadamu
Kwa upande wa mwongo huo uliochapishwa Jumatatu tarehe 24 Machi 2025, katika kesha la hafla hiyo ya miaka 30, Kardinali Kevin Farrell anaandika kuwa: "Katika wakati wa ukiukwaji mkubwa sana wa utu wa mwanadamu, katika nchi nyingi zinazoteswa na vita na kila aina ya unyanyasaji (hasa dhidi ya wanawake, watoto kabla na baada ya kuzaliwa; vijana, watu wenye ulemavu, wazee, maskini, wahamiaji) ni muhimu kutoa sura ya utunzaji halisi wa kichungaji wa maisha ya mwanadamu, ili kutekeleza kile ambacho kimeandikwa tena katika tamko la hivi karibuni la Dignitas infinita la Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kifungu cha 1. 'Heshima isiyo na kikomo, yenye msingi usioweza kutengwa katika nafsi yake, ni ya kila mwanadamu, zaidi ya hali yoyote na katika hali au hali yoyote anayojikuta.' Kwa hivyo maisha ya kila mwanaume na kila mwanamke lazima yaheshimiwe, yalindwe na kuhamasishwa kila wakati. Kanuni hii, inayotambulika hata kwa sababu pekee, lazima itekelezwe katika kila nchi, katika kila kijiji, katika kila nyumba. "Kukuza hadhi ya kila mtu misaada ni matokeo ya mazungumzo ya mara kwa mara na maaskofu:" Wapokeaji wakuu wa misaada ya kichungaji na Walinzi wa kila wakati, kwa kila mtu.
Mons. Gervasi, Mwongozo wa kuchungaji ni mazungumzo yanayoendelea na Maaskofu ulimwenguni kote
“Mwongo wa Kichungaji ni matokeo ya mazungumzo yanayoendelea na maaskofu.” Hayo yalisemwa na Monsinyo Dario Gervasi, Katibu Mkuu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, akipendekeza jinsi ya kutumia njia ya kisinodi ya utambuzi katika roho kuhusu mada nyingi zilizounganishwa na maisha ya mwanadamu na njia za kutetea, kulinda na kukuza katika muktadha mbali mbali wa kijiografia na kitamaduni.
“Wapokeaji wakuu wa Mwongozio huo wa Kichungaji ni maaskofu ambao, wakati wa ziara zao za mara kwa mara (Ad Limina mjini Vatican), daima walisisitiza uharaka wa kujitolea upya kulinda na kukuza maisha na utu wa kila mwanadamu.” Katika mkutano wa wavuti ulioandaliwa na Baraza ka Kipapa hilo mnamo 2024 na wakuu wa Tume za Familia na Maisha za Mabaraza ya Maaskofu ulimwenguni kote, mchakato wa pamoja wa kukuza Utunzaji wa Kichungaji wa Maisha ya Mwanadamu ulianzishwa, kwa kuzingatia mwongozo wa hivi karibuni uliotolewa na Waraka wa Dignitas infinita. "
Unaweza kupakua mwongozo huo kupitia tovuti:www.laityfamily.va
Ili kuunga mkono mchakato huu, Mfumo wa Kichungaji unatoa pendekezo ambalo pia linapendekeza jinsi ya kutumia mbinu ya kisinodi ya utambuzi katika Roho kuhusu masuala mengi yanayohusiana na maisha ya binadamu, pamoja na njia za kutetea, kulinda, na kukuza katika maeneo mbalimbali ya kijiografia na mazingira ya kiutamaduni. Monsinyo Gervasi aliendelea: “Katika mazungumzo ya pamoja, lengo ni kuunga mkono safari ya kila Jimbo ili waweze kuwekeza rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya malezi yenye ufanisi zaidi ya walei na kuongeza uelewa miongoni mwa vizazi vijana kuhusu thamani ya maisha ya binadamu.”
Mwongozo ulilochapishwa kwa lugha tatu unapatikana katika Tovuti ya Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha hapa: www.laityfamilylife.va. Kama tulivyosema hapo awali mwongozo huo unatoa mbinu iliyosasishwa ili kukuza Utunzaji wa Kichungaji wa Maisha ya Mwanadamu kwa njia iliyoenea katika majimbo ulimwenguni. Kwa ajili hiyo, Kanisa linamtia moyo kila Askofu, Padre, mwanamume na mwanamke mtawa, na walei kusoma Mwongozo huu wa Kichungaji, na kujitahidi kuendeleza Utunzaji wa Kichungaji wa Maisha ya Mwanadamu, ambao unaweza kuwapa wafanyakazi, waelimishaji, walimu, wazazi, vijana na watoto malezi sahihi ya kuheshimu thamani ya kila maisha ya mwanadamu.